Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Hilo liswahili lako limeshapigwa!

Chezea Kenyatta wewe!

He is a business-oriented politician, sio kama huyo kikongwe wa pwani.

Ndio maana wakenya wanamchekea usoni na kumzoza kisogoni maana wanajua wameshapata GOIGOI la kulichuna.
Tuna simama na mama Samia !!! Mama shupavu ,Mama mjanja ,Mama mstaarabu Misukuma tupa kuleeee chooni
 
UZI WA VILAZA HUU,WENYE POOR I.Q SHOULD BE IGNORED....!
*GES ITAUZWA KENYA
*UMEME TUTAUZA KENYA
*MAMA AMESISITIZA UJAZO WA KIBIASHARA
BAINA YA NCHI ZETU.
*KUONDOA MAKWAZO MIPAKANI
*KODI ZA MIPAKANI KUANGALIWA UPYA
*KAMATI ZA BIASHARA KUKUTANA MARA KWA MARA
*TWENDENI TUKAWEKEZE KENYA,SIONI UBAYA MOJA YA BANK ZETU KUFUNGUA TAWI KENYA KURAHISISHA BIASHARA ZA WATANZANIA KENYA KAMA WAO NA KCB YAO HAPA.A
Hapo hapo wajinga hawaelewi
 
Kinacholalamikiwa ni viwanda vya ndani kunyimwa gesi halafu unaenda kumpa mtu wa nje, kwani ukatumia hata 1% tu ya ubongo wako, utapungukiwa na nini?
Kwahiyo miaka yote hatuna viwanda kwa sababu tulikua hatuna ges!!
Viwanda vingapi vya Tz viliomba gezi vikanyimwa!??
Acheni Mwanamke Mwenye akili ajenge nchi!?? Uchumi wa Tanzania chini ya mwendazake ulikufa ndio maana alishindwa kuongeza hata walimu mishahara kwa miaka yote aliyotawala Tanzania
 
Huyu Mama anatufanya sisi wajingaaaaa... kumbe tunamwangalia tu akili zake zinapofikia

Eti takwimu za uwekezaji wa Kenya hapa kwetu kazitaja kwa dola na idadi ya miradi

Takwimu za uwekezaji wa Tanzania nchini Kenya kazitaja kwa trilioni za shilingi ya Kenya na idadi ya makampuni

Yani vitu vinne tofauti, makusudi kabisa ili kutuchanganya tusiweze kulinganisha...
 
Kwahili kweli tutamkumbuka JPM

Mama Samia asijilegeze kwa Wakenya, Hawa watu sio wazuri wanataka tuendelee kuwa soko la viwanda vyao ilihali products zingine tunaweza kuzitengeneza wwnyewe

Mama awe makini sana na aendelee kuwapiga pini kama JPM alivyofanya.

Shauri yetu Wadanganyika
Marehemu aluwadanganya sana mkamuona yeye ni Mungu wenu mkamuita Mungu !!! Mama ni mjanja kuliko mwendazake mama anafufua uchumi uliokua ICU !!!!
Jpm alishindwa hata kumiongezea mwalimu wa Tz mshahara
Hosp zilikosa dawa
Ajira hakuna
Alipalikia ukabila
Alipeleka maendeleo chato
Sasa tumwache Mama afanye kazi hutakiiiii hama nchi
 
Hayo maneno ya mkosaji !!fikra za miaka ya 50!!, wanawake wameongoza wazungu na kuleta maendeleo makubwa itakuwa kwa mwafrika, tena mtanzania?!!huyo mwanaume aliyeongoza miaka mitano , maendeleo gani ameyaleta?hao kina mseveni, mugabe, derby, biya, sasongweso zaidi ya miaka 30, madarakani walifanya nini?!acheni hizo muhukumuni mtu kwa uwezo wake na sio JINSI, yake.MAMA KANYAJA TWENDE,
Lisukuma hilo limepagawa
 
