Chadema hoja zao ni tume huru, kuibiwa kura, corona yani upumbavu mtupu. Ukiwaambia wafanye siasa ya kutoa solution kwa matatizo ya wananchi unaambulia matusi. Wenyewe kila siku ni maslahi binafsi ya chama tu halafu wanategemea wachaguliwe. 2020 wamevuna walichopanda wananchi hawakuwa na sababu ya kuwashika na kuwach
Nchi yoote hadi mende na nzi wa chooni ni kijani, CHADEMA bado haiishi midomoni mwenu mna shida gani?
1.Je, chadema ndio Walifunga mipaka mwaka Jana na wakulima wakashindwa kuuza mahindi hadi kilo moja ilifika tsh 100/= na walipolalamika wakaambiwa walishe mifugo?
2. Je, chadema ndio Waliwapiga marufuku wafanyabiashara wa mahindi kwa kuwapa amri ya ghafla ya kusaga na ku-pack wauze unga?
3.Je, chadema ndio walimlazimisha tajiri Summry aliekuwa na zaidi ya magunia elfu hamsini ayauze humu ndani kitu kilichopelekea kupata hasara kubwa maana alilazimika kuuza debe kwa tsh 2000//=?
4. Je, chadema ndio waliovamia soko la korosho kwa mtutu wa bunduki na kutoa ahadi hewa ya ununuzi wa korosho kwa bei ya juu tena kwa kishindo cha awamu ya tano na mwishowe korosho haikununuliwa na kuwaachia wakulima umasikini ambao duniani haujawahi kuwepo, mwisho wakaokota kampuni feki la kununua korosho kutoka Kenya nalo likapotea kusiko julikana.
5.Je, Chadema ndiyo iliharibu soko la mbaazi na mazao jamii ya mikunde mfano eneo niliko kilo ya mbaazi ilifika tsh. 2500/= lakini baadaye ilipelekea bei kushuka na kufikia kilo ya mbaazi tsh 100/= na wateja walikosekana?
6. Zitto kaonesha namna ambavyo serikali ilifeli ktk kutatua changamoto za masoko ambapo hata yale masoko yanayosuasua yakaishia kufa kifo cha mende badala kuishauri kutokana na makosa hayo jitu linakurupuka na kuivamia Chadema, huku ni kutumia kichwa kama kama pamba na fuko la kuhifadhi meno.