TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

TANZIA Zanzibar: Salim Turky, Mwanasiasa Mkongwe na Mgombea Jimbo la Mpendae Zanzibar, afariki dunia

Mwenyezi Mungu amrehemu Mh. Salim Turky apumzike kwa amani. Kitendo cha kukodi ile ndege iliyompeleka Lissu Nairobi baada ya kukoswakoswa kuuwawa ni ubinadamu uliopitiliza. Lissu anapaswa kuahirisha kampeni zake akamzike huyu shujaa.
 
Rip Mzee Turku, huyu mzee alisaidia kulipia ndege ya kumsafirisha lissu kwenda Nairobi, mashetani yalipo mshambulia kwa risasi 38
Mzee Turky alifanikisha upatikanaji wa ndege ya kumsafirisha Lissu kwenda Nairobi ikiwa ni pamoja na udhamini, lakini malipo ya ndege yalifanywa na Chadema.
 
Lissu Hana shukrani aliendelea kuponda CCM hata Kama walimsaidia. Mbowe mwongo hakutoa chochote Hadi turky akawasaidia ndege ya rafiki zake akawahishwa Nairobi kwa matibabu zaidi Hadi leo kapona kwa msaada wa Wana CCM. Turky alitoa ndege alikuwa mbunge wa CCM chadema mlikuwa wapi?
Siyo mahali pake kwa sasa. Uccm hadi kwenye misiba? Tabia hii mtakoma lini?? Ndiyo maana mageuzi ya kimfumo ni muhimu sana kwenye nchi yetu kwa sasa.
 
R I P Bilionea, Mgombea na kada wa CCM ndugu Salim Turkey.
 
Lissu aliposhambuliwa Watanzania wengi (wakiwemo CCM, CDM, CUF, ACT, wasio na vyama ,nk, akina Ndugai, Tulia, Ummy, Turky, nk) wali-react naturally kibinadamu kama binadamu mwadilifu anavyo-react kwa matukio ya nmana hiyo: walisikitika na kila mmoja akitafuta jinsi gani ya kuokoa maisha ya mhanga huyo! Ilikuwa ni baada ya siku chache bosi wao alipoonesha bila kificho kuwa hakufurahia kunusurika kwa mtu huyo, ndipo walipoanza nao kulazimisha moyo wa kishetani (ili wasipoteze ulaji wao) hadi kufikia kumfanyia dhihaka na hatimaye kumvua ubunge wake. Kumbuka kuwa ni Bw. Nyalandu mwana CCM pekee aliyesema liwalo naliwe nitaendelea kuonesha kujali na kulaani udhalimu huu, na matokeo yake ilibidi aondoke CCM!! Duniani kuna binadamu wanyama, ambao kila Jumapili au Ijumaa hutaka public iwaone kuwa ni watu wa Mungu lakini ni wanyama, ni wanyama, ni wanyama. Huwa natamani Mungu awape adhabu wakiwa bado hapa hapa duniani.
Ubinadamu hauna siasa.
 
Mengi, Mafuruki, Turky, Manji(kafa kisaikolojia baada ya kupewa kesi), Mo (kafa kiuhuru tangu atekwe), Rostam ( kafa kiuhuru tangu mdogo wake apewe kesi), Seth na Rugemalira ( Wao gerezani) Lowasa na Sumaye ( walishajisalimisha), Dialo ( anapumulia mashine) ZAKARIA (huyu ni mwanaume wa Tarime...).

Kwa kifupi MATAJIRI AIDHA WAISHI KAMA MASHETANI AU WAREST IN PEACE!

"hapa kazi tu".
 
Back
Top Bottom