Zitto ataka wanaoikosoa ACT-Wazalendo waanzishe chama chao

Zitto Kabwe yuko sahihi!

Chadema usoni mnajifanya kukomaa lakini ruzuku ya wabunge wa viti maalumu mnapokea!
 
Huwezi ona ni mbaya kama wewe ni mwana ACT mfia chama!! Binadamu huwa tunapenda vyetu bana
 
Wakati anasema atampigia kula tutundulisu mlimwita shujaaa. Ila Leo kwakuwa amegoma kutengeneza kiki yakusema anatishiwa ili akaishi ugaibuni kama hiyo michezo mnayocheza kwenye kikundi chenu, leo hiii unamwita msaliti. Huuu ndo mwisho wa kiki na maigizo yenuu
 
Wanasiasa wanategemea siasa kuishi,sasa kama eisitii wamepata nafasi sidhani kama wangekataa,ndiyo maana da Halima aliona waende tu bungeni na wenzake

Halima hakwenda kwa ruhusa ya chama, ni tofauti na Zitto wao ni uamuzi wa chama.
 
Swadakta, Umesema vyema kabisa. Mfano mzuri ni mwasiasa mashuhuri wa ACT- Maganga alijiondoa chama hicho baada ya kuona Zitto hafai. Akajiunga na chama kingine, sijui kama kafanya makubwa sana huko ili kutimiza matakwa yao dhikdi ya chama tawala.

Huu ni mfano mmoja tu, kuna wengi waliondoka na kusema baada ya uchaguzi jina Zitto litafutika katika medani ya siasa na hivyo kufutika midomoni mwa wananchi. Cha ajabu nyie ndio mnaempaisha Zitto mitandaoni na mitaani. Mmmm hili jina kubwa! Dua la kuku halimpati mwewe.
 
Wenzetu Wachadema wanamuamini sana zitto,sijajua wanatumia kigezo gani kushirikiana huyu MHA
 
Mbona hajakosea cho chote kwenye tweet hiyo. Kawaambia ukweli mtu. Hiko chama cha ACT alikianzisha mwenyewe baada ya kufukuzwa na akina Tundu Lissu huko chadema. Amehangaika kukijenga kutoka zero level hadi hapo kilipofikia, na anaendelea kuhangaika nacho kukijenga. Kimezidi kuimarika. Kupasuka kwa CUF vipande vikubwa viwili kilicholeta pande moja kuu chini ya jemadali la siasa za upinzani Tanzania kujiunga na chama chake, kimezidi kuimarisha chama chake. Akina Lissu and Company wamejawa na wivu kwa mafanikio yake hayo. Wanataka wambomolee chama chake.

Ndiyo ukweli kwamba hivi vyama mnavyovishabikia vina wenyewe. Ni mali yao na na vinatakiwa viwanufaishe. Chadema ni mali ya Mzee Mtei upende usipende. Ni CCM tu ndiyo haina mwenyewe kwani historia ya uanzishaji wake miaka hiyo ya 1920s ni tofauti kabisa. Hakuna mtu ye yote ambaye anaweza kudai kwamba ccm ni ya kwake. Ni kama zilivyo club za Yanga na Simba, hakuna anayeweza kudai kuwa ni mali zake.
 
Hivi mnabishanaje na mtu ambaye alishafika bei siku nyingi? Wao na Maalim Sefu ni Wamoja. Maalim Sefu bado alikuwa anapokea mshahara wa serikali na alikuwa kazi kubwa ya kuvuruga na amemaliza amepewa cha kustaafia.
Never believe a politician. All are liers.

No kama wale waluolipa wanawaamini Mwema, Marando, na Membe ambao ni Waandamizi Wakuu "Agents" . Yaani kabisa hawa wawe wapinzani? Akili nyingine utafikiri zilichomolewa zikajazwa pumba za mtama.
 
CCM siyo Saccos bali Chama cha Siasa Cha Wanachama tofauti na Vyama vya Upinzani ambavyo ni mali na watu siyo vya wanachama.

CCM sio chama cha siasa, bali ni kikundi cha dola kilochovaa koti la chama cha siasa. Chini ya awamu hii, CCM ndio imekata Ile shaka yetu kuwa CCM ni chama cha siasa. Rejea Magufuli alipopokea WanaCCM kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha. Fahamu kuwa jeshi limetengwa rasmi na siasa kikatiba, lakini siku Ile hilo lilifanyika mchana kweupe bila kujali katiba inasemaje.
 
Wanasiasa wanategemea siasa kuishi,sasa kama eisitii wamepata nafasi sidhani kama wangekataa,ndiyo maana da Halima aliona waende tu bungeni na wenzake
Kila mtu anategemea kazi yake kuishi. Mwalimu anategemea ualimu kuishi, mhandisi anategemea uhandisi, mkulima anategemea kilimo, mwanasiasa anategemea siasa, wewe unategeme uchikwuemeka na kadhalika. Ndiyo dunia inatutaka tuishi, tupate chakula kwa jasho letu kwa kufanya kazi. Siasa ni kazi kama kazi zingine.
 
Kwanini chadema mnaumia sana na mambo ya ACT?
Kuwa chama cha pili cha upinzani ni pigo kubwa kwa chadema.

Ushauri wangu kwa CHADEMA: Waungeni mkono ACT ili CCM wasipate nafasi ya kuwagawa. Hii ndio dawa pekee ya kuishinda CCM.
 
Eeenh Heee, ameiga tu huyo; kwani wewe huoni kile chama kubwa ilivyofanywa kuwa mali ya mtu? Ni nani anafurukuta mbele ya mwenye chama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…