Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

CCM ukweli upo wazi na haupingiki mmemfanya vibaya kwenye historia ya marehemu Benard Membe kipengele cha siasa ,mmeshindwa kuelezea alihama CCM na kugombea Urais kupitia Act wazalendo, hivyo hivyo pia kwa msemaji wa familia

Zitto kabwe umefanya vizuri kuwakumbusha waweke record vizuri ya historia ya marehemu kupitia siasa , lakini kwangu mimi Zitto kabwe atabaki kuwa mwanasiasa mnafiki.
 
Nafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Acheni umbea
 
CCM ukweli upo wazi na haupingiki mmemfanya vibaya kwenye historia ya marehemu Benard Membe kipengele cha siasa ,mmeshindwa kuelezea alihama CCM na kugombea Urais kupitia Act wazalendo, hivyo hivyo pia kwa msemaji wa familia

Zitto kabwe umefanya vizuri kuwakumbusha waweke record vizuri ya historia ya marehemu kupitia siasa , lakini kwangu mimi Zitto kabwe atabaki kuwa mwanasiasa mnafiki.
CCM hatataki kusikia

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023



Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili

Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.

Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.

Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.

Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.

Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo walituma mtu kumshambulia kwa tuhuma mbalimbali.

Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.

View attachment 2621369
Zitto Kabwe
Aidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.

Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.

“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe

Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.
Salamu za Zito kabwe zimelenga kumsimanga hayati Magufuli na kuonyesha kwamba,Membe alikuwa bora kuliko Magufuli ikiwemo kuendekeza mtifuano kwenye taifa hili ,inahitaji akili kubwa kulitambua hilo alilifanya Zito kabwe
 
Namuona Zito hapa na vazi lake jeupe tayari kwenda kuzikwa na Maembe. Kipara nae hatulii kila saa kugeuka nyuma tu kwa kina Lukuvi anafosi tabasamu na kucheka kwingi, hivi hajui kama the next ni dingi yake?
Ikiwa next ni "dingi yake" wewe ni lini ?!!!
 
Kuna shida mbili tu hapo;

Moja, kasema ukweli na kwa kawaida ulweli haupendwi.

Pili, amepitiliza dakika!
 
Mnaofatilia msiba wa Membe nafikiri mnamsikiliza sasa Zitto akimuelezea marehemu Membe.

Zitto badala ya kumuongelea Membe anaushambulia utawala wa Magufuli mpaka kumuita JPM mpuuzi.

Na kwanini wenzake wamepewa dakika mbili ila Zitto kapewa dakika zaidi. Zitto anachafua hali ya hewa...
Kabla ya Magufuli Zitto alikuwa milionea kwa kulipwa na serikali ili aisaliti CHADEMA na upinzani. Magufuli aliifuta ile ajira. Je Zitto angempenda Magu aliyekata mrija wake? Na bahati mbaya kule Chadema alishafukuzwa akadhani uenyekiti wa PAC ni wake wa kudumu. Waulize wakuu wa mashirika watakueleza Zitto alikuwa anapewa nini ili awaongee vizuri bungeni. Kuna mmoja alimnyima kabisa Zitto akatumia madaraka ambayo hakuwa nayo akaita polisi wamweke ndani. Sasa wakati wa Magufuli Zitto hata huo uenyekiti wa PAC ukafutika. Zitto akarudi kuwa mbunge wa kawaida halipwi kwa usaliti wala kwenye PAC. Adui namba moja wa Zitto akawa JPM. Ila sasa naona mambo yameanza kumwendea poa. Atasema sana.
 
Kwa hiyo ni kuamua kuununua ugomvi wa hao wanasiasa?. Safari bado ni ndefu kwetu sisi watanzania.
Wana siasa wana wafuasi. Mimi binafsi sioni logic ya kucheka mtu aliyekufa, maana ntakufa pia
Lakini wanasiasa wajinga, wanathubutu kusema maneno ambayo ni kufuru kabisa, kama wao wataishi milele.
Wanachekwa sababu, yanawafika siku sio nyingi baada ya maneno yao yenye mbwembwe nyingi
 
Back
Top Bottom