Zelensky: Tumewapa hasara kubwa hurusi

Zelensky: Tumewapa hasara kubwa hurusi

Mkuu unajua gharama ya kifaru kimoja cha urusi jaribu hata kugoogle ,kifaru kimoja ni billion 23 za kibongo ,sasa linganisha kifaru kimoja kinatoa gorofa ngap,hapo hujapigia gharama za helicopter, ndege,magar,na vifaa vingine tatizo wabongo mnajua kifaru ni bei ya vits.hapo sijajumuisha gharama za ile meli ya kisasa,vikwazo ,na asett zote ambazo ziko freezing zimetaifishwa
Vita ni hasara nzito mno. Hapo hujaweka yale magari vita, ila kwa vifaru hakika putin wamemtia hasara, kwenye ile meli ndo kabisaaa.
 
Hayo yooooote uliyoyaandika niliyaona pengine hata kabla hujayaona lakini nimechagua kumpuuza maana kama angekuwa na akili japo kidogo asingeweka rehani maisha ya wanançhi wake kwa faida ya Marekani na washirika wake! Ninachosema ni kwamba, angekuwa na akili pasingekuwa na vita!
Bado hujakua mdogo wangu, ukikua na ukawa umeenda shule vizuri huwezi kuwa na option nyingine zaidi ya kulinda nchi yako.
 
Kikubwa tunaona kama Zelensky anapigana
Lkn ni pressure kubwa anayoipata to kwa Marekani
Marekani ndo mpango mzima na waliipanga hata kabla Mccain hajafariki
Hapo ni timing inatafutwa
Mrusi si Afghanistan,Zelensky yuko mtu kati anatumika na hana ujanja hata kiduchu

Ipo video Mccain na kiongozi 1 wa US wakiongea na wanajeshi wa Ukraine na kuwaahidi watawapa kila aina ya silaha na support yote ili kupigana Urusi

Imegoma tu kupanda hapa
Upo sahihi kabisa, hii ngoma ilipangwa muda tu. Kwasasa kinachofanyika ni utekelezaji, ni mjinga pekee atakayeweza mlaumu zele.
 
Ukrainian President Volodymyr Zelensky said the Ukrainian army has already destroyed more than 1,000 Russian tanks, nearly 200 Russian aircraft, and almost 2,500 armored fighting vehicles.

Despite these losses, Russian troops still have equipment to launch additional attacks, Zelensky said.
Source CNN today 1/05/2022
Kama kuna kaukweli basi urusi kazi wanayo,huwenda ikawa ndio .maana wamekimbia kiaina wakidai lengo lao ni East.

Zelensky ni kjiana fulani mpuuzi amepewa madaraka.

Hajui nnii maana ya madaraka.Ni hivi kuwasaidia watu wako, hasa wa chini. Ndio wengi.
 
Mkuu acha jazba Ukraine hawakutaka vita kabla wao walivamiwa walilala asubuhi wakaamkia mabomu kila upande ndio wakaanza kujilinda, hata wewe ukishambuliwa lazima utaumia kwa sababu hukujua adui anaanza wapi., tunawashangaa Russia ambao tumeaminishwa kwenye masikio yetu kwamba Mrusi hataki mchezo sijui ana hichi na hichi leo nikisomewa hasara aliyoipata kwenye hiyo operation ni aibu kubwa kwake, na wengi tumepata kujua na kujifunza kumbe Russia ilijenga heshima ya woga na kimchongo kwamba ni taifa kubwa kivita kumbe hata Ruwanda anaweza kusimama naye kwenye vita.

Marekani baada ya kumjua udhaifu wake sasa kashapewa majibu kama anataka vita na Marekani aanze wao marekani hawataacha kuipa silaha Ukraine kumshughulikia Putin, kabla putini alionya sasa kashapewa jibu kwamba hawatasita kuipa silaha Ukraine lakini na Ujerumani wamejibu pia kwamba ndani ya Ukraine kuna jeshi lao linatoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine yoote hayo kaambiwa putini wa mchongo sasa kama ni mwaname arushe japo jiwe kule Washington maana kila kitu sasa keshaekewa wazi.

Meli yake ya kivita iliripuliwa ni muingereza na anajua kila siku anasogeza vinu vya nuclear lakini ana kitetemeshi kupiga huko ulaya ama Marekani kwanini?
Nilikuwa najua ni mtata ktk vita ila sikujua kama ni kichaa kiasi hiki, UK hakamatiki ktk hii vita.
 
Bado hujajumlisha USD 600B za russia zilizopigwa pini westerns.
Ww tumia akili, there is a big difference between natural resources na pesa,unaweza kutumia natural resources kuzalisha hiyo USD 600B,na vizazi vyote vikaendelea kuishi kwenye hiyo ardhi. Hiyo pesa ni ndogo Sana,kumbuka maeneo yaliyochukuliwa na Urusi ndio uchumi wa Ukraine upo. Usiandike kishabiki ww
 
Naona kama wewe ndo ungenyamaza kimya chief, yeye ana haki ya kujitapa.

