Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Sheria imetamka wazi vipindi viwili renewable, unless otherwise iwepo sababu za kutokuendelea.
Kwa hiyo hamba option ya kumwo doa CAG kwa kipindi kimoja
kama hawezi kuondolewa baada ya kipindi kimoja walikuwa na maana gani ya kuweks renewable?
 
Sioni impact ya kesi hii kipindi hiki. Kama Mahakama baada ya kesi hii ingemrejesha Ptof. Assad kwenye nafasi yake ningeona umuhimu wa matokeo ya mashauri kama haya maana ni mengi.
Huioni faida Kwa sababu sheria zinakupita kushoto. Hii ni moja Kati ya hukumu zenye faida Sana nchini.
 
Kusemwa kwa kiongozi ni kawaida ila mimi nazungumzia kuchukiwa, jinsi anavyosemwa Magufuli na yanayoendelea huwezi kufananisha na hao viongozi wengine. Huyo Nyerere kumsema tu ni kama dhambi nakumbuka Lissu alivyomsemaga Nyerere jinsi watu walivyomjia juu anamkosea adabu Baba wa taifa, huyo Mkapa na Kikwete walisemwa kawaida tu hawakuchukiwa labda ndio hivyo walikuwa wanauma na kupuliza tofauti na Magufuli.

Leo hii ccm wenyewe wanaweza kumsema Marehemu(Magufuli) ila hawana ujasiri wa kumsema Mstaafu Kikwete, ndio maana nikasema huu uamuzi wa mahakama ni unafki tu ni katika muendelezo wa vita na marehemu.

Mtu kama Zitto hukuti anamkosoa rais Samia sasa ila ana muda wa kukosoa Marehemu hadi kwa hasira anafikia kutamka kuwaambia wenye kumpenda Magufuli wakazikwe naye, hiyo sio hali ya kawaida. Kwahiyo kilichotokea hakina maana yeyote kwa nchi ambayo tunajua isingeweza kutoa uamuzi huo kwa rais aliye madarakani na ndio maana nasema ni vita tu dhidi ya marehemu.
 
Sasa Kwanini Mahakama inatoa Majibu Leo?

Kwanini Haikuingilia kati wakati Ikiwa Inavunjwa kwa Wakati ule na Kuja Kujisemesha Leo?

Tanzania hakuna wakusimama na wananchi bila wanachi wenyewe kuamua 2025.
 
Rais alitakiw akushughulikia waloiba na sio Ashughulikiwe aliyeonesha wizi wakati ndio kazi yake ya kisheria.

Kifupi Jpm alikuwa fisadi
 
Msimamo wangu ni kwamba kuwa na katiba mpya huku tunaendelea na CCM ni ujinga kwa sababu hawata ifuata.
 
Haki iliyocheleweshwa Ni sawa TU na haki tuliyonyimwa.Uamuzi huu hauna msaada wowote kwa taifa kwa Sasa.Yaani mahakama inasubiri mpaka Magufuli afe ndo ijitutumue ! Ni sawa na uwe na ulinzi wa mbwa nyumbani,wezi waingie ndani ya nyumba,mbwa anaufyata mkia muda wote,Wezi wanaiba na kukomba kila Kitu na kuondoka,Halafu baada ya masaa let's say 10,NdoHuyo mbwa anaanza kuwabwekea.Shem on you !
 
Tuna safari ndefu sana kwenye kulinda na kuheshimu Katiba ya Nchi.
 
Hizo ni athari za utawala wa kidhalimu wa Magufuli. Kila rais wa CCM hatakubali mikutano tena, maana wanajua CCM haiko madarakani kwa ridhaa ya umma.
Kwahiyo katiba ifanyiwe marekebisho isomeke Hivyo !!
 
Tuna safari ndefu sana kwenye kulinda na kuheshimu Katiba ya Nchi.
Obama alisema Africa doesn’t need strong people! It needs strong institutions ! Sijui alikuwa ana maana gani !!!
 
Obama alisema Africa doesn’t need strong people! It needs strong institutions ! Sijui alikuwa ana maana gani !!!
Mahakama Imara
Bunge Huru
Polisi Huru
Tume huru ya Uchaguzi
Wizara zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba
Taasisi huru za Ujasusi
Haki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…