leta hoja ndio maana huwa nasema watu wanajiunga na vyama vya siasa kwa kufata watu na wala siyo hoja jenga hoja na usije na hoja ya kusema furani ana wivu, kwanza wote hao wanao tuhumiana kwann waseme leo, mda wote huo walikuwa wapi, kwann chadema hawakusema kipindi tu zitto amepewa hzo hela na mkono, na pia kwa nn zitto hakusema haukusema wakati mbowe amepewa hizo hela....SIASA BWANA MPAKA MGOMBANE,.......ndo tujue siri zenu..........hakuna cha nan wala nan ENZI ZA NYERERE WOTE NI MAGIDANYANGA.....
 
heeeee.MBOWE vipi tena?unasema tatizo si kupewa bali umepewa kwa sababu ipi,sasa hizo tuhuma za zitto kupewa magari hazijaweka wazi alipewa kwasababu ipi,kama zitto akitakiwa ajibu tuhuma na wewe mbowe jibu zako,majibu yako ni mepesi mno..INAELEKEA CHADEMA KUNA MADUDU MNO
 

Je ZZK katamka neno CHACHA WANGWE!??? Au unaropoka!????
 
FALLLLLLLLLLLACYYYYYYYYYYYYYYYYYYYY HUNA HOJA JENGA HOJA JIBU KWA HOJA WOTE WEZI........tu
 

Soma post vizuri ndio ujibu!
 
mimi sijaelewa kosa la zitto liko wapi?? yaani zitto azushiwe., atukanwe, atengwe, aitwe majina yote, mpaka kupewa tuhuma 11, leo hizo tuhuma 11 hili la mkono halimo

ghafla wanakuja na tuhuma za kitoto, jamani jiweke wewe nafasi ya zitto hata kama unaheshimu wakubwa wako kiasi gani lakini nido hivyo tena, uvumulivu una mipaka

mbowe kwisha habari yake, na huu ni mwanzo tu
 

Unakosea sana kumlinganisha zitt nzt na shonza na mwampamba zito ni ubavu cdm,mnasema alikuwa wapi kutoa shutuma zidi ya ufisadi wa mbowe lia hamuhoji tundu alikua wapi hadi jana aliporusha kombora kwa zitto kuwa kahongwa magari na mkono?zitt asingesema hadi kachokonolewa ss tunajua pumba na mchele mnasema ztt ajibu hoja mbona mbowe hajajibu hata hoja moja na hamuhoji?zitt ni zaici ya hao mnaotolea mfano ngojeni muone kifo cha cdm chakaribia
 

Ndo nini mkuu!?
 
Katika maandishi yake na matamshi yake kijana ZZK amekiri kupokea magari mawili kutoka kwa mwanasheria nguli hapa nchini Mkono ili kuuza chama na kukisambaratisha katika chaguzi. Hayo ameyakiri yeye mwenyewe ZZK na kuzifanya tuhuma zote anazotuhumiwa kuhusu kikuhujumu chama kuanza kujianaika zenyewe.

ZZK badala ya kutetea amekiri na kuanza kurusha makombora kwa mwenyekiti wa Taifa ikiwa ni mikakati mahususi tangia pm7, mabadiliko 2013 na majukwaa yote ZZK na kundi lake wamekuwa wakiyatumia. Nia yao ni kumchafua mwenyekititi wa cdm taifa na katibu mkuu kwani wao ndio mihimili ya chama.

Katika tuhuma zake kwa mwenyekiti anakiri kujua michango ya mwenyekiti ambayo amepokea kwa niaba ya chama na kukiwezesha chama. Wapo wengi kutoka CCM wamechangia CDM na hawakutaka majina yao ya tajwe, na kmichango yao imewasilishwa ndani ya chama kwa nia nzuri, ni mzee Sabodo aliyekubali high risk kujitambulisha na michango yake.

Tatizo kwa ZZK ambalo yeye anashindwa kulijua ni nia ya michango na misaada aliyopokea kama yeye binafsi ili kukiangamiza chama. ZZK hana tena weledi wa kusema yeye sio fisadi. Anakiri wazi alipokea magari ya Mkono eti kwasababu alifanya mazoezi ya vitendo kwenye law firm yake. Wakati ZZK anatuhumiwa kuwa ni mnafiki kwa kusema hapokei posho kumbe mlango wa nyuma anauza chama kwa kupokea bahasha za magari na mengine mengi.

