Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign..
1.Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania..Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya.
a.Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje.
Ulichoandika hapo ni sawa na kusema tusiwauzie mahindi Wakenya, kwa sababu tukiwauzia watakuwa hawana shida ya chakula, na matokeo yake watakuwa wanashiba na kufanya kazi vizuri sana na hivyo watatuzidi!!!
Hivi kwanini Wabongo huwa mnadhani hizi raslimali mnazo nyinyi tu, na kwamba mkiacha ku-share na wengine, ndo basi tena watateseka huku sisi tukinawiri?
Btw, kwanini urudi nyuma na kila kitu kuwa Made In Kenya?! Kwanini usishauri na sisi tuendelee kuwekeza kwenye viwanda, na kuzalisha bidhaa bora zaidi na hatimae kuwazidi hao Wakenya?
FYI, pale Ethiopia kuna ujenzi wa Grand Renaissance Dam ambaounatarajiwa kutoa umeme wa kumwaga!!!
Kama unadhani njia ya kushindana na Kenya ni kutomuuzia gesi, kumbuka atakuwa na uwezo wa kununua umeme unaozalishwa kwa maji kutoka Ethiopia!!!
Kule Somalia ndo vile tu hapajatulia lakini na kwenyewe kuna hazina kubwa ya gesi!!! Wale jamaa wakishatulia, usishangae wao wakaanza kuzalisha gesi kabla yetu tuliolelewa na tamaduni za ",,,kwani gesi inaoza; ibaki tu ardhin na wenyewe tukishakuwa na uwezo wa kuchimba, tutachimba"
b.Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania.
Kwanini Tanzania tushindwe?! Kama hao wawekezaji watavutika kutokana na gesi kutoka Tanzania, nini kitafanya washindwe kuingia Tanzania inakotoka hiyo gas?
Au unajaribu kusema we're failure, na hatuwezi kushindana nao katika kuita wawekezaji? Kama ndivyo, solution ni kutokuuza raslimali yetu au solution ni kujitathimini kwanini tunashidwa kuvuta hao waweka
c.Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa
Elimu inahitajika kuhusu raslimali ya gesi manake hapa watu wanachanganya sana madesa!!!
Kwa kifupi tu ni kwamba, gas inayotarajiwa kuwa exported haijaanza kuchimbwa hata tone!! Gas hiyo wala haina uhusiano ni ile ambayo imeshaanza kutoka Mtwara hadi Kinyerezi
d.Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya.
Kwa sababu tu wanatarajia kuuza gesi Kenya?!
2.Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania.Dsm,Zanzibar na Kilimanjaro.
Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways..otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania.
3.Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele..
Lini KQ iliacha kuingia Tanzania? Wakati KQ bado inaingia Tanzania, kuna route ngapi za ATCL zinazohusisha Tanzania na Kenya?