1. Anatetea kiapo chake cha kulinda Ukraine.
2. Yeye ndo amevamiwa na sio kwamba amevamia.
3. Ukubwa wa jeshi la Urusi mpaka sasa ameweza kuwadhitibiti kwa sehemu Kyiv isichukuliwe.
4. Operation toka siku 3 mpaka sasa umeingia mwezi wa 3, ongera kwake kwa ujasiri huu.
5. Ameshambulia sehemu kadhaa kwa udogo Russia, na amepiga mpaka meli bora kabisa ya kisasa ya Kirusi yenye mifumo ya S300 defence system. Jamaa kajihidi mno.
6. Amedhihirisha kuwa russia wamemtia hasara sababu inaonekana hasara amepata yeye tu ila kumbe hata Russia amepata.
7. Amefanya ulimwengu ujue mrusi kuna mda mikwara mingi kama msukuma aloshinda tatu mzuka milioni 5 kumbe vitendo hamna kitu.

Mwisho kabisa huu ndo uanaume, sio unavamiwa na baunsa unakuwa mnyonge kumtoa mkeo na familia, mwanaume lazima upambane.
Unajua akili ni mali sana Yani unacho msifia Ukraine ni sababu tu Kyeiv haikuchukuliwa? Mwenye akili anajua wazi wanaye pigana na Mrusi ni NATO na USA Kwa kutumia uwanja wa Ukraine. Mwenye akili hawezi kubali nchi yake irudishwe nyuma miaka 30 na watu wake wengine sasa ni maomba omba. Hebu we kwanza jibu Ukraine kapata nini tokea vita kuanza? Mrusi Kisha imeza Mashariki na sidhani kama ataikomboa kiulaini. Mrusi hio Kyeiv anaitwanga Kila akiamua
 
Ujinga wake ni kuongoza Vita vya kuwaondoa wavamizi kwenye taifa lake ?....angekaa kimya mngembeza na kumuita dhaifu na mnyonge bora akomae tu.


Rais Ronald Reagan alikuwa pia msanii ila ndiye aliyeiangusha na kuisambaratisha USSR iliyokuwa kubwa yenye kutisha kuliko Urusi ya sasa,hii kauli ya kujumuisha 'wote' ni makosa.
Umeongea point nzuri Sana, jamii za wenzetu hazimpi mtu mmoja kuamua anvyotaka yeye. Right kama zelenesky angekuwa mjinga nguvu ya umma ingemuangusha. Wakati Russia anaanza operation yake alitoa amri kuwa wanaume wenye nguvu wasiikimbie nchi na wao waliitika, civilian walijiunga na mafunzo ya kujilinda ili kukomesha uonevu wa Russia. Warusi wao sio Malaika watu wafahamu hata wao wanaweza kuwa waonevu kama mabeberu.
 
Umeongea kwa hisia bila logic, punguza mihemko kisha leta nondo za kueleweka. Russia alianza kupika propaganda kitambo kuwa ( ukraine is an artificial country ) so iko chini ya kivuli cha Russia, stalini aliwahi kuwasulubu ukraine kwa kuwanyanganya mashamba then wakadead kama million nne na kidogo. Mgogoro huu umeanza tangu 2014 mpaka inatokea leo. Ukraine sio wajinga wamekaa sana kwenye meza ya maridhiano lakini imeshindikana. Kuna watu wanajali hadhi na heshima ya taifa leo. Kama kiongozi wao angekuwa amekosea nguvu ya umma ingemuondoa hata kabla ya Russia kuvamia. Niukweli mchungu Russia amekosa ushawishi ndani ya ukraine ndio maana raia na jeshi hawajaogopa military superiority yake wameamua zichapwe. Kusurrender tunaweza sisi tu ambao mkuu wa mkoa anaweza kutukataza mjini bila kuoga ila wenzetu wana nguvu za kiume kwelikweli ( strong balls ).
Vuta picha kijana alomjibu hapo juu ndo anakuwa kiongozi wa nchi au familia, si aibu hii? Mwanaume unapaswa kuwa na ujasiri hasa. Ukiona kabisa hiki hakiwezekaniki sema hakiwezekaniki na sio kuanza maongezi.

Demand ya Russia kwa Ukraine ilikuwa ni kubwa mno, na ni ya muda mrefu, maana yake kuwa hata wale waliopita hawakumuunga mkono putin juu ya matakwa hayo.
 
Drop down to this example, Jirani yako akizusha ugonvi na wewe, akakupa sharti la kuikabidhi familia yako ( mke na watoto), utakubali au utasalimisha familia yako kwake? Utapigana nae au utakimbia? Acha uzembe wa kufikiri mzee baba
Asamehewe huyu kijana nikwaida kuwa na watu wenye inferiority complex. Kuna watu niwaoga kiasi cha kushindwa hata kuua panya licha kuvamia nyumba na kula nafaka.
 
