View attachment 2032644
Utukufu wa Mungu ni wa ajabu sana ! Leo Mtukufu Rais kwa kinywa chake mwenyewe ametamka kwamba ameona mambo ya hovyo ambayo amebambikiwa na awamu zilizopita , ameongea mengi na kukemea vikali kundi la watu waliomuangushia gari bovu kwenye awamu yake kwa lengo la kumchafua .
Mh Samia hakuwataja wapinzani , bali amewataja wanaccm wenzake na viongozi waliomo kwenye serikali yake mwenyewe , hawa watu wa hovyo ndio walewale waliokuwemo kwenye awamu ya 5 , hawa ndio waliomuangushia gari bovu mama na kumlisha maneno ya uongo ya kwamba Freeman Mbowe ni Gaidi , Njama zote za kumbambika kesi ya Uongo ya Ugaidi Mbowe zilipangwa kwenye awamu ya 5 na hawa hawa watu wa hovyo waliotajwa leo
Kesi ya uongo iliyofunguliwa kishamba sana bila hata ushahidi wa kuthibitisha ugaidi wa Mbowe , sasa inadhalilisha Nchi kila mahali duniani , mliyoyasikia huko EU ni ushahidi wa kwamba hili ni gari bovu aliloangushiwa mama na utawala uliopita kwa msaada wa vyombo vya dola , ANAPASWA KUTOONA AIBU KUIFUTA KESI HII ILI KULINDA HESHIMA YA UTAWALA WAKE , na baada ya kufuta uchafu huu unaoleta harufu kali na mbaya duniani kote , tunaamini atafanya mabadiliko kwenye uongozi wa vyombo vya dola nchini , Ili kuondoa watu wa hovyo wanamuangushia gari bovu
KUANZA UPYA SI UJINGA .