Zitto Kabwe: Mwambieni Waziri Mkuu "Watu wake hawawezi kumpenda kama wana hofu ya kupigwa na kutekwa"

Kipindi kile cha mwendazake walikuwa hawamtaji PM ni Magu moja kwa moja nini kimetokea mbona mama hatajwi mzigo anaangushiwa PM!!

Hii laana ya unafiki tulio nayo sijui kama kuna siku itakuja kuisha.

Kuna mda nakaa nawaza hivi ile ndege iliyopata ajali bukoba ingekuwa ni hizi alizonunua Magu ukosoaji ungekuwaje!!
 
Mh Waziri Mkuu Kasim Majaliwa lichukulie uzito hili alisemalo Zitto Zubeir Kabwe huyu kuna watu wako nyuma yake wana ajenda ya siri dhidi yako tunaweza tukasema huyu ndiye Ole Sabaya wa awamu ya sita kuwa makini ni hayo tu.
 
Kwahiyo watu wasiojulikana sahizi ni kosa la waziri mkuu sio rais tena kama mlivyokua mnaaminisha umma 2021 kurudi nyuma? Mna nini na Majaliwa? Anakwamisha mambo yenu yepi? Mnadhani mnammudu?
 
Uongozi wa Hayati utaendelea kuwa mfano mbaya Kwa vizazi vyote hapa Tanzania na dunia
 
Majaliwa anachafuliwa na matendo yake mwenyewe hakuna anayemchafua.
 
Kama hujui si ungekaa kimya tu kuliko kuwa mropokaji kama huyo swahiba wako nepi ah nape.
Mropokaji ni Bashiru anayelalamikia serikali aliyotumikia juzi juzi tu hata miaka mitatu bado ameshafilisika.
 
Kalalamika sana[emoji28][emoji28]
Angekuwa amelalamika usingeonana wanaumana huko. Si umeonana uvccm na kina nape wameanza kujitoa akili.

Usiku huu ninapokuambia wapo msoga state house wanajipanga kuwatumia misukule yao kina steve mengele kumjibu dr bashiru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…