Kwa nini hajasema hivyo? Na unajuaje kwamba hakupewa magari na kuyauza au kuyatoa kwa watu wake?
The fact kwamba ana magari mawili tu haimaanishi kwamba hajapewa magari na Mkono.
Nilitegemea kama hajapewa magari na Mkono, aseme "sijawahi kupewa magari na Mkono, kama una uthibitisho uweke wazi". Hii ndiyo kauli mtu mwenye uhakika kwamba hajawahi kupewa magari na Mkono anatakiwa kuitoa.
Sijaona kauli kama hii kutoka kwa Zitto, kama umeiona naomba utusaidie hapa.
La, kwa kutoweka wazi habari hii ya kupewa magari na Mkono, wengine tunaona anakwepa kujibu suala kwa sababu alipewa kweli.
Walatini wanasema "Qui tacit consentire", that means "silence implies consent".
Ukishutumiwa, usipojibu shutuma ila na wewe kuanza kutoa shutuma dhidi ya aliyekushutumu, wasomi wa mambo haya wanaojua tricks of the game wanapata nafasi ya kuamini kwamba zile shutuma ulizoshutumiwa awali, maadam hazijajibiwa, ni za kweli.
Na labda hazijajibiwa kwa sababu ni za kweli, hazina jibu zaidi ya kukubali hatia.
Na Zitto kaona bora kutojibu kuliko kukubali hatia.