Zijue Mbinu Hizi za Kuwa Tajiri("Milionea")

Zijue Mbinu Hizi za Kuwa Tajiri("Milionea")

Watu wengi wana ndoto za kuwa matajiri. Wanafanya kazi kwa bidii usiku na mchana ili wawe matajiri. Hata hivyo ni wachache wanaofanikiwa kuupata utajiri. Leo nakutajia baadhi ya mbinu muhimu za kupata utajiri au kuwa milionea/bilionea – sizungumzii utajiri unaopatikana kwa bahati au kwa kurithi.

Utajiri unapatikana kwa kutumia mbinu sahihi, nidhamu, na uthabiti. Kama kweli unataka kuwa tajiri, tumia mbinu hizi:

1. Anza kuwa na mtazamo(mindset) wa utajiri
Utajiri huanzia kwenye mawazo. Watu matajiri huifikiria pesa tofauti na watu wa kawaida. Ili kujenga mtazamo wa utajiri fanya hivi:
  • Matumizi yako ya pesa yawe ya chini kuliko kipato chako(spend less than you earn)
  • Weka malengo ya kifedha ya muda mrefu.
  • Kaa katikati ya watu wenye mafanikio na maarifa ya kifedha.
2. Weka pesa benki na wekeza kwa hekima
Kuweka pesa benki peke yake hakutakufanya uwe tajiri, lakini ukiwekeza utafanikiwa. Kwahiyo badala ya kuweka pesa zako zote benki:
  • Wekeza kwenye hisa, dhamana, au mifuko ya pamoja. Kabla ya kuwekeza fanya utafiti.
  • Anzisha biashara yenye uwezo wa kukua.
  • Wekeza kwenye mali isiyohamishika(real estate) au mali nyingine zenye thamani inayoongezeka.
3. Uwe na vyanzo vingi vya mapato
Chanzo kimoja tu cha mapato hakitoshi sana kama unataka kupata utajiri mkubwa na wa kudumu. Watu matajiri hupata pesa kutoka kwenye vyanzo vingi vya mapato kama vile nyumba za kupangisha, gawio(dividents), au mirahaba(royalties), biashara za mtandaoni nk.

4. Dhibiti fedha zako vizuri
Huwezi kuwa tajiri kama utashindwa kudhibiti au kusimamia fedha zako. Kwahiyo:
  • Uwe na bajeti na ufuatilie(track) matumizi yako.
  • Epuka madeni yasiyo ya lazima na tumia pesa kwa busara.
  • Uwe na akiba ya dharura(emergency fund) ili uweze kuyakabili matukio au hali zisizotarajiwa.
5. Elimu haina mwisho. Jifunze tena na tena masuala ya kifedha
Dunia ya kifedha inabadilika kila wakati. Watu matajiri huendelea kujifunza kwa:
  • Kusoma vitabu kuhusu utajiri na usimamizi wa fedha.
  • Kuhudhuria semina za biashara na uwekezaji.
  • Kujifunza kutoka kwa washauri na wataalamu wa fedha.
6. Uwe mvumilivu (be patient and persistent)
Utajiri hauoti kama uyoga. Wajasiriliamali wengi walichukua miaka kadhaa kuwa matajiri. Hivyo uwe mvumilivu, na usikate tamaa unapokutana na changamoto.

7. Ukianza kupata utajiri, wafundishe wengine mbinu ulizotumia
Andika vitabu, uza. Wafundishe wengine masuala ya kifedha kwenye semina, warsha, makongamano, kwa malipo.

Ukishakuwa tajiri usimsahau Mungu.
Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako... jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake...( Kum 8:10-11).

Ukimsahau Mungu Maandiko haya yanaweza kukuhusu:
“Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo. Akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje?

Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanaitaka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu anayejirundikia mali kwa ajili yake mwenyewe, lakini si tajiri mbele ya Mungu.”( Luka 12:15-21)

View attachment 3236711
Asante milionea
 
chama cha wanaume bahili.
Luka 6:38(NEN)
"Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa."
 
Eti live below ur means 🤣🤣🤣
huo mshahara wenyewe tuu kwa budget simple ya ugali maharage ikifika tarehee 15 hela kwishney
Duh! Basi siku moja moja funga, unywe maji tu asubuhi mpaka jioni. Kufunga(fasting) ni afya na pia unasev pesa; hiyo itakuwezesha ku-live below ur means🤣🤣🤣
 
Mkuu hizi ulizotaja sio mbinu bali ni kanuni za kufuata ili kuwa tajiri,

Mbinu siku zote huwa hazina mambo mengi yani hazihitaji maandalizi mengi,

Mtu yeyote mwenye mbinu za kuwa tajiri aje atusaidie
 
Duh! Basi siku moja moja funga, unywe maji tu asubuhi mpaka jioni. Kufunga(fasting) ni afya na pia unasev pesa; hiyo itakuwezesha ku-live below ur means🤣🤣🤣
Mwee! Hiyo ugali maharage tayarinfunga tosha alafunwataka nigunge tena hapa aisee
Sie wengine tutaishia kuwa maskin tusijiumize sana ati
 
Mkuu hizi ulizotaja sio mbinu bali ni kanuni za kufuata ili kuwa tajiri,
Aliyenifundisha Kiswahili na Kiingereza ni mwalimu mzuri.
  • Mbinu (Strategies): Ni mipango ya utekelezaji ili kufanikisha jambo fulani. Katika muktadha wangu, hizo ni mbinu za kujijengea utajiri.
  • Kanuni (Principles): Ni misingi au mwongozo wa maadili na sheria zinazotawala jinsi mtu anavyopaswa kuishi au kufanya kazi.
 
Rubbish/ utumbo mtupu
Uwo mda ulotumia kuandika ungeutumia kusoma biblia au quran ungepata kitu
 
Back
Top Bottom