Zanzibar yatangaza maambukizi mawili huku wote wakitokea Tanga na kuingia Zanzibar

Zanzibar yatangaza maambukizi mawili huku wote wakitokea Tanga na kuingia Zanzibar

kuanzia tarehe 13 na 18 walikuepo zanzibar so kunauwezekano pia maambukizi wameyapata wakiwa zanzibar. afu ni aibu kwa waziri mzima kusign barua hajaisoma vizuri angeisoma vizuri angeomba wabadili kwanza tarehe leo ni tarehe 5 april na sio tarehe 5 march ndo uone jinis wakiwa wanasign mikataba wanavosign tu bila kusoma contents
Watu wa aina yako wamebaki wachache nchi hii.

Sijui kama siku za mbeleni tutajirekebisha, au ndio hivyo tena tunaelekea madongo kwinama.
 
Halafu Wakuu wa mikoa ya Dar na Arusha wanazidi kuambukiza watu kwa kushawishi misongamano kwenye kampeni zisizo rasmi
 
Kwahiyo sasa tuanze kuwaamini wanaosema takwimu zinazotolewa na wizara ya Afya sio za kweli, kwasababu hao wagonjwa wawili wakiwa Tanga hawakutambulika.

Na hii maana yake nini Makonda anavyotuambia tukafanye kazi, alikuwa anayajua haya, au aliongea tu kama kawaida yake?!

Sasa ndio ajifunze, aache kukusanya watu hovyo kwenye vituo vya daladala, atasababisha maambukizi yaongezeke, bora na yeye ajifungie ndani kwa usalama wake, aache ujuaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasipotambulika watawekwaje kwenye idadi ya wagonjwa, na Kwa nini wenye Dalili za maambukizi hawataki kujitokeza, huu nao ni uuwaji tu, mtu unajua unazo Dalili zote bado unajifungia, mbona tunaipa kazi nzito Serikali?
 
IDADI YA WAGONJWA WA COVID19 WAONGEZEKA Z’BAR

Wizara ya Afya Zanzibar imetangaza wagonjwa wapya wawili wa maambukizi ya virusi vya #Corona na hivyo kufanya idadi ya waliopata maambukizi hayo kufikia saba.

Wagonjwa hao wapya wote ni Watanzania, wanaume wenye miaka 33 na 27 na waliingia Zanzibar wakitokea Tanga.

View attachment 1409432
View attachment 1409430
View attachment 1409431
Sasa hapo Tanga, kwenye maboti ya kwenda Zanzibar watu wote waliokuwemo kama wamepata hata robo tu ya idadi utakuwa balaa
 
Wasipotambulika watawekwaje kwenye idadi ya wagonjwa, na Kwa nini wenye Dalili za maambukizi hawataki kujitokeza, huu nao ni uuwaji tu, mtu unajua unazo Dalili zote bado unajifungia, mbona tunaipa kazi nzito Serikali?
Mkuu sisi waafrika sijui tunakwama wapi unakumbuka Ukimwi ulipoingia halafu watu wakawa wanauambukiza kwa makusudi "ati kilio cha wengi ni harusi" sasa hivi naona korona nayo watu wanasema usipoijua unapona ukijitambua unavuta kwa kihoro.
 
kama ni tarehe 13 na tarehe 18 hapa kuna watu wana makonda disease, yaani kwa hizo tarehe watu wanamuota makonda. Huyu wa tarehe 13 ameishi Zanzibar kwa Siku 18 na huyu wa tarehe 18 ameishi Zanzibar kwa siku 13 na ugonjwa inadaiwa unaoneka ndani Siku 14. Hapa habari ya kumlaumu Makonda inatokea wapi? Inaonekana kuna watu wanatamani kusikia kila siku wagonjwa wanaonekana kwa mamia, Ea Mungu tusaidie.
 
Usikute barua iliandikwa March waziri ndiyo kaisoma leo hizi taasisi zetu zina mapungufu mengi mojawapo ni uzembe
kuanzia tarehe 13 na 18 walikuepo zanzibar so kunauwezekano pia maambukizi wameyapata wakiwa zanzibar. afu ni aibu kwa waziri mzima kusign barua hajaisoma vizuri angeisoma vizuri angeomba wabadili kwanza tarehe leo ni tarehe 5 april na sio tarehe 5 march ndo uone jinis wakiwa wanasign mikataba wanavosign tu bila kusoma contents

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila shaka hao watakuwa wameupata wakiwa Zanzibar, hii ina maana Zanzibar serikali iwafuatilie kwa haraka sana hao waliokuwa wanakaa na hao wawili, mamaaaaa, itakuwa imeingia mitaani nn, duh🐙😥
 
Huko Tanga walikotoka wameambukiza watu wangapi? Naona tunacheza na moto aiseee...
Serikali makini inafatilia na kuwaweka quarintine watu wote waliokuwa na uhusiona wa karibu na wagonjwa.
 
Back
Top Bottom