Binafs sioni umuhimu wa kuwa wabinafsi ktk nishati hiyo baina Tz na Kenya,kizuri share na mwenzio.Kuna miradi mimiipogine ipo pale kwaajili ya kukuza biashara na uhusiano mzuri.Tz tunaenda kuwa na surplus ya umeme wa maji mwakani ambao ni wa bei nafuu.Tutangulize maslahi mapana ya nchi zetu mbili badala ya kutanguliza ubibafsi na woga kwenye ushindani wa biashara
Shida sio kuuza nje..Tunauza nje kwa faida ipi je sisi wenyewe imetutosheleza kwanza?
Kama uwekejazi wa gas ulitokana na kodi za watanzania basi watanzania hao hao kwanza ndio wafaidike na kodi zao..
Tuuze gas baada ya sisi kuwa imetutosheleza kile kinachozidi (surplus)ndio kiuuzwe..
Viwanda vyetu wenyewe vinahitaji gas lakini gas hiyo hiyo hawapewi..inakuwaje unakwenda kumpa jirani yako!..
 
Napenda kuandika kidogo tu kulingana na uwelewa wangu juu ya Ziara ya Mama nchi Kenya na mikataba mlio tiana sign..
1.Ujenzi wa bomba la gas kutoka Tanzania kwenda Mombasa kwa ajili ya matumizi ya viwanda nchini Kenya,hapa mama unefail pakubwa sana maana yake nikwamba bidhaa za Kenya zitakuwa zinazalishwa kwa gharama nafuu zaidi na kuteka soko la Africa Mashariki kuliko Tanzania..Tutarudi miaka ya nyuma tena kila kitu Made in Kenya.
a.Hii sera yetu ya viwanda itakufa maana hatuweza kushindana tena na product kutoka Kenya na vijana wetu watazidi kuwa wachuuzi wa bidhaa kutoka nje.
Ulichoandika hapo ni sawa na kusema tusiwauzie mahindi Wakenya, kwa sababu tukiwauzia watakuwa hawana shida ya chakula, na matokeo yake watakuwa wanashiba na kufanya kazi vizuri sana na hivyo watatuzidi!!!

Hivi kwanini Wabongo huwa mnadhani hizi raslimali mnazo nyinyi tu, na kwamba mkiacha ku-share na wengine, ndo basi tena watateseka huku sisi tukinawiri?

Btw, kwanini urudi nyuma na kila kitu kuwa Made In Kenya?! Kwanini usishauri na sisi tuendelee kuwekeza kwenye viwanda, na kuzalisha bidhaa bora zaidi na hatimae kuwazidi hao Wakenya?

FYI, pale Ethiopia kuna ujenzi wa Grand Renaissance Dam ambaounatarajiwa kutoa umeme wa kumwaga!!!

Kama unadhani njia ya kushindana na Kenya ni kutomuuzia gesi, kumbuka atakuwa na uwezo wa kununua umeme unaozalishwa kwa maji kutoka Ethiopia!!!

Kule Somalia ndo vile tu hapajatulia lakini na kwenyewe kuna hazina kubwa ya gesi!!! Wale jamaa wakishatulia, usishangae wao wakaanza kuzalisha gesi kabla yetu tuliolelewa na tamaduni za ",,,kwani gesi inaoza; ibaki tu ardhin na wenyewe tukishakuwa na uwezo wa kuchimba, tutachimba"
b.Kenya itatumia mwanya huu kuvutia wawekezaji kutoka nje kuwekeza Kenya kuliko kuja kuwekeza Tanzania.
Kwanini Tanzania tushindwe?! Kama hao wawekezaji watavutika kutokana na gesi kutoka Tanzania, nini kitafanya washindwe kuingia Tanzania inakotoka hiyo gas?

Au unajaribu kusema we're failure, na hatuwezi kushindana nao katika kuita wawekezaji? Kama ndivyo, solution ni kutokuuza raslimali yetu au solution ni kujitathimini kwanini tunashidwa kuvuta hao waweka
c.Tunasafirisha gas kama kuna surplus ya viwanda vyetu na matumizi yetu kama Taifa.Viwanda vyetu bado vinahitaji nishati ya gas lakini bado upatikanaji wake umekuwa mgumu na kwa gharama kubwa
Elimu inahitajika kuhusu raslimali ya gesi manake hapa watu wanachanganya sana madesa!!!

