Acheni umbeaNafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Aaaamin [emoji120]Alale pema peponi Mzee MEMBE
CCM hatataki kusikiaCCM ukweli upo wazi na haupingiki mmemfanya vibaya kwenye historia ya marehemu Benard Membe kipengele cha siasa ,mmeshindwa kuelezea alihama CCM na kugombea Urais kupitia Act wazalendo, hivyo hivyo pia kwa msemaji wa familia
Zitto kabwe umefanya vizuri kuwakumbusha waweke record vizuri ya historia ya marehemu kupitia siasa , lakini kwangu mimi Zitto kabwe atabaki kuwa mwanasiasa mnafiki.
Aaamin[emoji120]Alale pema peponi Mzee MEMBE
Kila mtu atakufa....hakuna kutangulia wala KUCHELEWA.....He is next....itakuwa hajajiweka pia kwenye list.
Salamu za Zito kabwe zimelenga kumsimanga hayati Magufuli na kuonyesha kwamba,Membe alikuwa bora kuliko Magufuli ikiwemo kuendekeza mtifuano kwenye taifa hili ,inahitaji akili kubwa kulitambua hilo alilifanya Zito kabweRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023
Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili
Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.
Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.
Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.
Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.
Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo walituma mtu kumshambulia kwa tuhuma mbalimbali.
Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.
View attachment 2621369
Zitto KabweAidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.
Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.
“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe
Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.
Uovu umejaa nafsini kwako.....Ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha kamwe.
Tuache wafu wazikane. Mbwa kala mbwa.
nasikia le mutuz is no more
Ikiwa next ni "dingi yake" wewe ni lini ?!!!Namuona Zito hapa na vazi lake jeupe tayari kwenda kuzikwa na Maembe. Kipara nae hatulii kila saa kugeuka nyuma tu kwa kina Lukuvi anafosi tabasamu na kucheka kwingi, hivi hajui kama the next ni dingi yake?
Kupiga nini mkuu wangu?Avae Hata sita, si tunajua pa kupiga
Aaaamin [emoji120]Mungu wa huruma amjalie pumziko jema Bernard Membe.
'Yeye aniaminiye ajapo kufa anaishi milele'.
Mama yetu?Kuna tetesi wasaidizi wake walimtaka asihudhurie kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi na yeye ameng'ang'ania.
Huenda leo akaja na barakoa.
Aaaaaamin [emoji120]Rest in Peace Membe, watanzania tunakulilia, Mungu akulaze mahali pema peponi AMEN
Kabla ya Magufuli Zitto alikuwa milionea kwa kulipwa na serikali ili aisaliti CHADEMA na upinzani. Magufuli aliifuta ile ajira. Je Zitto angempenda Magu aliyekata mrija wake? Na bahati mbaya kule Chadema alishafukuzwa akadhani uenyekiti wa PAC ni wake wa kudumu. Waulize wakuu wa mashirika watakueleza Zitto alikuwa anapewa nini ili awaongee vizuri bungeni. Kuna mmoja alimnyima kabisa Zitto akatumia madaraka ambayo hakuwa nayo akaita polisi wamweke ndani. Sasa wakati wa Magufuli Zitto hata huo uenyekiti wa PAC ukafutika. Zitto akarudi kuwa mbunge wa kawaida halipwi kwa usaliti wala kwenye PAC. Adui namba moja wa Zitto akawa JPM. Ila sasa naona mambo yameanza kumwendea poa. Atasema sana.Mnaofatilia msiba wa Membe nafikiri mnamsikiliza sasa Zitto akimuelezea marehemu Membe.
Zitto badala ya kumuongelea Membe anaushambulia utawala wa Magufuli mpaka kumuita JPM mpuuzi.
Na kwanini wenzake wamepewa dakika mbili ila Zitto kapewa dakika zaidi. Zitto anachafua hali ya hewa...
Wana siasa wana wafuasi. Mimi binafsi sioni logic ya kucheka mtu aliyekufa, maana ntakufa piaKwa hiyo ni kuamua kuununua ugomvi wa hao wanasiasa?. Safari bado ni ndefu kwetu sisi watanzania.