Sawa mkuu lakini hata ingekuwa ya kwanza kuna faida gani kama tunauza nchi? Vitu vingine inabidi watu waangalia kwa mapana na marefu. BTW walishatishia siku nyingi kuwa hao wawekezaji wameshaondoka kujenga sehemu nyingine lakini nashangaa kumbe bado wanafukuzia. Hivi faida kwa nchi ingekuwa nzuri kihivyo Tanzania tangu Tanzania waanze kusuasua kuhusu huu mradi si ungekuta nchi nyingine zimeshawachukuwa? Kwani Tanzania ndiyo nchi pekee yenye bandari Afrika? Chema cahajiuza, kibaya chajitembeza. All in all uwekwe wazi huo mkataba kama wana nia njema. Tuwe makini tutajikuta siku sijazo tuna vikosi vya kupigania ardhi ya Tanzania iliyoporwa. Na wawekezaji wa mradi mkubwa kama huo hawaingii hivi hivi. Wanahakikisha watakuwa na uwezo wa ku-influence uchaguzi wa nchi husika ili asipatakine rais atakayewageuka. Anyways sioni wa kuuzuia tena huu mradi baada ya Magufuli kuondoka. Ndiyo maana unaona wameshajitokeza watu wanaopiga kelele mara hii.