Zitto aanika siri nyeti za Mbowe! Adai hatakufa kama Chacha Wangwe
Nafurahi sana pale ambapo watu wenye akili wanasoma mambo yanayo andikwa humu jf na kuyatafakari. Mtu ukitafakari saana mambo ya humu jf utaona kuwa wengi huenda kwa mihemko zaidi ya halisia.
Mh. Zitto Kabwe, umetuhumiwa na CC ya CDM. Unaacha kujitetea hizo tuhuma ulizo vikwa, unatoka kabisa kwenye somo unaenda kuleta mambo ya mwaka 47!!!Muda wote weye ulikuwa kimyaa. Hasira ni M/kiti wako kamtuma Lisu akuseme. Mjibu basi huyo Lisu. Unapomwacha Lisu ukaleta issue ya Mbowe tena ambayo usingaliisema inaonesha kuwa moyo wako haupo sawa na Mbowe.
Mambo ya kifamilia ya Mh. Mbowe yanahusu nini hongo ulizopokea weye kutoka kwa Mkono? ZZK jibu tu tuhuma zako, tena sio kwenye fb bali fuata the right channel na utajibiwa tu. Kila hatua unayochukua ni hatua mbovu zaidi. Kama ungeandika barua yako ya kujitetea kwa CC na ukaomba msamaha kwa tuhuma hizo, ukaeleza kuwa litakuwa pigo kubwa kwa Wananchi wa Kigoma Kask. wewe kuupoteza ubunge wako, hapo sasa, hata sisi tungeweza kuomba msamaha pamoja na weye kwa CC.
Tungesema umeliona kosa hivyo kurudia hapana na kwamba CC lazima nao wakuamini. Hayo hutaki kwa sababu ulihakikishiwa na hao waliokutuma ambao hujakanusha mpaka sasa. Wao walikuhakikishia kuwa watakuweka CDM kama mwanachama wa Mahakama na ndicho wanakazania kufanya. Sawa, kabisa lakini nadhani CCM ndiyo watalia zaidi siku si nyingi. This is going to be a reference in every court proceedings to come of which am quite sure they will be many from ccm soon and very soon.
Mzanzibari walie mrimua mbona hakwenda mahakamani? Kiburi mnachopewa na hilo lichama kitawaharibu tu. Ungeshuka ukaonwa na umma ndipo ungekaa juu siku zote wala si kwa hizi fitna zako.

Punguka mihemko.... wamemwaga mboga naye kamwaga ugali.. tatizo liko wapi? Pipooooooz!!! GONGO FC UFIPA.
 
Kwani lisu alikuwa wapi kusema haya dogo kawashika pabaya lazima mtambike kama kawaida yenu.

nani atambike?
cpo huko nilishakombolewa cfanyi matambiko!

hakuna aliyeshikwa pabaya zaidi yake yy aliyekimbilia mahakamani.
kifupi its too leiiiiiit sio mwanachama tena wa cdm icpokuwa kwa mahakama tuuu
 
kinachomsumbua zitto sio kingine bali wivu dhidi ya mbowe,zitto anatamani sana kuitwa kamanda wa anga.....ila amesahau hayo yote yametokana na ubunifu wa mbowe....kwa yote niliyosikia kuhusu mbowe kamanda wa anga bado nina imani naye kwakuwa kipindi chote cha uongozi wake chama hakijawahi kushuka😛eace:
 
Mavi ya kale hayanuki hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu
 
Kwa bhata mbaya,,,ni kama amechelewa,lakin najiuliza haya mambo yana tija kwetu???wananch wa kawaida kabisa

Ndio yana tija make yanawaanika watu wanaokuja kutuomba ridhaa kila baada ya miaka 5 ili tuwapime kama ni wasafi au lah. Zinduka ndugu.
 
Wakati tukisubiri CHADEMA "wajifafanue" kuhusu mtafaruku huu ambao, bila shaka kabisa, umeharibu sana taswira ya chama, Serikali nayo iwe makini. Siku zote tumekuwa tukiamini marehemu Chacha Wange alifariki katika ajali ya kawaida, lakini kwa kauli iliyotoka kwa Mh. ZZK, basi vyombo vya Dola viifanyie kazi. Kwa kuanzia ZZK na Mbowe wahojiwe kikamilifu hadi tuondolewe shaka kabisa kuhusu kifo hicho.

Ni unafiki mkubwa kwa Watanzania kujidai tunajenga taifa la amani huku idadi ya misiba isiyoeleweka au kuelezeka ikizidi kuongezeka. Inawezekana wanasiasa wananufaika kwa kuacha mashaka katika mambo muhimu lakini sisi ni binadamu kwanza kabla hatujajumuika katika jamii zetu mbalimbali ziwe za kiukoo, kikabila, kidini, kisiasa, n.k. CHADEMA inaweza kujiadhiri kiasi chochote na hata kufa ikitaka, lakini haikubaliki katika "michezo ya kisiasa" maisha ya binadamu nayo yachezewe kiasi hiki - hata kama ni kwa kauli za kizushi tu; lazima watu wawajibike. Kama aliuawa, wauaji wachukuliwe hatua; kama ni uzushi, mpayukaji naye achukuliwe hatua. Hiki sio kitu cha kujinasibu nacho.


