Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Mahakama Kuu, Masjala Kuu imebainisha kwamba uamuzi wa kuondolewa katika utumishi wa umma kwa aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ulikiuka Katiba.

Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu, Dk Benhajj Masoud (kiongozi wa jopo), Juliana Masabo na Edwini Kakolaki, kufuatia kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Profesa Assad aliteuliwa kushika wadhifa huo na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Novemba 5, 2014 na alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi Novemba 4, 2019 baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipomteua Charles Kichere kushika wadhifa huo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Serikali mwaka 2019 ilieleza kuwa Profesa Assad kipindi chake kilimalizika Novemba 4, 2019.

Zitto aliamua kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani hapo akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad katika wadhifa huo na uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya, akidai kuwa Profesa Assad alikuwa hajatimiza muda wake wa utumishi kikatiba yaani umri wa kustaafu.
Zitto aliamua kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani hapo akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad katika wadhifa huo na uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya, akidai kuwa Profesa Assad alikuwa hajatimiza muwa wake wa utumishi kikatiba yaani umri wa kustaafu.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 8 ya mwaka 2020, Zitto akiwakilishwa na mawakili Dk Rugemeleza Nshala na Nyaronyo Kichere, alikuwa akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad na kuteuliwa kwa Kichere kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi.

Alidai kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma namba 11 ya mwaka 2008 kinachoweka mihula miwili ya miaka mitano ya utumishi wa CAG, ambacho ndicho kilichotumika kuondolewa kwa Profesa Assad, kinakinzana na masharti ya Katiba.

Zitto alidai kuwa Ibara ya 144(1) ya Katiba ambayo inaeleza kuwa CAG atatumikia wadhifa huo mpaka umri wake wa kustaafu, yaani miaka 60 kikatiba au miaka 65 kisheria, sawa na kifungu 62(a) cha sheria hiyo kinavyoeleza.

Hivyo, alikuwa akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi, ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba na kwamba kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kutimiza umri wa kustaafu ni batili na pia uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya ni batili.

Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyosomwa jana ilikubaliana na hoja za Zitto kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi kuweka mihula ya miaka mitano mitano ya utumishi wa CAG ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba Ibara hiyo ya 44 ambacho kinaendana na Katiba.

Mahakama hiyo imesema kuwa wakati kifungu hicho kinaweka mihula ya utumishi wa CAG, Katiba inazungumzia umri wa kustaafu na si mihula.

Hivyo, Mahakama imesema kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kulikuwa ni batili.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imekataa maombi ya Zitto kutamka kuwa uteuzi wa Kichere ni batili, badala yake imesema kuwa uteuzi wake ni halali kwa kuwa aliteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu hukumu hiyo, Wakili Nshala amesema imeacha utata baada ya kukubali kuwa kuifungu hicho cha sheria kinachoweka mihula badala ya umri ni batili na kwamba Profesa Assad aliondolewa kinyume cha Katiba lakini ikasema kuwa uteuzi wa Kichere ni halali.

Zitto katika taarifa yake kwa umma akizungumzia kipengele hicho amesema kuwa amewaelekeza mawakili wake kukata rufaa Mahakama ya Rufani kwa lengo la kubatilisha uteuzi wa Kichere.

Wakili Nshala alisema kuwa wako tayari kwa maelekezo ya mteja wao, Zitto kukata rufaa Mahakama ya Rufani katika kipengele hicho ili kupata ufafanuzi zaidi.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniface Luhende alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia uamuzi huo, hakuweza kupatikana kwa kuwa simu yake haikuwa hewani.
Legacy inabomolewa huku🤣🤣
 
Kwani hii kesi/shauri lilifunguliwa lini? Kama lilifunguliwa baada kifo cha mwendazake basi huu utakuwa ni unafiki. Kama ilifunguliwa kabla ya kifo, basi nafuta kauli yangu ya unafiki.
 
Hili jamaa huwa jinga sana na sijui wanaomuona huyu mtu sijui msomi aisee km wasomi ndio hawa na kina Lissu kuna wasomi vichekesho sana hiyo nchi
 
Magufuli alikuwa ni KICHAA na maamuzi yake mengi yalikuwa ya HOVYO HOVYO tu. Japo wanaojiita WANYONGE eti wanamkumbuka lakini Mimi nawahurumia kwa kuwa wana akili ndogo ambazo haziwezi kuchambua uwongo wake na ukweli.

Prof Assad alifanya kazi yake vizuri kuonyesha matumizi yasiyoonekana ya Tsh 2.4 Trillion. Hiyo ndiyo sababu za kumuachisha mkataba.

