Walichofanya cdm jana, nawaza angekifanya Zitto ingekuwaje?.
Walichofanya Cdm jana ndio alikuwa anakifanya Zitto nyakati za Kikwete akaitwa mnafiki, leo nisahihi kabisa Zitto kuwaita wanafiki Chadema maana waliyokuwa wanamtuhumu nayo, ndio wameanza kuyafanya.
Kamwe mwenye nguvu haombwi maridhiano, bali mwenye nguvu ndio huomba maridhiano pindi anapoona nguvu zake zinataka kupunguzwa na wafuasi wavyama vingine.
Chadema jana mmejidhalilisha na naamini JPM hatawapa nafasi ya maridhiano bali atawananga kwenye mikutano yake ijayo.
Inawezekana mlikuwa na lengo zuri, lkn sikwawakati huu baada yakususia uchanguzi wa vitongoji na vijiji.
Labda niulize tu Chadema wanaomba maridhiano ya nini?.
Waruhusiwe na Magufuli kufanya mikutano ya siasa?.
Wawaruhusu Wananchi kutambua viongozi wa serikali za mitaa?.
Mtu mnamtuhumu kawaua ndugu zenu kina Mawazo,Ben Saanane,kawapiga risasi ndugu zenu,kawafunga viongozi wenu,na anawambia mjaribu hata kumwaga mkojo muone chamtema kuni.
Mnamtuhumu ananunua viongozi wenu,mliomba viongozi wa dini wawaombee maridhiano lakin aliwapuuza leo mnaenda hadharani kuomba maridhiano.
Kipindi nyie mnataka kuacha siasa za kiharakati mrudi kwenye siasa za Zitto kabwe, mnaemuomba msamaha yeye anafanya siasa za kiharakati bila kujali nyie mtamuonaje.
Maridhiano hayaombwi bali yataletwa na mawazo Kama ya ukuta ukuta.
Yetu waungwana macho, tunasubir tuone itakuwaje, muda huwa mwalimu mzuri.
Zitto alikuwa na siasa za hivyo, za kukaa chini, AKATUKANWA NA KUITWA MAJINA YOTE, na hata bungeni zitto alimtambua JPM
CDM imeumizwa sana, mno, na imepotea na haina hata kiongozi mmoja wa serikali za mitaa. Mbowe kaona kabisa anapotea na chama chake na kaona the best way ni kuomba PO!!! bila kusahau anakiuza chama mchana kweupe mara ya pili
1. angeomba audience na rais alipokatza mikutano ya siasa; HAKUFANYA
2. Angeomba maridhiano baada ya yeye kuwekwa ndani na kesi hizi za akina akwilina, HAKUFANYA
3.Angeomba maridhiano kabla ya uchaguzi wa serikali za Mitaa , ambao ndio wa muhimu sana kuliko hata ubunge anaoutaka; HAKUFANYA
Watu wake akiwemo Lema, sugu,mdee, wamkuwa wakimtukana rais matusi ya aibu ya nguoni!!!! hivi anataka maridhiano gani?? wakati wao ndio hawana heshima na since day one walimkataa JPM???
Siasa za urafiki tulizihimiza sana, na Mbowe alipaswa kuwaziba midomo watu wake wasimtukane rais. RAIS katukanwa sana kipindi hiki kuliko nyakati zozote za maisha ya nchi hii
Maridhiano HAYAPO, kinachotokea CHADEMA inajizika kabisa, na hata wale wafuasi wanaojilewa SIDHANI kama wana nguvu
maria sarungu, fatuma karume, maaskofu wale wa kuandika vi article kigogo, etc. wanajuta hii leo
Before that tuliona akina mwanakijiji ambao walikuwa wanaipenda chadema kwa dhati wakibadioi ideology zao kwa CDM kumleta fisadi Lowassa, na kuwaacha watu kama akina SLAA...Ambaye alikuwa ICON ya upinzani
CDM haina baba, haina mama, haina uongozi, haina nguvu tena, maana imepoteza kila kitu. Kinachobakia ni Mbowe kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania, FINLAND, Lema kuwa board member wa chama cha pareto, na SUGU ubunge wake anajua hatapata yeye, atapangiwa majukumu mengine
NILIJUA KABISA KWA UELEWA WA SIASA ZA TANZANIA, issue ya kudeal na Magufuli ingefanyika kuanzia mwanzo kabisa bila kukata tamaa au kutulia....hapo katikataki kuna damage zimefanyika na hasa chadema ndio wameumiza watu na wamemuumiza rais, WATATAKIWA KUOMBA MSAMAHA KWA MATUSI NA DHARAU ZA WAZI, ikfika hatua hii ndio mtakumbuka maneno ya zitto
JPM, uzuri wake habadiliki, anapiga kazi, na kanyoosha mstari, haangalii jumuia za kimataifa wala za kinanilii
wale waliohama CDM kwenye CCM, walitukanwa pia............