Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Kuna kipindi Wazungu huwa wanasema sisi Waafrika tuna Low IQ kuna kipindi huwa nafikiria kuwa wako sawa

Nadhani asilimia 60% ya Bara letu tukufu la Afrika ni chini ya IQ 60
 
In second you. Iwe kama umeme
 
Yaani tumechomewa ila tusijali kutotekeleza mambo hayana maslahi wala tija kwetu. Sidhani kama kumefanyika makubaliano yoyote yenye kutubana kisheria. Ni ku express nia tu.
 
Hizi ni akili za mataga tu. Hujui hata dhana ya competitive advantage?! Sisi tutapata kuinua uchumi wetu kupitia mauzo ya gesi huko Kenya, wao watapata kuinua uchumi wao kupitia kupunguza gharama za kusindika bidhaa ya viwandani. Kila upande unapata - win-win position.
 
Nchi ina gesi ya kutosha. TPDC haina pesa za kuisambaza. Mauzo/export ya gesi huko Kenya inaweza kutuongezea pesa za uwekezaji kwa TPDC kuendeleza kusambaza gesi. Pengine nikushauri. Uchumi ni sayansi siyo hizia. Na hiyo ndio iliyokuwa tabia ya mwendazake.
 
Kiukweli nchi hii bado haijafikia stage ya kuongozwa na mwanamama,tuwe wakweli tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Kwani ulishawahi kuuona huo mktaba wa hayo maingiliano? au una bwabwaja tu

Samia amezungukwa ni wachumi alioteuwa hivi karibuni, tuseme wewe ndio umeliona hili kuliko wao?

Alimradi unakuja tu hapa uandike kitu chochote
 

Hii gas ni ya waliogundua. Sio ya serikali kwa asilimia 100
 
Binafsi naona kama umewahi sanaaa hili la bomba gesi wamekubaliana kutafuta pesa zaa ujenzi wa ilo bomba naa bado hayo mazungumzo hayajaisha...

Ukisemea la gesi kwann una sahau kusemea pia la MW 400, ambazo tayyari project ni on going uwekaj wa njianza kusafirishia huo umeme kwenda kenya na hii ilisainia na mpendwa wetu
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
sio vizuri kumusema mtu vibaya lakini mama anafeli pakubwa sana sitaki niwe mnafiki hii nchi mama itamushinda ni suara la muda tuuh hana maajabu yeyote ???
 

1. Nadhani wewe ndiye huelewi alliances za mashirika kuwa ni kwenye codeshare, kwamba abiria mwenye ticket ya shirika moja anaweza kusafirishwa na kampuni nyingine kwenye njia wanazoshirikiana. Vile vile aliance hizo huzuia partners washindanie njia, yaani usitumie njia ambayo partner wako anatumia. Kwa hali hiyo partnership ya KQ na ATCL itaweza kuifanya ATCL isishindanie njia nyingi ambazo tayari ni za KQ.

2. Kuhusu hasara unakuza hasara ya ATCL kupita kiasi. CAG alikuambia sehemu kubwa za kinachoitwa hasara siyo hasara itokanayo kuendesha biashara vibaya bali ni mlundikano wa madeni ya zamani na tozo za serikali, ambazo rais SSH ameahidi kuzindoa. Sasa wewe kudai kuwa ni kutokana na volume ya capital pia huenda hujasaoma mahesabu ila unatafuta ama kuhalalisha hasara za KQ au kuzidi kudharau operations za ATCL.

ATCL ilipata hasara ya TSh 150b kwa mwaka ambazo ni sawa na US$ 64.7m ambao ni wastani wa USD5.9m kwa kila ndege (fleet ya ATCl ni ndege 11); KQ ilipata hasara ya KSh 36.2b ambazo ni sawa na US$338.63m ambao ni wastani wa USD 8.5m kwa kila ndege (fleet ya KQ ni ndege 40). Kwa akili yako ni kampuni gani iliyopata hasara kubwa hasa ukigundua kuwa KQ hawalipii uwanja wa JKIA wakati ATCL inalipia kutumia JNIA.
 
sio vizuri kumusema mtu vibaya lakini mama anafeli pakubwa sana sitaki niwe mnafiki hii nchi mama itamushinda ni suara la muda tuuh hana maajabu yeyote ???
Sema amefeli wapi na nini? Nyie mabaki ya magu bado hamtaki kukubali tu.
 
Wafuasi wa jiwe jengeni hoja vizuri,jiwe ndio keshakufa kumchonganisha mama na mfu ni wendawazimu,

Ushauri ni kuhakikisha viwanda vyetu vya ndani vipewe kipaumbale kwenye kupata gesi lakini kutouza gesi Kenya eti kisa tukiwauzia wakenya viwanda vyetu vitakufa,haya ni mawazo yakipumbavu.

Huyu jiwe mnamsifia bure,Tanzania tulikuwa na mashamba yetu ya maua yakutosha Arusha,jiwe kayapandishia kodi za hovyo mashamba yakashindwa kujiendesha yakafungwa,leo tunaagiza maua kutoka kenya kwasababu ya huyu jiwe mnaemuona shujaa.


Mungu amelikoa taifa,kilichotekea haikuwa bahati mbaya.
 

Another too much know
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…