Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Haya ndiyo maneno tunataka kuyasikia, CCM walijua nguvu ya upinzani wakiungana ndiyo maana wakaja na sheria iliyoondoa nafasi ya wao kuungana.

Mkiendelea kuunganisha nguvu kwa namna hii Bara na Visiwani, nafasi ya CCM kushinda uchaguzi Mkuu huu ni finyu kama Ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.

Bravo Zitto Kabwe, huu ni wakati wa Tundu Lissu.
#Niyeye2020✌
Wametunga Sheria nyingi za kijinga ili Wapinzani wasiungane lakini imekufa kwao
 
Mzee wa kazi we utagombea lini kiti cha uraisi?

Naona kama unawatoa wenzako chambo, huku wewe ukiingoja Tanzania yenye waelevu wengi.
 
MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.

Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:

1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.

2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.

3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.

Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natanguliza Shukran kwenu

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020

Hii ni akili kubwa Mungu akujalie iPhone haraka.
 
Duh....tamko hili Lina maana Sana...hasa kufuatia ajali yake mbaya...
 
Back
Top Bottom