Zitto Kabwe: Katika ndege 12 alizonunua Hayati Magufuli, ndege 6 hazifanyi kazi, ziko grounded, zina kutu, ingawa tuliambiwa ni mpya

Zitto Kabwe: Katika ndege 12 alizonunua Hayati Magufuli, ndege 6 hazifanyi kazi, ziko grounded, zina kutu, ingawa tuliambiwa ni mpya

..usimshambulie Zitto binafsi, shambulia hoja yake.

..hivi unaona ni sahihi ndege hizo 6 kuwa grounded muda mfupi baada ya kununuliwa?
Sasa ndege inarushwa bila kufanyiwa service na hata bajeti ya service watu wanapiga unategemea hiyo ndege hata kama ilikuwa mpya itakuwa imara tena?

Unajua muda mwingine huwa natazama umashuhuri wa huyu jamaa zitto kabwe kwasasa ndipo nagundua jamaa hana jipya la kuoffer kwenye political platform ya Tanzania zaidi ya kuongea vitu ambavyo havina ukweli.

Sasa wewe watu wanaiba mabilion ya pesa sasa hivi huwezi sikia akikazania. Ila kila anapokwenda yeye ni magufuri hiki magufuri kile yaani utadhani yule mzee alimgongea mkewe sasa anakisirani naye. [emoji23][emoji23][emoji23]

Jamaa ni mpumbavu sana huyu miaka hii sijui ndio wenge la umri kwenda.
 
Wakati mnashangilia manunuzi yale ya kihuni si mlikuwa mnataka kuonekana wajanja? Kelele zilipigwa kuwa dhalimu anachofanya sio sawa, mkawa mnaenda uwanja wa ndege kupokea mitumba mkisaka sifa za kisiasa na kuchafua wapinzani kubwa hawataki maendeleo. Mmechukua hela za wakulima wa korosho bila kufuata utaratibu, saa hii mnataka mpewe ushauri.
Mimi hayanihisu hayo
Wewe umekuwa mnajimu au mganga kujua kuwa mimi ni mmoja wenu huko?

Ukiwa mtu wa dhana ni moja ya unafiki
Jifunze kutokudhania mtu badala yake andika kwa wahusika tu

Mimi niko nje ya nchi tangu 1989 hizo siasa zenu mmalizane wenyewe

Kwa kukusaidia humu wamo mpaka wabangaladeshi na mpaka walioko Mexico wanachangia humu
Jifunze kujadili kwenye mitandao huru
Nimechangia hoja tu mengine mtapambana wenyewe

Wizi wa hizo ndege tunajua sasa nini kifanyike ndio suala Zima hapa
Na sio mapambio
 
hata nyumba ikijenga mpya baada ya muda ikikaa bila watu inachakaa sasa ndege kuwa na kutu sio sababu ya kuwa zilikuwa sio mpya.
 
Zilikuwa zinahatamia toka jiwe akiwa hai, zilipofika tu ziliandaliwa viota zikataga na mpaka sasa zinalalia, hayo mayai tayari ni viza.
Acha uongo bwana. Ndege huwa zinataratibu zake sio daladala ile kusema itapeleka abiria na kugeuka kuwahi wengine huku ikisimama njiani kupiga debe.

Ndege inatakiwa service kubwa na ndogo kwa kila mruko na ndio maana kwenye kila airport kunakuwa na karakana ndogo na kubwa ili ndege zinazoonyesha hitilafu ndogo ndogo zinachekiwa zikitua kufikisha abiria na kuondoka na kufanyiwa check up kubwa zikirejea zilipotoka.

Serikali sababu ya kuwa na msururu wa watendaji wazembe na wapigaji wasiokuwa na mbinu za kuendesha mashirika kwa faida huwa pesa za miradi kama hii kutokea hazina hazifiki hadi chini na zikifika hazitoshi so kunatokea magepu mengi sana na matokeo ndio hivyo.