Kwasababu ZZK ameamua kuingia msituni na kufungulia bomba la maji chafu, ni wakati wa kumpuuza yeye na kundi lake kwani nia yao kubwa ni kuona CDM inasambaratika. Lazima wajue CDM sio watu wanne au watano na hawezi kutishia uhai wa chama kwasababu ya tamaa yake binafsi ya madaraka, fedha, utukufu na kujikweza.

Ninaamini kabisa ZZK ahajui uongozi, hana hekima, busara, utulivu wala maono. Hajui maana ya chama cha siasa zaidi ya kuamini yeye ana akili sana. Wanapiga sana kelele ila wanashindwa kuwa viongozi. Kama CDM imesimamiwa na ikawa chama imara cha upinzani ambapo sasa kila mtanzania alipo anayejitambua anaweza kutetea masilahi ya sehemu yake kwa jukwaa la cdm. CDM imejengeka kitaifa na kumfanya kila mwenye nia njema kuweza kuwatetea wananchi wake walipo bila kuingiliwa.

ZZK pamoja na kuwa Mbunge wa KK kwa muda wa miaka 7 sasa na naibu katibu mkuu ameshindwa kujenga chama ndani ya jimbo lake la uchaguzi na kuambulia nafasi chache sana za madiwani kama sio moja. Kiongozi anapimwa kwa matokeo ya uongozi wake na mafanikio. Ndio ZZK ni maarufu na kila mtu anamjua, hata JK ni maarufu kama ilivyo kwa babu Seya nk Ila kujulikana na kila mtu sio tija, na hapa ndipo Watz huwa tunakosea, mtu kujulikana sana lazima iendani na utendaji wake. Unapotaka kujipambanua kuwa kiongozi wa chama cha siasa lazima utendaji wako wa kisiasa ndani ya chama uwe bayana, zaidi ya kulalamika kila siku hana la kuonyesha.

Ameshindwa kuunganisha nguvu na wabunge wenzake na siku zote amekuwa na chembe za usaliti. Ndio kesi iko mahakamani, vyovyote vile itakavyoamuliwa kwani sasa ni dhahiri inapikwa kwa msemo inaandaliwa inaandikwa.

Namtakia kila kheri huko aendako ila akumbuke tu uongozi ni busara.
 
Zitto hajakose lolote kujibu hoja hii ya magari na kutaja za mbowe kiasi kwa leo maana wamemchokoza wao kwa kumtuma lisu kuleta longolongo hiii, na yeye anayajua mengi ila kwa kuwa amekomaa kisiasa alikuwa anayamezea mpaka wao walipoanza mchezo huu wakidhani yeye hana la kusema au amesahau ya kwao ndio matokeo yake ndio haya, kawamwaga kamasi kwa kumwaga makubwa na mazito kabisa, namuomba zitto aendelee kumwaga na ya uvunguni maana inawezekana yako mengi na leo kamwaga kiasi akisubiria maamuzi ya kamati kuu ili afanye kufuru ya kufu gua mwaka 2014. Wamemwaga mboga na yeye anamwaga ugali, yumo kwenye chama muda mrefu sio kama lissu anayepelekwa pelekwa na mbowe
 
Soma post vizuri ndio ujibu!

Sikurupuki kama wewe unae suburi vipande vya fedha ili uaminishe watu uongo ilimradi umepata chochote, tumia akili yako basi tuhuma zinajibiwa sio kutafutiwa tuhuma za uongo ili kuficha tuhuma zanazo takiwa kujibiwa huo ni uchanga sana kwenye siasa huyo alitakiwa awe Monitress kiluvya huko chadema walikosea sana kumpa cheo huyo mbwiga mwenzio.
 
wote wanafiki ZITTO na MBOWE kwa sababu ganai usingekuwa waraka tusingeyajua hayo yote......kwa nn chadema hawakusema mapema tuhuma za zitto, na kwa nn zitto hakusema mapema tuhuma za mbowe siasa za tz bwana uchafu mtupu wote wana makosa ya kujibu mbele za mungu......wote wezi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…