arola
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 550
- 187
Nafurahi sana pale ambapo watu wenye akili wanasoma mambo yanayo andikwa humu jf na kuyatafakari. Mtu ukitafakari saana mambo ya humu jf utaona kuwa wengi huenda kwa mihemko zaidi ya halisia.
Mh. Zitto Kabwe, umetuhumiwa na CC ya CDM. Unaacha kujitetea hizo tuhuma ulizo vikwa, unatoka kabisa kwenye somo unaenda kuleta mambo ya mwaka 47!!!Muda wote weye ulikuwa kimyaa. Hasira ni M/kiti wako kamtuma Lisu akuseme. Mjibu basi huyo Lisu. Unapomwacha Lisu ukaleta issue ya Mbowe tena ambayo usingaliisema inaonesha kuwa moyo wako haupo sawa na Mbowe.
Mambo ya kifamilia ya Mh. Mbowe yanahusu nini hongo ulizopokea weye kutoka kwa Mkono? ZZK jibu tu tuhuma zako, tena sio kwenye fb bali fuata the right channel na utajibiwa tu. Kila hatua unayochukua ni hatua mbovu zaidi. Kama ungeandika barua yako ya kujitetea kwa CC na ukaomba msamaha kwa tuhuma hizo, ukaeleza kuwa litakuwa pigo kubwa kwa Wananchi wa Kigoma Kask. wewe kuupoteza ubunge wako, hapo sasa, hata sisi tungeweza kuomba msamaha pamoja na weye kwa CC.
Tungesema umeliona kosa hivyo kurudia hapana na kwamba CC lazima nao wakuamini. Hayo hutaki kwa sababu ulihakikishiwa na hao waliokutuma ambao hujakanusha mpaka sasa. Wao walikuhakikishia kuwa watakuweka CDM kama mwanachama wa Mahakama na ndicho wanakazania kufanya. Sawa, kabisa lakini nadhani CCM ndiyo watalia zaidi siku si nyingi. This is going to be a reference in every court proceedings to come of which am quite sure they will be many from ccm soon and very soon.
Mzanzibari walie mrimua mbona hakwenda mahakamani? Kiburi mnachopewa na hilo lichama kitawaharibu tu. Ungeshuka ukaonwa na umma ndipo ungekaa juu siku zote wala si kwa hizi fitna zako.
Punguka mihemko.... wamemwaga mboga naye kamwaga ugali.. tatizo liko wapi? Pipooooooz!!! GONGO FC UFIPA.