Usimamizi mbovu ndio tatizo sio rais aliyenunua ndege.
 
Zilikuwa zinahatamia toka jiwe akiwa hai, zilipofika tu ziliandaliwa viota zikataga na mpaka sasa zinalalia, hayo mayai tayari ni viza.
lakina sio kazi ya Rais tena kuna wahusika waliokuwa wanapaswa kufanya kazi yao ulitaka rais akafanye tena kazi huko airport?
 
..usimshambulie Zitto binafsi, shambulia hoja yake.

..hivi unaona ni sahihi ndege hizo 6 kuwa grounded muda mfupi baada ya kununuliwa?
Jukumu la kuzifanyia service au matengenezo ni la nani? Marehenu au mama yako?
 
This is illogical and nonsensical.

Tatizo sio mnunuzi ila walioachiwa kuendesha. Unaweza pesa gari mpya Leo ila kama hulitunzi na kulifanya service litakufa tu in no time.

Kuna watu ukiona simu zao utadhani walinunua miaka ya 90 kumbe za mwaka huu huu 2023.

Uchakavu wa kitu ni utunzaji wa mmiliki mwenyewe sio manufacturer au mnunuzi.

Nipo around mazee.
Kabisa yaani.
 
Kitendo cha kununua Ndege 12 kwa muhula mmoja ya uongozi ni ufisadi uliokithiri.

Tena huku ukikataa manunuzi yake kukaguliwa na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.

Kwanini basi ungeanza hata na Ndege mbili ukaona Tija yake yake ndio utathimini kuongeza au vinginevyo.
Ogopa sana mtu anayejiita mwenyewe kuwa ni Mzalendo.
Zile ndege zote kwa jumla hazifiki hata trilioni mbili. Hii ni hela ambayo kwa kutazama ile miamala aliyokuwa anaikusanya kwenye malipo ya kodi mbalimbali huku chini ukichanganya na vyanzo vingine kama malipo ya tanesco, na makampuni mengine yaani hiyo ni hela ndogo sana.

Tatizo letu watanzania huwa kutumia akili sijajua tunafeli wapi. Ni kwann kipindi cha magufuri waliokuwa wakilalamika sana kupita maelezo hadi michozi walikuwa ni viongozi, watoto wao, hawa viongozi wa upinzani, wamiliki wa NGO's, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa etc na wananchi wa kawaida walikuwa poa tu na wengi wao hawakuwa wakipitia hali kama ya sasa.

Haujiulizi kwann sasa hivi hawa viongozi wakubwa, wadau wao, washirika, viongozi wa upinzani etc, wanashindwa kumtamka magufuri hata kwa zuri hata moja, ingawa mambo aliyofanya mengine yanawafaidisha kwa sasa?

Kimsingi kuna siri nzito sana inafichwa na hili kundi la mchwa ambalo wanataka wao pekee yao ndio wafaidike na rasilimali za hili taifa. Kwakifupi hawa watu wameshakuwa compromised inapokuja swala la masilahi ya taifa.

Zile ndege ni chache sana kwa idadi ya mikoa tuliyo nayo. Lengo kuu ni kila mkoa at least uwe na ndege mbili au tatu ambazo zinapiga safari ili kuboost Biashara na mawasiliano. Hizi ndege aina ya bombardier ni ndege nafuu sana kumaintain na hazina usumbufu kama watu wanakuwa serious na biashara.

Zile story za sio lazima kununua ndege unaweza kukodi ni story za kibiashara tu. Unaweza kununua ndege zako hata mia ukiwa na watendaji wazuri faida utaiona na utakuwa na afadhali kuliko yule anayekodi. Sema watanzania tuna kasumba moja, yaani jambo akisema mzungu basi linakuwa kama ibada yaani mwafrika hawezi waza nje ya akili ya maneno ya mzungu.

