Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Hata kama alivunja katiba kwa ajili ya maendeleo ya watu kuna shida gani? Wakati mwingine kwa kiongozi mwenye maono anatakiwa a - dictate ili mambo yaende.
 
Yule mwendakule kuzimu alijigeuza mwanzo na mwisho wa kila mtanzania...akiamua ufe unakufa, ndio maana tulimsifu tu ili tuendelee kuwa hai.
KAMA HUAMIN MUNGU WA MBINGUNI YUU HAI NA ANAWEZA mkumbuke mungu wa duniani magufuli
Acha kufuru paka wewe...ulikua na connection gani na magufuli hadi akuue ..au kuna ndugu yako gani aliuawa na magufuli.
 
Acha kufuru paka wewe...ulikua na connection gani na magufuli hadi akuue ..au kuna ndugu yako gani aliuawa na magufuli.
Mkuu hao watu wana matatizo kwenye ubongo, unakuta mtu hana mbele wala nyuma huyo Magufuli hakuwa akimjua ila et nae anakwambia alikuwa anaishi kwa hofu ya kuogopa kutekwa na Magufuli.
 
Mkuu hao watu wana matatizo kwenye ubongo, unakuta mtu hana mbele wala nyuma huyo Magufuli hakuwa akimjua ila et nae anakwambia alikuwa anaishi kwa hofu ya kuogopa kutekwa na Magufuli.
Kabisa mkuu...walalamike wafanya biashara waliokua wanakwepa kodi hapo inaleta mantiki kwa mtazamo wao.
 
Majadiliano ya kuirudisha yanaendelea kumbuka zuio lilikuwa Ni amri ya Rais Mwendazake so taratibu za kisheria zinaangaliwa.
Jambo lipo kikatiba hivyo zuio lilikuwa ni batili na huyo aliyezuia hayupo, mangi Samia katengua ambayo aliyaamrisha Magufuli?
Kinachoendelea sasa ni Samia mwenyewe ndio mwenye kuzuia hiyo mikutano na wala sio suala la amri ya marehemu.
 
Majadiliano ya kuirudisha yanaendelea kumbuka zuio lilikuwa Ni amri ya Rais Mwendazake so taratibu za kisheria zinaangaliwa.
Kwani katiba inasemaje kuhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa?majadiliano ya nini wakati katiba inaelekeza kazi za vyama vya siasa,Rais wa Tanzania yuko juu ya katiba ndio Maana hauwezi kumshita hata akivunja hiyo katiba,juzi hata tumesikia mkurugenzi wa TRC alifukuzwa kazi na mamlaka kisa kumsema Samia kuhusu tozo,na katiba inaruhusu mtu kutoa maoni lakini baada ya maoni kafuzwa Kazi mpaka mahakamani kagonga mwamba.
 
Jitu kwa kukosa maarifa linamtetea Magufuli, tuonyeshe basi kivipi hakuvunja katiba- hawezi. Eti oooh mzalendo, wapi pameandikwa ukiwa mzalendo ruksa kuvunja katiba
 
Jitu kwa kukosa maarifa linamtetea Magufuli, tuonyeshe basi kivipi hakuvunja katiba- hawezi. Eti oooh mzalendo, wapi pameandikwa ukiwa mzalendo ruksa kuvunja katiba
Asadi ameudumu vipindi viwili vilimtosha kukaa pale, Magufuli alimkuta na akamwongeza miaka 5,kwanza Asadi nae ni visadi tu ndie aliyeifirisi Nssf pamoja na Dau wakati akiwa mkurugenzi wa bodi,kwa kuanzisha mradi mkubwa isiyokuwa na kichwa wala miguu mladi wapige ela.
 
Ndugu kila kitu sio udini, tukiwa hivyo mbona tujiharibia utu wetu.

Je, tunaweza sema Marehemu Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu ya dini yake?

Hapana Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu maono yao yalitafautiana sana.
Kweli kabisa. Asad alitumiwa na maadui wasiolitakia taifa maendeleo ili kuhakikisha anaichafua serikali kupitia ukaguzi wake na hasa issue kama hela mambo ya siri yeye Asad alitaka eti azikague yaani ni sawa na kuiweka wazi bajeti ya CIA
 
Asadi ameudumu vipindi viwili vilimtosha kukaa pale, Magufuli alimkuta na akamwongeza miaka 5,kwanza Asadi nae ni visadi tu ndie aliyeifirisi Nssf pamoja na Dau wakati akiwa mkurugenzi wa bodi,kwa kuanzisha mradi mkubwa isiyokuwa na kichwa wala miguu mladi wapige ela.
Hayo maelezo peleka kwa Jaji akatengue hukumu. Umepiga porojo kidogo badae ukarukia kwa Dau
 
Sheria imetamka wazi vipindi viwili renewable, unless otherwise iwepo sababu za kutokuendelea.
Kwa hiyo hamba option ya kumwo doa CAG kwa kipindi kimoja
Nadhani unaisikia tu hiyo sheria kutoka kwa mashabiki na wahasimu. Sheria inasema atakuwa madarakani kwa maximum vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Aliyepo akimaliza mitano ya mwanzo atakuwa na haki ya KUFIKIRIWA kupewa kipindi kingine cha miaka 5. Sasa alifikiriwa ikaonekana asipewe. Hiyo sheria unayosema wewe ni ipi?
 
Kosa lake ni kutumia sheria iliyovunja katiba.
Asingetumia hiyo sheria angekuwa amevunja sheria. Kumbuka kuwa hiyo sheria ndiyo inayotumika kuwaajiri maDeputy CAG. kufanya value for money audits na maboresho mengi yaliyomo kwenye audit za sasa za CAG.

Kama hiyo sheria ni batili hata mambo yote hayo ni batili. Waweza kwenda mbali zaidi na kusema kuwa hata appointment yake ilikuwa batili kwa sababu aliingia kazini kufuatana na sheria hiyo hiyo iliyoamuriwa kuwa ni batili
 
Back
Top Bottom