Zelensky: Tumewapa hasara kubwa hurusi

Vita ni hasara nzito mno. Hapo hujaweka yale magari vita, ila kwa vifaru hakika putin wamemtia hasara, kwenye ile meli ndo kabisaaa.
 
Bado hujakua mdogo wangu, ukikua na ukawa umeenda shule vizuri huwezi kuwa na option nyingine zaidi ya kulinda nchi yako.
 
Upo sahihi kabisa, hii ngoma ilipangwa muda tu. Kwasasa kinachofanyika ni utekelezaji, ni mjinga pekee atakayeweza mlaumu zele.
 

Zelensky ni kjiana fulani mpuuzi amepewa madaraka.

Hajui nnii maana ya madaraka.Ni hivi kuwasaidia watu wako, hasa wa chini. Ndio wengi.
 
Nilikuwa najua ni mtata ktk vita ila sikujua kama ni kichaa kiasi hiki, UK hakamatiki ktk hii vita.
 
Bado hujajumlisha USD 600B za russia zilizopigwa pini westerns.
Ww tumia akili, there is a big difference between natural resources na pesa,unaweza kutumia natural resources kuzalisha hiyo USD 600B,na vizazi vyote vikaendelea kuishi kwenye hiyo ardhi. Hiyo pesa ni ndogo Sana,kumbuka maeneo yaliyochukuliwa na Urusi ndio uchumi wa Ukraine upo. Usiandike kishabiki ww
 
Unajua akili ni mali sana Yani unacho msifia Ukraine ni sababu tu Kyeiv haikuchukuliwa? Mwenye akili anajua wazi wanaye pigana na Mrusi ni NATO na USA Kwa kutumia uwanja wa Ukraine. Mwenye akili hawezi kubali nchi yake irudishwe nyuma miaka 30 na watu wake wengine sasa ni maomba omba. Hebu we kwanza jibu Ukraine kapata nini tokea vita kuanza? Mrusi Kisha imeza Mashariki na sidhani kama ataikomboa kiulaini. Mrusi hio Kyeiv anaitwanga Kila akiamua
 
Umeongea point nzuri Sana, jamii za wenzetu hazimpi mtu mmoja kuamua anvyotaka yeye. Right kama zelenesky angekuwa mjinga nguvu ya umma ingemuangusha. Wakati Russia anaanza operation yake alitoa amri kuwa wanaume wenye nguvu wasiikimbie nchi na wao waliitika, civilian walijiunga na mafunzo ya kujilinda ili kukomesha uonevu wa Russia. Warusi wao sio Malaika watu wafahamu hata wao wanaweza kuwa waonevu kama mabeberu.
 
Vuta picha kijana alomjibu hapo juu ndo anakuwa kiongozi wa nchi au familia, si aibu hii? Mwanaume unapaswa kuwa na ujasiri hasa. Ukiona kabisa hiki hakiwezekaniki sema hakiwezekaniki na sio kuanza maongezi.

Demand ya Russia kwa Ukraine ilikuwa ni kubwa mno, na ni ya muda mrefu, maana yake kuwa hata wale waliopita hawakumuunga mkono putin juu ya matakwa hayo.
 
Drop down to this example, Jirani yako akizusha ugonvi na wewe, akakupa sharti la kuikabidhi familia yako ( mke na watoto), utakubali au utasalimisha familia yako kwake? Utapigana nae au utakimbia? Acha uzembe wa kufikiri mzee baba
Asamehewe huyu kijana nikwaida kuwa na watu wenye inferiority complex. Kuna watu niwaoga kiasi cha kushindwa hata kuua panya licha kuvamia nyumba na kula nafaka.
 
Kama Ukraine ndo ingekuwa UK au France au German, pasipo Nuclear, sasa hivi putin angekuwa mafichoni.
 
Inakuwaje anayejifanya anashinda vita ndiyo analialia kila siku?
 
Sasa mimi na wewe nani asiyetumia akili, kila natural resources itakulipa sawasawa na matakwa yako? Hizo sehemu aizoshika ndo zitafanya Ulaya irudi kununua gas kwake? Hiyo sshemu ataishika milele?
 
Kwahiyo mpaka sasa hajaamua kuitwanga? Kwanini alipoenda alirudi nyuma? Laiti mngejua ninyi ndo hamtumii akili wala usingetamka yote hayo. Ulitaka Ukraine atii masharti ya Urusi kirahisi tu si ndio?
 
Kama Ukraine ndo ingekuwa UK au France au German, pasipo Nuclear, sasa hivi putin angekuwa mafichoni.
Back in history, russia na German waliwahi kuivamia Poland kuna upande wa mashariki walitolewa kamasi kidogo, unfortunately Hitler aliwatwanga wakasalimu amri. Kwenye hii vita beberu anamkono mrefu Sana, kuna paper zimechambua udhaifu wa vifaru vya urusi ambavyo vimeteketea kwelikweli. Yaani St javelin imeviharibu kinoma kikipigwa juu kinaungua chote
 
Kuna masilaha yanapelekwa huko Ukraine kutoka kwa mabeberu, tutasikia ya kusikia siku za mbeleni ila ile Mariupol itakombolewa siku za mbeleni.
 
Inakuwaje anayejifanya anashinda vita ndiyo analialia kila siku?
Hiyo ni mbinu pia ya mapambano, akilia mnamuona kama weak ila kumshika haiwezekani. Anajua hana uchumi wa kutosha kupambana na Russia, kwahiyo kuomba msaada sio vibaya, mbona uganda aliomba msaada kwa Gadaffi, Mozambique, South Afrika, visiwa vya comoro havikuwahi kuomba msaada? Rais kuba msaada kulinda mipaka ya ardhi kupitia vita ni kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…