Wananchi wa ukraine wanajua aggressive character kuliko wewe, una feel pity na wananchi wa ukraine wenyewe. Walijua Russia angewavamia siku moja ndio maana walianza kutoa mafunzo kwa raia wake mpaka vibibi kizee. Ukraine ni taifa la wanaume waukweli hawataki dharau kama alichowafanyia Stalin kuwanyanganya mashamba, rais wao pia ni mwanaume sio mzembe kukubali kubaki nchini kwake akiendelea kutoa amri za mapambano. Hii vita Russia asipoangusha huu utawala , jamaa watajijenga sana wakishirikiana na wazee wa faida aka mabeberu.
Kama Ukraine ndo ingekuwa UK au France au German, pasipo Nuclear, sasa hivi putin angekuwa mafichoni.
 
Ukrainian President Volodymyr Zelensky said the Ukrainian army has already destroyed more than 1,000 Russian tanks, nearly 200 Russian aircraft, and almost 2,500 armored fighting vehicles.

Despite these losses, Russian troops still have equipment to launch additional attacks, Zelensky said.
Source CNN today 1/05/2022
Kama kuna kaukweli basi urusi kazi wanayo,huwenda ikawa ndio maana wamekimbia kiaina wakidai lengo lao ni East.
Inakuwaje anayejifanya anashinda vita ndiyo analialia kila siku?
 
Ww tumia akili, there is a big difference between natural resources na pesa,unaweza kutumia natural resources kuzalisha hiyo USD 600B,na vizazi vyote vikaendelea kuishi kwenye hiyo ardhi. Hiyo pesa ni ndogo Sana,kumbuka maeneo yaliyochukuliwa na Urusi ndio uchumi wa Ukraine upo. Usiandike kishabiki ww
Sasa mimi na wewe nani asiyetumia akili, kila natural resources itakulipa sawasawa na matakwa yako? Hizo sehemu aizoshika ndo zitafanya Ulaya irudi kununua gas kwake? Hiyo sshemu ataishika milele?
 
Unajua akili ni mali sana Yani unacho msifia Ukraine ni sababu tu Kyeiv haikuchukuliwa? Mwenye akili anajua wazi wanaye pigana na Mrusi ni NATO na USA Kwa kutumia uwanja wa Ukraine. Mwenye akili hawezi kubali nchi yake irudishwe nyuma miaka 30 na watu wake wengine sasa ni maomba omba. Hebu we kwanza jibu Ukraine kapata nini tokea vita kuanza? Mrusi Kisha imeza Mashariki na sidhani kama ataikomboa kiulaini. Mrusi hio Kyeiv anaitwanga Kila akiamua
Kwahiyo mpaka sasa hajaamua kuitwanga? Kwanini alipoenda alirudi nyuma? Laiti mngejua ninyi ndo hamtumii akili wala usingetamka yote hayo. Ulitaka Ukraine atii masharti ya Urusi kirahisi tu si ndio?
 
Kama Ukraine ndo ingekuwa UK au France au German, pasipo Nuclear, sasa hivi putin angekuwa mafichoni.
Back in history, russia na German waliwahi kuivamia Poland kuna upande wa mashariki walitolewa kamasi kidogo, unfortunately Hitler aliwatwanga wakasalimu amri. Kwenye hii vita beberu anamkono mrefu Sana, kuna paper zimechambua udhaifu wa vifaru vya urusi ambavyo vimeteketea kwelikweli. Yaani St javelin imeviharibu kinoma kikipigwa juu kinaungua chote
 
Umeongea point nzuri Sana, jamii za wenzetu hazimpi mtu mmoja kuamua anvyotaka yeye. Right kama zelenesky angekuwa mjinga nguvu ya umma ingemuangusha. Wakati Russia anaanza operation yake alitoa amri kuwa wanaume wenye nguvu wasiikimbie nchi na wao waliitika, civilian walijiunga na mafunzo ya kujilinda ili kukomesha uonevu wa Russia. Warusi wao sio Malaika watu wafahamu hata wao wanaweza kuwa waonevu kama mabeberu.
Kuna masilaha yanapelekwa huko Ukraine kutoka kwa mabeberu, tutasikia ya kusikia siku za mbeleni ila ile Mariupol itakombolewa siku za mbeleni.
 
Inakuwaje anayejifanya anashinda vita ndiyo analialia kila siku?
Hiyo ni mbinu pia ya mapambano, akilia mnamuona kama weak ila kumshika haiwezekani. Anajua hana uchumi wa kutosha kupambana na Russia, kwahiyo kuomba msaada sio vibaya, mbona uganda aliomba msaada kwa Gadaffi, Mozambique, South Afrika, visiwa vya comoro havikuwahi kuomba msaada? Rais kuba msaada kulinda mipaka ya ardhi kupitia vita ni kawaida.
 
Back
Top Bottom