Umesema upo Tanga .
Labda uanze kutuambia kuwa amedanya nini Tanga ambacho kimeinua maisha ya watu?
Kama ni viwanda bado hajafikia hata robo ya vile alivyoacha Mtawala wa kwanza yaani mkoloni.
Tanga ni kati ya mikoa yenye utajiri mkubwa sana wa mali asili lakini hakuna miundo Mbinu bora zaidi ya barabara kuu zilizojengwa tangu uhuru na nyingine awamu ya tatu na nne.
Kila siku ni uzinduzi tu , Hela zinazokusanywa kwenye jiji na halmashauri zote zimepelekwa kununua ndege nane Cash. Yaani unachukua pesa za maskini unaenda kununua ndege Cash kwa Mabilionea wa Dunia badala ya kukopa ulipe kibiashara. Hapo lilichokua kinatafutwa ni 10% . Jiulize ni kwa nini watawala wapo tayari kuua hata maelfu ya watu ili wasalie madarakani. Ni binadamu gani asiyeogopa dhambi ya kuua?
Jibu ni jepesi wanalinda mali zao wanazojua wazi akija mpenda haki wataulizwa walizipataje kwenye nchi maskini kama hii yenye madeni makubwa hukuo kwa mabeberu.
Hizo mali wanamkusanyia nani wakati wanasema asiyefanya kazi asile? Je,hao wajukuu wao wanawawekea mali kila kona ya nchi wakati hata hawajazaliwa wameshafanya kazi wapi ili wakute hizo mali wanalimbikiza.
Mimi kwa kweli siwezi kumdhuru mtanzania mwenzangu ili tu hawa mabilionea wa CCM waendelee kula kodi na kujilimbikizia mali
Yani mtu akawadhulumu Wazanzibari kwa sababu ya kumtafutia Huseni Mwinyi urais ambao alikua nao Baba yake na wamechuma mali kupitia madaraka na kodi za watanzania mpaka wamelewa mali !! Itakua ni dhambi kubwa sana kuiba kura kwenye uchaguzi wa Zanzibar na hata wa Bara kuiba kura ili JPM aliyekaa kwenye uwaziri miaka 20 na Urais miaka 5 ili tu aendelee kuwakalia watu waliomkataa. Hata Shetani atatucheka kuwa hivi hawa wanataka Mali za nchi zote ziende kwa watu wale wale halafu wanalalamika maisha ni magumu.
Weka mbunge akizingua piga chini achukue pesa zake akafanye biashara sio kuhonga wapiga kura kama wanavyoanya CCM.
Chagua Rais akizingua na kujifanya nchi ni mali yake na kuendekeza ukabila ,piga chini atumie pesheni na Kiinwa mgongo chake akawekeze sio kuzunguka mitaani na mamifuko ya pesa kugawia watu ambao ungefungua hata shamba la kisasa wangepata ajira. Unagawa Pesa ili upate kura upate pesa za watanzania wanaokamuliwa kulipa kodi.
Magufuli au Lisu yeyote atakayeshinda kwa Haki anapaswa kutambua kuwa hii nchi sio mali yake.
CCM kupitia mifumo yake imewapa mamlaka watawala kuifanya nchi kuwa mali ya mtu binafsi ndio maana wanasema kuwa mukimpa nchi ataiuza. Ujinga huo haupaswi kuendelea ,eti mtu mmoja anaweza kujifungia chumbani na mke wake na kuweka mikataba ya kuuza au kununua nchi bila kuulizwa na mtu.
Mwaka huu wasimamizi wa uchaguzi ni lazima wasomewee Duwa maalumu sio kushila vitabu vya dini na kuapa kwenda kufanya uhuni ?
Na zaidi wale viongozi wa dini kama akina Shekhe Musa na Askofu Gwajima na Mkunde wajitokeze kwenda kuangalia uchaguzi kama ni wa haki au ni dhulma ili watu watakapokataa viongozi wasiochaguliwa wasije wakalaumu na kuanza kuimba nyimbo za amani bila Haki huku wezi wakiishi kwa raha Mustarehe na waliodhulumiwa wakiishia Gerezani. Hakuna haki hiyo Mbinguni na duniani. Mshahara wa dhambi ni mauti.
Sijawahi kumsikia kiongozi wa Tume wala Bashiru na Polepole wakizungumzia habari za Uchaguzi wa huru na wa Haki.
Wamebaki kutishia watu mabomu na risasi kama vile hayo marisasi yakishawaua hao watu yanaweza kuwatafutia mahali pema peponi au Jehanamu .
Yesu alisema msiogope watu wanaoua mwili tu lakini hawana wanaloweza kuamua juu ya roho zenu. Tukijua maana yake tutaishi kwa upendo ,haki ,utu na amani kwa watu wote.
Kinachowasumbua CCM ni ubinafsi tu na uroho wa madaraka ndio maana kila mtu anajipendekeza kwa Kuwaumiza wengine utafikiri hii nchi imeumbwa na makada wa CCM.