Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,888
MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.

Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:

1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.

2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.

3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.

Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natanguliza Shukran kwenu

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020
 
Na Mimi Kura Kwa Lissu!

1. Uhuru- Saivi tunaishi kwa wasiwasi uki- comment tu hata huko twitter kukosoa unaweza kujikuta una kesi ya money laundering.

2. Haki- Ukiwa mpinzani sahau kupata haki hapa nchini.

3. Maendeleo ya watu- tuna midege na mavitu ya pesa kubwa lakini hali ya maisha ni ngumu sana, ajira usiseme.

Tundu Antipas Lissu umepata kura yangu.

Mungu Akubariki Sana, Mkombozi wetu.
 
Back
Top Bottom