Halafu WAJINGA wanaojiita WANYONGE wanasema Magufuli alikuwa anapiga vita UFISADI. SI kweli kabisa kinyume chake Magufuli alikuwa ni FISADI aliyepita viwango vyote na ambaye alipenda awe aniba peke yake na kikundi chake cha akina Dotto James, Makonda, Bashiru, Chamuriho, Alexander Mnyeti to mention just a few
 
Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha. Bila katiba mpya tena kwa njia ya machafuko, tusitegemee hatua zozote kuchukuliwa kwa hawa walevi wa madaraka.
Cc: UHURU JR
Magufuli aliamua kutoongeza mkataba wa Asaad. Sheria ilimruhusu kufanya hayo.

Leo mahakama inasema ile sheria inapingana na katiba. Sheria yenyewe iliwekwa kabla Magufuli hajawa rais wa JMT.

Sasa hapo Magufuli ana kosa gani?
 
Magufuli aliamua kutoongeza mkataba wa Asaad. Sheria ilimruhusu kufanya hayo. Leo mahakama inasema ile sheria inapingana na katiba. Sheria yenyewe iliwekwa kabla Magufuli hajawa rais wa JMT. Sasa hapo Magufuli ana kosa gani?

Kosa lake ni kutumia sheria iliyovunja katiba.
 
Hili jamaa huwa jinga sana na sijui wanaomuona huyu mtu sijui msomi aisee km wasomi ndio hawa na kina Lissu kuna wasomi vichekesho sana hiyo nchi
Unailaumu mahakama au Zitto. Mahakama imetoa hukumu kwamba Magufuli alitumia sheria batili.
 
Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha. Bila katiba mpya tena kwa njia ya machafuko, tusitegemee hatua zozote kuchukuliwa kwa hawa walevi wa madaraka.
Cc: UHURU JR
Na mikutano ya hadhara kuzuiwa mpaka saa hii katiba inasemaje ??!
 
Umeelewa lakini? Kilichopo ni mgongano kati ya Sheria na Katiba! Katiba inatamka kuwa mkaguzi mkuu atatumikia mpaka afikishe miaka 60 ndipo astaafu lakini sheria ya ukaguzi inatoa mwanya kuwa mkaguzi mkuu atakuwa na vipindi viwili vya utumishi katika kiti chake, yaani miaka 5 ya kwanza then ikimpendeza Rais atamteua tena, kwaiyo Magufuli aliutumia mwanya wa sheria ambayo inafafanunua Katiba, wakati uo Zitto alienda Mahamani kupinga kifungu hicho cha Sheria na kwa mujibu wa Sheria zetu, sheria yoyote inayokinzana na Katiba basi kifungu hicho ni batili.

Sheria za namna hii tunazonyingi sana katika Taifa letu! Ata lile la Ndugai kulazimishwa kujiuzulu ni sawa tu na ili la Assad sapo wanaoamua wanaangalia upepo kuwa sasahivi Magufuli hayupo basi hakuna cha kuhofia, ila now Samia yupo ndiye alitefanya Ndugai atoke basi ili haliwezi kukubaliwa kule!
Unaweza sema bora Magufuli alitumia mwanya wa kisheria kukinzana na Katiba ila Samia hakutumia lolote kwa Ndugai zaidi ya power aliyonayo.
Chifu,

HAIPO HIVYO... Kwanza hakuna cha "Rais ikimpendeza"! Pili, hapo ulipotaja katiba na sheria, ni kwamba ume-interchange,

Katiba inasema CAG atakaa ofisini kwa miaka 5 na ANASTAHILI mkataba wake kuwa renewed, lakini atatakiwa kuachia ofisi akifika miaka 60 AU umri MWINGINE utakaotajwa na sheria.

Sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma ya mwaka 2008 Kifungu cha 6(2) kimetaja umri mwingine ni miaka 65!

Kinachoweza kumfanya awe terminated kabla hajafika hiyo 65 ni endapo atafanya kosa miongoni mwa yale yaliyotajwa kwenye katiba, na hapo hadi aundiwe tume ya kijaji kuchuguza tuhuma dhidi yake!!

In short, CAG HATUMBULIKI... usipomtaka, na kama hana kosa kama yalivyotajwa kwenye katiba basi umlazimishe kujiuzuru!
 
Kwa hizo Akili za kwenda kuambiwa na "I do you"

Au kwa Vision ipi hasa ambayo wapinzani wa nchi hii waliyonayo?

Kwenda kukaa na wazungu halafu wawafundishe jinsi ya kuleta mifarakano kwenye nchi zenu kwa faida zao?

Kazi kubwa ya kituonyesha mfano kwa upinzani wa kitanzania ni kununulika kwa Shekeli tu.

Kuanzia Mr Chairman mpaka kina Zitto!

Kuanzia yule aliyemuuzia chama Lowassa mpaka yule aliyemuuzia Chama Membe!

Hadi hawa Wa- bonge wanaobongewa na kulainika asubuhi.

Kifo cha CCM au Anguko la CCM litatokana na wana CCM wenyewe!

Kesi ni ya Magufuli na Zitto, ila unaiongelea CHADEMA. Tusubiri kesi ya watu wasiojulikana waliomlima risasi Lissu.
 
Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
Bado tuuu shujaa anakumbukwaa
 
Back
Top Bottom