Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Amesha saini, jinyonge.
 
Mkuu, "competitive advantage" ipo wapi hapa, mbona siioni?
Usiwe na shaka mkuu, mengi ya haya uliyosikia hapo ni kulisha upepo tu!

Kama bomba hilo litajengwa, huo si mpango wa leo wala kesho. Huenda hata Samia mwenyewe asilione hilo bomba lina picha gani.

Haya mambo mengine ni ya kupandisha 'pressure' za watu bila ya sababu zozote za maana.
 
Hili ni jibu lililofanyiwa kazi.
Hongera.
 
Sio kwa wakenya ninao wajua mimi...... Yaani wao wakuache wewe ukafungue biashara kwao kule..... Labda Uganda sio kenya.....
But kunao waTz weengi wenye biashara kubwa na ndogo pia. Wachaga wamejaa kwenye biashara ya nguo za mtumba. Kama hujui Kenya ni a country where you can own land ukiwa foreigner. No one can take that from you. Hata serikari haiwezi kuichukua. Fanya utafiti wako.
 
Shida inayotusumbua wengi ni mawazo ya inward looking na protectionalism by 100% we need strategically to balance.
 
Pengine hofu ni ile ya Tanzania kuwa nchi ya kuzalisha mazao ghafi kwenda kenya na kutokuwa na viwanda vya ndani vya kuchakata mazao au kuzalisha finished products na hivyo kubana ajira ya ndani. Kwa hilo tujipange na sera yetu ya viwanda ndiyo itakuwa na comparative adv.
 
Mngekuwa mnataka viwanda mngeweka sheria na kanuni nzuri za uwekezaji sio kuzuia gesi kwenda nje ya nchi.
 
Bomba la gesi linatumika chini ya asilimia 10 tu
 
Viwanda vya ndani vilianza kunyimwa gesi lini??
Kinacholalamikiwa ni viwanda vya ndani kunyimwa gesi halafu unaenda kumpa mtu wa nje, kwani ukatumia hata 1% tu ya ubongo wako, utapungukiwa na nini?
 
Mahindi na dengu tunauza Kenya gesi eti hapana?hii imekaaje?
 
Mmmmmmhmn mbona ngumu kumeza
 
H
Ii project ya kupeleka gesi Kenya ni ya muda mrefu watu walichelewesha kufanya maamuzi. Bora uamue kuliko kukaa kimya na kuchelewesha mambo.
 
Maza ni zaifu?
 
Kwani ulisikia Samia katoka Kolomije? Naye ni wa mjini kuliko Kenyatta kwahiyo ngoma droo. Aliyekuwa wa shamba now anaongoza malaika huko nchi ipo kwa mtoto wa mjini sasa hivi.
Kenyata mtoto wa mjini kwa kutafuta hela Na kuweka mbele maslah ya Kenya. Wa kwetu anaonekana mtoto wa mjini kwa kiswahili kizuri Na misemo mizuri
 
Hoja ni kwamba utampaje jirani gesi akaendeshee viwanda vyake wakati viwanda Vya ndani vinapata shida kuipata hiyo hiyo gesi?
 
Dust, mbona ndugu yenu alizuia kuingiza sukari nchini, kwa kufunga mipaka mwisho wa siku imepanda bei kutokana na kuadimika na kukosa ushindani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uelewa wako ni mdogo mnno. Kenya na Tanzania zinategemeana sana kibiashara. Hakuna haja ya kuwekeana figisu. Fungua fursa watu wademke.

Badala ya kulalamika, sisi inatakiwa tuangalie fursa na kuzichangamkia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…