Zitto kaenda Ukraine kwa ufadhili wa taasisi iitwayo Benthrust foundation, inayomilikiwa na Jonathan Oppenheimer. Bodi ya ushauri ya taasisi hii inaundwa na wazito kama Olusegun Obasanjo, Ellen Johnson Sirleaf, Gregg Mills, Ernest Bai Koroma. Kwenye hiyo safari pia Bob Wine alikuwepo. Benthrust inatuhumiwa kuwaweka vibaraka madarakani kwenye nchi nyingi za Afrika kwa maslahi yao binafsi. Huwa ni wataalamu wazuri wa kusuka migogoro ndani ya nchi ambayo wanashindwa kupenya kirahisi. Kimsingi ukiona kiongozi anajihusisha na hawa jamaa ujue ni kibaraka wao na sio mzalendo. Binafsi ninamkubali sana Zitto kwa uwezo wake binafsi ila naweza sema sio mzalendo na hafai kuwa kiongozi wa nchi hii. CCM itazidi kuwa madarakani kwa kuzikataa taasisi za hovyo kama hii Benthrust.