Kwa kifupi tu ni kwamba, gas inayotarajiwa kuwa exported haijaanza kuchimbwa hata tone!! Gas hiyo wala haina uhusiano ni ile ambayo imeshaanza kutoka Mtwara hadi Kinyerezi
d.Kenyatta amecheza karata yake vizuri katika ujenzi wa gas kuliko Mama sijui washauri wake wamekwama wapi natarajia kuona Kenya ikinufaika zaidi katika utawala wa Mama kuliko kipindi chochote kile katika historia ya Tanzania na Kenya.
Kwa sababu tu wanatarajia kuuza gesi Kenya?!
2.Ushirikiano wa anga..hapa Kenyatta anatafuta namna ya kuisaidia Kenya airways..inakwenda ku dominate soko na anga tena kama huko nyuma.hapa kumbuka faidia kubwa ya Kenya Airways inatokana na safari za Tanzania.Dsm,Zanzibar na Kilimanjaro.
Hapa tutalajie Air Tanzania ikifa kifo cha mende kutokana kutoweza kumudu ushindani na Kenya airways..otherwise kufanyike changes za haraka katika Management ya Air Tanzania.
3.Soko la utalii hapa Kenyatta amecheza vizuri kama pele..
Lini KQ iliacha kuingia Tanzania? Wakati KQ bado inaingia Tanzania, kuna route ngapi za ATCL zinazohusisha Tanzania na Kenya?
 
Raisi SSH hajakosea popote kwenye hiyo mikataba. Kwanza, gesi tunayo nyingi na tumepata mnunuzi, kwa nini asiuziwe? Huwezi kuogopa upinzani kwa kuficha bidhaa yako. Nafikiri cha muhimu ni kukumbuka kwamba hajakurupuka leo na kwenda kutia sahihi. Haya yote yalikuwa kwenye mchakato sema tu kulikuwa na ukiritimba kufikia makubaliano na kutia sahihi. Cha muhimu ni kuwa hiyo mikataba iwe ni ya win-win situation, siyo ya upande mmoja kufaidika na mwingine kutopata chochote.
 
Muacheni mama awajengee uchumi wenu maana kiongozi wa malaika alishauua. Mshukuruni Mungu amewaokoa huo uchumi wenu ulishaenda kuzimu. Hujasoma media za bongo huko kwamba soko la hisa la Dar limeanza kurejea hali yake.
Magufuli na Kikwete nani aliua uchumi. Au ule uchumi wa madawa ya kulevya ndiyo mliona maendeleo. Mpende msipende hakuna raisi wa TZ ambaye aliupandiksha na kuukuza uchumi kama Magufuli. Mnaweza mkamchukia lakini alitutoa chini kabisa na kutufikisha uchumi wa kati. Hata Nyere hakuweza hilo. Leo hii ingekuwa bado awamu ya NNE hata mawaziri na viongozi wakuu wa serkali wangekuw wamekwisha kuwa MATEJA.
 
UZI WA VILAZA HUU,WENYE POOR I.Q SHOULD BE IGNORED....!
*GES ITAUZWA KENYA
*UMEME TUTAUZA KENYA
*MAMA AMESISITIZA UJAZO WA KIBIASHARA
BAINA YA NCHI ZETU.
*KUONDOA MAKWAZO MIPAKANI
*KODI ZA MIPAKANI KUANGALIWA UPYA
*KAMATI ZA BIASHARA KUKUTANA MARA KWA MARA
*TWENDENI TUKAWEKEZE KENYA,SIONI UBAYA MOJA YA BANK ZETU KUFUNGUA TAWI KENYA KURAHISISHA BIASHARA ZA WATANZANIA KENYA KAMA WAO NA KCB YAO HAPA.A
Ww ndio kiazi kweli...
kwenda kuwekeza Kenya mtaweza?
Tz mtabaki Ku produce raw materials
tu
 
Back
Top Bottom