Huko sahihi kabisa. Hebu angalia uchambuzi hapa chini.
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi Mkuu 2020, pamoja na kanuni nyinginezo kwenye kanuni hizo, Kanuni ya 30(1) inatamka kwamba watu wanaoweza kuruhusiwa kuweka pingamizi dhidi ya Mgombea Urais au Ubunge watakuwa:-
1. Mkurugenzi wa Uchaguzi;
2. Msajili wa Vyama vya Siasa ;
3. Msimamizi wa Uchaguzi;
4. Mwanasheria Mkuu wa Serikali; au
5. Wagombea/mgombea (m)wenzake
Aidha, Kanuni 30(5) inamtaka Msimamizi wa Uchaguzi [pengine ndiye aliyeweka pingamizi - Mungu apishe mbali!] kutoa uamuzi wa pingamizi hilo na kisha kumfahamisha mgombea ubunge.
Lakini pia, Kanuni 31(3) inaelekeza mgombea ubunge aliyewekewa pingamizi asiporidhika na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi akate rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (hebu fikiria iwapo pingamizi hilo limewekwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi!) kupitia Msimamizi wa Uchaguzi (pengine ndiye huyo huyo aliyeweka pingamizi na kisha akasikiliza pingamizi lake mwenyewe)!
Kisha, [Kanuni 31(4)] inaelekeza kuwa Msimamizi wa Uchaguzi husika (huyo huyo aliyeweka pingamizi na kisha kulitolea maamuzi) aandae nyaraka zote na ushahidi (wa mgombea ubunge aliyekata rufaa Tume dhidi ya maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi (pengine aliyesilikiza pingamizi aliloliweka mwenyewe dhidi ya mgombea) kisha kuziwasilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (fikiria hali itakuwaje iwapo pingamizi dhidi ya mgombea liliwekwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, halafu apelekewe rufaa dhidi ya pingamizi lake iliyoamuliwa na mwajiriwa wake akimpendelea bosi wake!).
Hii model regulations (kanuni za mfano wa kuigwa) imechukuliwa kwenye kanuni na uzoefu wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (vitongoji, vijiji na mitaa) wa mwaka jana (2019) 'uliofanikiwa' sana! Ni brand new electoral democracy ya Tanzania.
Kwenye uchaguzi huo (2019) kiasi cha wapiga kura 95% hawakuweza kupiga kura kwa kuwa wagombea wa upinzani katika vitongoji, vijiji na mtaa hiyo waliwekewa mapingamizi na wasimamizi wa uchaguzi kisha wagombea wa CCM wakapitishwa na kupewa ushindi a kupita bila kupingwa.
Asilimia 95 ya Wapiga kura wa Tanzania walizuiwa/walinyang'nywa haki yao ya kupiga kura (disenfranchised).
Tunaweza kuanza kujadili uhalali (legitimacy) wa viongozi wa kisiasa wanaochaguliwa kwa mtindo huo.
NEC/RPP kuwekea m(wa)gombea pingamizi inamaanisha partiality of the NEC or the Government vis-a-vis the
2020 elections!