Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Watanzania sasa tumekuwa kama watu wa mataifa makubwa ya democracy yaani hata kiongozi akienda kombo(kinyume) basi huwa hatubabaiki huwa tunatoa ukweli mtupu
 
Ukweli siku zote haufichiki
 
Kila hotuba lazima ilete taharuki na sintofahamu sasa sijui ndio style au nini?!...
 
... anapwaya mno kihekima ukilinganisha na watangulizi wake.
 
Naombeni kujua tu "mtukufu" hana washauri au haandaliwi hotuba? Mimi si mchochezi,kwa nia nzuri tu nataka kujua
 
Magufuli ni mtu wa matani sana, sema watu hawajazoea utani wa usukumani ndio maana wanapata nae shida.
 


Acha uongo kila mtu anajuaje CUF walishinda wakati kura hazikuhesabiwa zote na tume haikutangaza matokeo? Mtu kujitangazia kuwa ameshinda ndiyo unataka kuaminisha watu kiupotofu kuwa CUF ilishinda? Endelea kuota ndoto bandia ambazo hazitakuja kutimia.
 
Mtu anaota usiku ana......
Kumbe kwny kuota vya usiku sote tunaota hajalishi kabwela au Kiongozi.
 
'Mlivyokuwa Wajinga mkamkanyaga Mh. Mbarawa kwenye Uchaguzi sasa na Mimi kwa kuwaonesha nimekusanyaWizara Nyeti tatu nikamkabidhi aziongoze'-Mtu wa Watu

Mie napenda sana hotuba za Mh. Rais Magufuli kwa kuwa znatoka Moyoni kwake kabisa, Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu.

Hotuba za Jakaya nyingi zilikuwa anasoma Jakaya Mwenyewe baada ya January Makamba kuzihariri na kuhariri
 
Nani alikwambia kura hazikuhisabiwa zote? Kuhusu nani kshinda ni suala jengine lakini kura zilikwisha hisabiwa, usiite watu waongo bure kwa ignorance yako!

Mbona uchaguzi wa marejeo matokeo siku ya pili tu yalitangazwa? Usiwe mjinga wewe ukafanya watu wote wajinga. Bakia na denial concious yako mwenyewe ujifurahishe nafsi yako.
 
Hotuba murua itatoka leo ya kujenga na kuimarisha Muungano
Bado unaamini hotuba iliyotoka ni ya kuimarisha na kujenga umoja?sio kwa vitisho vile,Rais kujiona mungu MTU!Hata the most powerful man on earth,Barack Obama hajawahi kuongea kwa vitisho namna hii!
Rais anahutubia,wananchi tunaona aibu kwa matamshi yake yasiyo na busara wala hekima!
 
Hapo alikuwa anawakomoa akina nani sasa
 
Haya basi tujiaminishe kuwa ilikuwa ni hotuba iliyoeleweka na kupendwa na wapemba
 
Mtu anaota usiku ana......
Kumbe kwny kuota vya usiku sote tunaota hajalishi kabwela au Kiongozi.
Alitaka kusema ndoto bhana,"hata kama ni mwanaume unaweza ota ni ......(japo hakusema ila alitaka kusema mwanamke),akasita akaona hapa nitakuwa natukana,akaendelea "hata kama ni mwanaume unaweza ota unacheza mpira"
Kwa mwenye kuelewa kiswahili ameelewa nini ngosha alikusudia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…