Huyu mama ni mzuri kikweli ila ukiangalia ile video yake alipokuwa anampokea Diamond, halafu ukasoma background yake kwa kina unaweza kubaki unajiuliza maswali mengi sana kumhusu. Kwenye video alipokuwa akiongea alionekana tofauti na wakati alipopozi kupigwa picha; anapopozi kwa picha anakuwa mzuri sana wakati anapoongea anaonekana wa kawaida tu.
Background yake inaonyesha kuwa amekuwa anabadilisha wanaume kwa muda mrefu sana na mara zote amekuwa na ugumu wa kuwakeep; unashindwa kuelewa kwa nini wanaume wanampitia na kumwacha kwa muda mfupi. Hata mme wake waliyekaa pamoja kwa miaka kumi na nne na kuzaa watoto pamoja na kumsomesha na kumpa mali zote zile alizo nazo leo bado amekuwa hana penzi la dhati naye.
Magazeti ya Uganda nayo yanavyomwandika na jinsi wanaume waliompitia wanavyomchambua, nadhani inachangia sana kumfanya awe stressed na kuwa desperate kupata mwanamme wa kumtuliza; stress hizo zinaonekana usoni akiwa anaongea. Kulikuwa na ripoti ya kuwa alikuwa anakaribia breakdown kuhusu uandaaji wa pati hii kwa vile mme wake alikataa kumsapoti mwaka huu.
Hivyo kwake kumpata Diamond ilikuwa ni boost kubwa sana ambayo ni lazima atakuwa anamheshimu sana. Nadhani atakuwa na amani kidogo na Diamond katika kipindi hiki kwa vile watakuwa wanakutana mara moja moja na kujituliza, siyo ile ya kuwa beneti muda mwingi.
Hata hivyo Diamond atatakiwa pia awe msiri wa mambo yake mengine kwani huyu mama anajulikana kwa kuwa na wivu na hasira za haraka; ambayo ni tabia ya kawaida kwa wanawake wengi wa Libra.
Kwa wanaume wanaomkosoa Diamond nadhani siyo wakweli; hakuna mwanamme wa umri wa Diamond angeweza kuparamiwa kwenye ndege na manamke wa aina hii halafu akampuuzia. Mwacheni Diamond atumie ujana wake;
wote wawili wana rekodi zinazofanana kwa hiyo huenda watajuana vizuri sana. Wakishindwana wataachana kama ilivyokuwa kwa wengine waliowapitia.