Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG


Kunywa kinywaji chochote nitalipa bro. Ulichoandika kimenisisimua.
 
Mbona wamesubiri afe ndiyo wakatoa hukumu?
 
 
Ndugu kila kitu sio udini, tukiwa hivyo mbona tujiharibia utu wetu.

Je, tunaweza sema Marehemu Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu ya dini yake?

Hapana Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu maono yao yalitafautiana sana.
Ni kweli usemalo ila kwa baadhi ya vitu hata ufumbe macho bado unaoziona chembe chembe za udini.
We jiulize sa kimfarijishacho ni kipi hapo
 
Hoja yako ni ipi hapa?
Hoja yangu ni kwamba kuna katiba yenye manufaa kwa watawala, kuna katiba yenye maslahi kwa wanasiasa, na kuna katiba yenye maslahi kwa wananchi na maendeleo ya nchi yao kiuchumi na kisiasa.
 
Mahakama ya Tanzania imetangaza kumuondoa aliyekuwa mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) Prof Mussa Assad na Magufuli kama KINYUME CHA KATIBA *Lakini mahakama inakataa kutangaza uteuzi wa CAG Charles Kichere kama kinyume cha katiba * Mahakama pia inakataa kumrejesha Assad kama CAG mkuu
 
Hii aibu aibebe Job Yustino Ndugai; alikuwa chanzo cha yoote !
 
Ndugu kila kitu sio udini, tukiwa hivyo mbona tujiharibia utu wetu.

Je, tunaweza sema Marehemu Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu ya dini yake?

Hapana Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu maono yao yalitafautiana sana.
Niwatu wajinga sana ndio hununua airliner kwa cash.....
 
Ina maana kwa uamuzi huu Assad atarejeshwa ofisini au ?....

je bunge la spika Ndugai lililokataa kumpa ushirikiano lilivunja katiba ?...

Najiuliza iwapo Magufuli (Rip) angelikuwepo mpaka Sasa, mahakama ingeweza kutoa hukumu ya namna hii ?.....huenda uhuru wa huu muhimili bado sio kamilii..
Pascal Mayalla JokaKuu Nguruvi3 Mag3 zitto junior Tindo
 
Mbona wamesubiri afe ndiyo wakatoa hukumu?
Mahakama imekosea. Sheria inasema hivi:

CAG ATATEULIWA NA RAIS KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ISIPOKUWA ANAWEZA KUONGEZEWA TENA KIPINDI KISICHOZIDI MIAKA MITANO.

Professor Asad aliteuliwa kwa miaka 5, hakuteuliwa tena, hivi ndiyo sheria inavyosema. Si lazima ateuliwe TENA.

Kanuni waliyotumia ni ile ya kusema CAG hawezi kuondolewa madarakani, yaani katika mkataba wake wa miaka 5 (ambao alimaliza) au katika muhula wa pili KISICHOZIDI miaka 5 (ambayo hakupewa). Majaji wamejimisdirect.

Kuna pia IFRS na ISA, sheria na miiko ya Wahasibu (CAG ni Mhasibu, lazima awe CPA chini ya NBAA). Sheria zinasema auditor hawezi kufanya mfululizo kwa miaka 3 unless SHAREHOLDERS wakubali. Kwa hiyo Asad hii ilimbana pia. Huu ni utaratibu katika nchi zote Jumuia ya Madola.

Majaji Watukufu walitakiwa waombe AMICUS CURIA, Mhasibu awape huu ufafanuzi sasa sijui kama aliutwa. Kwa ujumla kesi hii imekaa zaidi kisiasa na kishabiki. Ili kutoweka precedent, AG na NBAA wanatakiwa wakate rufaa.

Asad hakufukuzwa, muda wake uliisha. Ile kulitukana Bunge alilofanya Marekani ni aibu udhaigu binafsi. Kwa kawaida angeshughulikiwa na NBAA Supika angelalamika (lakini ilikuwa ni haki yake Kikatiba kukataa kutukanwa), lakini halihusiani na hii kesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…