Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Inshu ni mameli makubwa ambayo hatujawahi kuyaona au tunahitaji mkataba upoje? Wekeni mkataba wazi tumalize mjadala vinginevyo hizo ni ngonjera tu ambazo hazina mwisho,hamna anayekataa kujengwa hiyo bandari ila tunaomba tujue yaliyomo ndani ya mkataba!
 
Hilo la kuuza nchi umeambiwa namwenda zake ikulu tu ndiyo wenye huo mkataba, kwanini usiwekwe wazi tu.
Kumbuka aliyekwambia yaliyomo ndiye huyo huyo aliyekwambia ATCL inatengeneza faida. Sikatai alichosema huenda ni kweli lakini ingekuwa vizuri ukiwekwa wazi ukajadiliwa tukawa na uhakika kuliko kuambiwa tu.
 
Mkataba sidhani kama utawekwa wazi. Na sababu ni kuwa siyo rafiki kwa nchi yetu. Hapa natumia hisia na uzoefu wangu kwa viongozi wetu.
 
Kwenye hii video hapa chini, Magufuli mwenyewe anausifu mradi wa bandari bagamoyo, anasema nothing will change kwenye huu mradi, nashangaa alikuja kugeuka baadae.

Your browser is not able to display this video.
 
Mkataba sidhani kama utawekwa wazi. Na sababu ni kuwa siyo rafiki kwa nchi yetu. Hapa natumia hisia na uzoefu wangu kwa viongozi wetu.
Kwani waliutekeleza? Kama hawakuutekeleza na siyo rafiki kwanini usiwekwe wazi? Maana siyo mkataba wamambo jeshi waweke wazi tuone kaa kweli nchi ilitaka kuuzwa maana aliyeuoana akatwambia ndiyr pia alitwambia ATCL inatengeneza faida na gawio likaletwa, ni afadhali uwekwe wazi tuache kusikia sikia tu tuwe na hakika na yaliyomo.
Yeye Zitto kasema kwakuwa hajui yaliyomo yeye aliona tu presentation, kama wale walikuwa na terms mbaya tunaweza tafuta washirika wengine au serikali ikajenga yenyewe ila anachelea kwa ukubwa wa bandari ile serikali haiwezi kuijenga bila usadizi.
Mimi ningependa wasifanye move bila kuweka mkataba wazi kama alivyosema zitto.
 
Sijui kwa nini tu huyu jamaa huwa siamini ayasemayo....

MNAFIKI!
Kwa hiyo hayo mameli makubwa tutayaona bagamoyo tu!! Zitto ovyo sana

MUUNGANO WA TANZANIA NI PAMOJA NA ZANZIBAR. SASA ZANZIBAR WANAJENGA BANDARI AMBAYO ITAKIDHI MAHITAJI YA MELI KUBWA , SASA KUNA SABABU GANI YA KUNG'ANG'ANIA KUJENGA BAGAMOYO KAMA SIO UFISADI WA HIYO HONGO YA WACHINA? MUDA UKIFIKA KAMA ITAKUWA NI LAZIMA BANDALI INAWEZA KUJENGWA MWAMBANI NA SIO LAZIMA BAGAMOYO NA SIO IWE NA MKOPO KUTOKA CHINA!
 
Hilo pia kalisema kuwa Oman ambao walikuwa washiriki kwenye huo mradi sasa hivi wanajenga zanzibar hivyo hatuwezi tenakujenga hiyo bandari labda watafute jinsi gani bandari kama wakiamua kujega zitakavyoweza kushirikiana kufanya kazi kwa pamoja.
Mnaomponda hamkumsikiliza laiti mngesikiliza msingekuwa mnamponda hapa.
 
Ni kijana aliyesoma uchumi lakini hajawahi kutumia elimu hiyo. Wakati anasema hayo lazima aelewe umuhimu Wa Durban ktk Afrika. Huwezi kuwa na matumaini ya muwekezaji eti meli kubwa zitakuja hapo Utadhani dunia nzima itatawaliwa na China. East Africa ina nchi 6 au saba ukiweka na visiwa vya Seychelles. Yaani Spain ilete bidhaa afrika ilazimike kuja Bagamoyo bila sababu wakati inapeleka bidhaa Durban! Wao wanataka kuiteka TZ na madini yake na ndo maana wanataka kukamata bandari zingine za TZ ziwe kwao.
 
Ndio maana siku zote huwa nasema Uchumi sio proffesion kama engineering, sheria etc.

Sijawahi kuta mchumi anaye ongea mambo ya maana zaidi ya porojo.[emoji1]
 
Ata mababu zetu waliletewa shanga zinazong'aa ambazo hawakuwahi kuziona Duniani na wakabadilishana na mapande ya almasi na Gold...by the way, hizo meli zitatoka Mars?! Au Bwana zitto anataka kutuambia yeye ndio katembea dunia hii kuliko Watanzania wote.? Politicians sometimes have to learn to respect other people from different walk of life..wasidhani wao ndio wanajua kila kitu.
 
Anajulikana sio mpk umsikilize.
Kinyonga at work
Hii tabia ya kushambulia watu bila kusikiliza hoja zao inashangaza. Hebu jaribu kuweka hisia zako pembeni kamsikilize halafu rudi uchangie.
Katoa maelezo mazuri sana.
1. Katwambia walichoona wao na wabunge wengine ni presentation ya hiyo bandari.
2. Ile haikuwa bandari ya kawaida kama iliyokuwepo bali ililenga kupokea meli kubwa sana zishushe mizigo halafu meli hizi tulizozoea ziichukue na kuisambaza afrika na kwingineko.
3. Ingemaliza ingekuwa bandari ya 3 kwa ukunwa duniani
4. Hata bunge halikuwahi kuona mkataba wake ni ikulu tu waliyouona hivyo hata wao hawajui kilichomo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwendazake, hivyo ingekuwa bora ungewekwa wazi ili watu wauchambua tujue yaliyomo.
5. Bandari ilikuwa ijengwe kwa ushirikiano wa Tanzania, China na Oman
6. Raisi Mwinyi ashawawahi waomna watajenga bandari zanzibar, hivyo anaona hakuna tena umuhimu wa kujenga bandari ya bagamoyo unless iwepo plan ya hiz bandari kushirikiana maana sisi ni nchi moja.
Sasa wapi alipokosea?
 
Africa is always the victim, nothing is ever our fault. Yaani kila muwekezaji ni mbaya na anataka kutuibia.
Huo ndo ukweli. Hakuna muwekezaji anayekuja nchi nyingine bila manufaa yake kwanza, Ni muhimu atuoneshe manufaa yetu. Tafuta nchi gani ya Afrika imenufaika na wawekezaji wa nje.

Elewa pia tabia ya weupe, tangu waarabu nenda kwa wazungu. Popote walipo huamini hatuko kwenye kiwango kimoja cha ubinadamu. Kwa Asia ndo kabisaaa! Sasa usiwe na matumaini kwamba unazungumza nao wakikupa thamani kama wewe unavyowapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…