MsemajiUkweli,
Natofautiana kidogo na wewe kumwona Zitto Kabwe kwa jicho hili....
Kwa maoni yangu wote wanataka kitu kimoja lakini kwa approach tofauti....
Zitto kwa mtazamo wake, anadhani njia hiyo anayoifikiria yeye, ndiyo the best approach kutatua mgogoro uliopo.....
Wenzake wa upande mwingine wanadhani meza ya mazungumzo ndiyo the best approach...
Wakati mwingine, approach zote mbili zinaweza kutumika...
Ya Zitto Kabwe Mara nyingi huwa ya mwisho baada ya meza ya mazungumzo (ndiyo hiki kinachoitwa maridhiano) kushindikana....
Ni jukumu letu wote kuamua tuzimalize kwa njia gani tofauti zetu za mitazamo ya kisiasa kwa sababu siasa ndiyo inayoamua maisha yetu ktk nyanja zote....
Tatizo ninaloliona mimi ni wenye madaraka na mamlaka ya kiserikali kuamini kuwa hicho kinachoitwa mgogoro wa kisiasa hakipo!!
Na kwamba kinachotafutwa na wanaoomba sisi kama jamaa kukaa meza moja "kuridhiana" si kuridhiana for real bali ni huu upande unaotaka hiyo kitu kutumia fursa hiyo kutaka kuharibu mikakati ya maendeleo ya wanaoongoza serikali na hivyo kufungua mlango wa kushindwa kwao kisiasa!!
Hapo ndipo lilipo tatizo yaani hakuna kuaminiana