Mkuu ata wachangiaji humu nashindwa kuwaelewa! Kwanini wasihoji au kuchangia juu kifo ch Chacha Wangwe Km ZZK alivyozungumza kupata uhalali Wa tuhuma zote za ZZK dhidi ya Mbowe na Cdm?

Maana kwa kauli ya ZZK juu ya kifo cha Wangwe tumepata pa kuanzia!
 
Leo nikiwa makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibroad slaa amerusha kombora kwa Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA Mheshimiwa Zitto Kabwe.


Kwa mujibu wa Dk Slaa,Zitto kabwe ni mnafiki mkubwa kumuhusisha mwenyekiti wa CHADEMA taifa mheshimiwa Freeman Mbowe na ufisadi wa kupokea pesa kutoka kwa Mheshimiwa Nimrod Mkono.


Dk Slaa amesema,ZITTO alikuwa wapi kufichua ufisadi huo hadharani wakati wa vikao vya chama tangu mwaka 2005 aje atoe shutuma na malalamiko yasiyo na ukweli leo anaposhughulikiwa na chama???.


Dk Slaa amesema, lengo la ccm,Zitto na vibaraka wote wa ccm akiwepo Habibu Mchange ni kutaka Mbowe na Dk Slaa wakosane ili chama kiyumbe ili wapate pa kusemea. Dk Slaa amesema Ccm na vibaraka wake walifanikiwa kuiangamiza NCCR-Mageuzi, TLP na UDP lakini mbinu hiyo chafu inayotumiwa na Ccm kupitia kwa Zitto haitafanikiwa kuiua CHADEMA.

Mapambano yanaendelea.
 
uzalendo uko wapi kila siku me nasema mtanzania ukombozi uko mikononi mwako hakuna mwanasiasa hata mmoja atakeye kukomboa kila mmoja ana matwaka yake, kwanza kubali ukatae lengo la mwanasiasa yoyote ni kupata madaraka bila kujali hayo madaraka atayapata katika mazingira gani? siasa za TANZANIA kwa sasa zimegeuka kuwa uchafu huyu anakuja na hili kesho huyu anakuja na lile, huku wakiacha kushughurikia matatizo ya watanzania, mtanzania amka tena amka acha kulala jikomboe mwenyewe.....wakati wanasiasa wanakula vinono wananchi tunatabika na kufa njaa huku wao wakichukua viposho vikubwa ss hatuna hata mia mfukoni je hawa wana nia nzuri na wewe.........fikra makini huzaa busara makini mikono yako ndo ukombozi wako
 
Huna kingine cha kuongea!? Maana hicho hakina umuhimu wa kuwepo hapa! Ongea point. Sio mipasho!

Afukuziwe mbali huyu zito...wakati wa kifo cha chacha wangwe alikuwa wapi asiongee huu uzandiki na uongo mpaka aje aongee wakati anafukuzwa chadema. Zito ni fisadi na mnafiki hafai hata kdg jamii inapaswa kumchukiya
 
Mbowe katuvunja moyo sana! Sikutarajia ujinga huu kutoka kwake

Unafikiri mbowe kakuvunja moyo zaidi kuliko aliye pewa suti yeye aka sign mkataba wa madini na gas??hahahaaaaaaaaa! Embu fungua akili kidogo basi achana na hivyo vituhuma vya kuokoteza ili kutafuta huruma ya kamati kuu'. Wewe lowasa anayajua mangapi ya jk. Lakini alipo tolewa uwaziri mkuu ameendelea na mambo yake? Zitto bado bwa mdogo sana kiakili bado ana zile zama za ''kanunua simu kampa demu walipo achana kampokonyaaaaaaaa" ni maneno tuu mkuu usihofu, waimbaji bwana utafikiri walijua zitto atamaanisha wimbo wao.
 
kwanini aliamua kuedit post ya awali? Nani alimshauri? Alipanic?
 
Leo ni mekata tamaa kuhusiana na siasa hasa za bongo mpinzani kupewa au kukopa pesa kwa mtu ambaye anasadikika ni fisadi na wachama tawala.Je mbavu za kumkosoa na kumwajibisha huyo wa chama tawala atakuwa nazo?

Kweli siasa mchezo mchafu.

source:gazeti la Rai

Mkuu,usiamini hilo gazeti mia kwa mia,sbr kauli rasmi ya Mbowe,Dr Kitila na zzk ni waandishi wa makala humo,yawezakuwa Mbowe amelishwa maneno
 
Punguka mihemko.... wamemwaga mboga naye kamwaga ugali.. tatizo liko wapi? Pipooooooz!!! GONGO FC UFIPA.

Kuna majitu yana mtetea mbowe wakati mbowe mwenyewe kakubali leo kuwa alipokea hizo hela lakini hazikua na lengo la kusaliti chama! Lakini alipokea hela za mafisadi
 
Back
Top Bottom