Kitendo cha kununua Ndege 12 kwa muhula mmoja ya uongozi ni ufisadi uliokithiri.
Tena huku ukikataa manunuzi yake kukaguliwa na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali.
Kwanini basi ungeanza hata na Ndege mbili ukaona Tija yake yake ndio utathimini kuongeza au vinginevyo.
Ogopa sana mtu anayejiita mwenyewe kuwa ni Mzalendo.
Zile ndege zote kwa jumla hazifiki hata trilioni mbili. Hii ni hela ambayo kwa kutazama ile miamala aliyokuwa anaikusanya kwenye malipo ya kodi mbalimbali huku chini ukichanganya na vyanzo vingine kama malipo ya tanesco, na makampuni mengine yaani hiyo ni hela ndogo sana.
Tatizo letu watanzania huwa kutumia akili sijajua tunafeli wapi. Ni kwann kipindi cha magufuri waliokuwa wakilalamika sana kupita maelezo hadi michozi walikuwa ni viongozi, watoto wao, hawa viongozi wa upinzani, wamiliki wa NGO's, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa etc na wananchi wa kawaida walikuwa poa tu na wengi wao hawakuwa wakipitia hali kama ya sasa.
Haujiulizi kwann sasa hivi hawa viongozi wakubwa, wadau wao, washirika, viongozi wa upinzani etc, wanashindwa kumtamka magufuri hata kwa zuri hata moja, ingawa mambo aliyofanya mengine yanawafaidisha kwa sasa?
Kimsingi kuna siri nzito sana inafichwa na hili kundi la mchwa ambalo wanataka wao pekee yao ndio wafaidike na rasilimali za hili taifa. Kwakifupi hawa watu wameshakuwa compromised inapokuja swala la masilahi ya taifa.
Zile ndege ni chache sana kwa idadi ya mikoa tuliyo nayo. Lengo kuu ni kila mkoa at least uwe na ndege mbili au tatu ambazo zinapiga safari ili kuboost Biashara na mawasiliano. Hizi ndege aina ya bombardier ni ndege nafuu sana kumaintain na hazina usumbufu kama watu wanakuwa serious na biashara.
Zile story za sio lazima kununua ndege unaweza kukodi ni story za kibiashara tu. Unaweza kununua ndege zako hata mia ukiwa na watendaji wazuri faida utaiona na utakuwa na afadhali kuliko yule anayekodi. Sema watanzania tuna kasumba moja, yaani jambo akisema mzungu basi linakuwa kama ibada yaani mwafrika hawezi waza nje ya akili ya maneno ya mzungu.
Mzungu alisema ukitembea kwenye jua kali la mchana utapata kansa ya ngozi. Ofcourse ni kweli ila kwa mtu mwenye albinism na wazungu wenyewe hili jua lina madhara. Ila waafrika unakuta nao wanacopy hii habari wanapakaa sunscreen kwenye ngozi ili watembee juani sasa wewe jua likikupiga una melanin ambayo inafanya ulinzi wa ngozi yako bila hata wewe kuwaza chochote unahangaika na sunscreen ya kazi gani? Machinga wote na wakulima wanaoshinda juani si wangejaa pale Ocean road kutibu kansa ya ngozi.
Juzi kati wakati wa korona, Magufuri akawakataza lock down mkasema vibaya mzee wa watu kuwa hajielewi sijui nini na nini, mzee alikomaa kweli kweli, mwisho wa siku aibu ikawarudia wanaharakati wa mchongo. Corona mbona haikusambaa na kuua inchi nzima?!
Wazungu wameshika sana vichwa vyetu kiasi kwamba tunaamini wapo accurate kwa 100% kumbe sio kweli na always hiyo haiwezi tokea. Tuwe tunatumia akili zetu.
Hawa viongozi uchwara akina Zitto wanalipwa kufanya uhaini ninyi mnawaona icon.