matonyamswanu
JF-Expert Member
- Dec 7, 2025
- 358
- 433
Watanganyika Kama mmeshindwa kulinda mali, na rasilimali zenu, kwa nini wasijibebee bure?Kwa muda mfupi Zanzibar imeweza kukarabati Amani stadium kwa viwango vya FIFA, imejenga kiwanja kipya cha Gombani, Tanganyika yenye watu 60m tumeshindwa kumalizia kiwanja kimoja cha Arusha hadi tuombe mkopo.
Tanzania ni mwenyeji wa AFCON 2027, kiwanja tunachokitegemea ni Benjamin Mkapa nacho kila siku kipo kwenye marekebisho. Kiwanja cha Arusha tuliambiwa (kisiasa) kipo kwenye finishing touches, nimekuja kukiona kumbe ni skeleton tupu.
Tuna-feli wapi.
New Amani Complex
View attachment 3542670
Gombani Stadium
View attachment 3542671
Arusha Complex
View attachment 3542673
Na bado watakomba kila kitu. Dhahabu hiyo imeenda, bandari tayari ya kwao, wamasai wamefurushwa na wanyama wanabebwa, ardhi wananunua watakavyo.

