Katika maandishi yake na matamshi yake kijana ZZK amekiri kupokea magari mawili kutoka kwa mwanasheria nguli hapa nchini Mkono ili kuuza chama na kukisambaratisha katika chaguzi. Hayo ameyakiri yeye mwenyewe ZZK na kuzifanya tuhuma zote anazotuhumiwa kuhusu kikuhujumu chama kuanza kujianaika zenyewe.
ZZK badala ya kutetea amekiri na kuanza kurusha makombora kwa mwenyekiti wa Taifa ikiwa ni mikakati mahususi tangia pm7, mabadiliko 2013 na majukwaa yote ZZK na kundi lake wamekuwa wakiyatumia. Nia yao ni kumchafua mwenyekititi wa cdm taifa na katibu mkuu kwani wao ndio mihimili ya chama.
Katika tuhuma zake kwa mwenyekiti anakiri kujua michango ya mwenyekiti ambayo amepokea kwa niaba ya chama na kukiwezesha chama. Wapo wengi kutoka CCM wamechangia CDM na hawakutaka majina yao ya tajwe, na kmichango yao imewasilishwa ndani ya chama kwa nia nzuri, ni mzee Sabodo aliyekubali high risk kujitambulisha na michango yake.
Tatizo kwa ZZK ambalo yeye anashindwa kulijua ni nia ya michango na misaada aliyopokea kama yeye binafsi ili kukiangamiza chama. ZZK hana tena weledi wa kusema yeye sio fisadi. Anakiri wazi alipokea magari ya Mkono eti kwasababu alifanya mazoezi ya vitendo kwenye law firm yake. Wakati ZZK anatuhumiwa kuwa ni mnafiki kwa kusema hapokei posho kumbe mlango wa nyuma anauza chama kwa kupokea bahasha za magari na mengine mengi.
Kwasababu ZZK ameamua kuingia msituni na kufungulia bomba la maji chafu, ni wakati wa kumpuuza yeye na kundi lake kwani nia yao kubwa ni kuona CDM inasambaratika. Lazima wajue CDM sio watu wanne au watano na hawezi kutishia uhai wa chama kwasababu ya tamaa yake binafsi ya madaraka, fedha, utukufu na kujikweza.
Ninaamini kabisa ZZK ahajui uongozi, hana hekima, busara, utulivu wala maono. Hajui maana ya chama cha siasa zaidi ya kuamini yeye ana akili sana. Wanapiga sana kelele ila wanashindwa kuwa viongozi. Kama CDM imesimamiwa na ikawa chama imara cha upinzani ambapo sasa kila mtanzania alipo anayejitambua anaweza kutetea masilahi ya sehemu yake kwa jukwaa la cdm. CDM imejengeka kitaifa na kumfanya kila mwenye nia njema kuweza kuwatetea wananchi wake walipo bila kuingiliwa.
ZZK pamoja na kuwa Mbunge wa KK kwa muda wa miaka 7 sasa na naibu katibu mkuu ameshindwa kujenga chama ndani ya jimbo lake la uchaguzi na kuambulia nafasi chache sana za madiwani kama sio moja. Kiongozi anapimwa kwa matokeo ya uongozi wake na mafanikio. Ndio ZZK ni maarufu na kila mtu anamjua, hata JK ni maarufu kama ilivyo kwa babu Seya nk Ila kujulikana na kila mtu sio tija, na hapa ndipo Watz huwa tunakosea, mtu kujulikana sana lazima iendani na utendaji wake. Unapotaka kujipambanua kuwa kiongozi wa chama cha siasa lazima utendaji wako wa kisiasa ndani ya chama uwe bayana, zaidi ya kulalamika kila siku hana la kuonyesha.
Ameshindwa kuunganisha nguvu na wabunge wenzake na siku zote amekuwa na chembe za usaliti. Ndio kesi iko mahakamani, vyovyote vile itakavyoamuliwa kwani sasa ni dhahiri inapikwa kwa msemo inaandaliwa inaandikwa.
Namtakia kila kheri huko aendako ila akumbuke tu uongozi ni busara.