Mzungu alisema ukitembea kwenye jua kali la mchana utapata kansa ya ngozi. Ofcourse ni kweli ila kwa mtu mwenye albinism na wazungu wenyewe hili jua lina madhara. Ila waafrika unakuta nao wanacopy hii habari wanapakaa sunscreen kwenye ngozi ili watembee juani sasa wewe jua likikupiga una melanin ambayo inafanya ulinzi wa ngozi yako bila hata wewe kuwaza chochote unahangaika na sunscreen ya kazi gani? Machinga wote na wakulima wanaoshinda juani si wangejaa pale Ocean road kutibu kansa ya ngozi.

Juzi kati wakati wa korona, Magufuri akawakataza lock down mkasema vibaya mzee wa watu kuwa hajielewi sijui nini na nini, mzee alikomaa kweli kweli, mwisho wa siku aibu ikawarudia wanaharakati wa mchongo. Corona mbona haikusambaa na kuua inchi nzima?!

Wazungu wameshika sana vichwa vyetu kiasi kwamba tunaamini wapo accurate kwa 100% kumbe sio kweli na always hiyo haiwezi tokea. Tuwe tunatumia akili zetu.

Hawa viongozi uchwara akina Zitto wanalipwa kufanya uhaini ninyi mnawaona icon.
 
..Zitto amesema ziko grounded kwasababu ya ubovu, sio hicho unachosema wewe.
Hawajielewi hawa watu. Zitto akiongea pumba zake, followers wake wanaunganisha hasira za ugumu wa maisha, kuachwa, na stress zingine wanakuja kumuunga mkono kwa kumtukana Hayati ambaye ni mwaka wa pili sasa toka ametutoka.
 
Zitto ametoa tuhuma nyingi dhidi ya Hayati Magufuli na utawala wake.

Mojawapo ni hiyo ya ndege 6 alizonunua Hayati Magufuli kuwa grounded wakati tuliambiwa ni ndege mpya.

Nasubiri kusikia kama Serikali au ATCL watakanusha tuhuma hizi.

Majibu ya ATCL, soma ATCL: Ndege mbili zina shida ya Injini. Ndege moja imekamatwa Uholanzi. Si kweli kuwa ndege sita hazifanyi kazi


Mbona hata Bunge la Mwendazake lilishasema haya kupitia Mbunge wa Kamati ya PAC bwana Robert Mbonaliba a.k.a Obama.

Zile ndege pia na ATCL CAG alishasema kila kitu.
 
Shekhe Zitto anafahamu fika kabisa kwamba, ikiwa tu binadamu hufikwa na magonjwa! Je hayo machuma ambayo leo yapo miaka 6 yakitumika mafuta yasiharibike na kufanyiwa ukarabati?

Hoja ya kwamba ndege zipo benchi zikiwa na kutu huo ni uwongo wa kijinga!
Jibu hoja acha porojo.
 
Mapangaboi yako chini. Yaani ndege mpya hata miaka mitano haijafika tayari iko chini....tulipigwa
Kumtukana JPM hakuta kujenga kisiasa hata watu wa kigoma watakukataa labda upewe ubunge wa mchogo ili kulipwa fadhila za aliyekutuma kumchafua JPMi
 
Kwaiyo kama zipo grounded ni Kosa la mbeba maono alozinunua au waendeshaji wa shirika wa Sasa au unataka JPM afufuke ili aliendeshe hilo shirika?

Hivi kama ukijenga nyumba warithi wako wakaamua kuigeuza ile nyumba danguro inabidi tukulaumu wewe kwa kujenga hiyo nyumba?

Zito Hana hoja ni shoga tu la kisiasa lenye njaa.
Kabla ujafa kuna watu walikushauri usijenge hayo majumba ila wewe ukakaidi na kujenga. Leo hayo majumba ni madanguru..je waliogeuza yawe madanguro na wewe uliekaidi ushauri nani wakubeba lawama? KARIBU
 
Back
Top Bottom