Kaijadan
Member
- May 31, 2017
- 41
- 35
Nyie hamjaelewana kdg....nyote mpo upande mmoja na mnaongelea kitu kimoja ila mwenzako alihisi upo tofauti naye.Tuwekee taarifa ya serikali hapa kuhusu makubaliano yaliyofikiwa!

Hakufunga goli lolote lile....ni muda tu ungetuambia ukweli.Goli aliyefunga Pascal Mayalla limerudishwa dk ya 87, naona upande wa pili wanapata Penalt ! kila mtu anaomba kipa wetu aucheze huo mpira usijae nyavuni wakati huo huo mchezaji wetu tegemezi nae anagaagaa kwa maumivu makali huenda akatolewa nafasi yake kuchukuliwa na mwingine!!
Wamefanya siri wapi? Sheria yenyewe inakataa usiri how possible upande mmoja wafanye siri wakati ni makubalano ya pande mbili. Mbona mnachanganyikiwa mapema hivi zikiwa ni mvua tu za rasharasha bado masika yenyewe kuwanyea kisawasawa.
Duh! Hatari sanaMAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO
Jana, Julai 19, 2019 Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick Gold Corporation imetoa Taarifa kwa Umma ya kuinunua Kampuni yake tanzu ya Acacia Mining Plc kwa jumla ya Dola za Marekani Milioni 428. Baada ya malumbano ya takribani miezi 5 Barrick na Acacia wamekubaliana juu ya thamani ya Kampuni ya Acacia kuwa ni Dola za Marekani milioni 951 (wastani wa TZS 2.2 Trilioni).
Itakumbukwa kuwa kabla ya sakata la Makanikia la Mwezi Machi mwaka 2017, Kampuni ya Acacia ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 4,400 (wastani wa TZS 10 Trilioni). Kwa mujibu wa kanuni za Masoko ya Hisa na Mitaji, taarifa za manunuzi ya makampuni huwekwa wazi pamoja na nyaraka nyengine zote husika.
Kwa Watanzania nyaraka muhimu katika mauziano haya ya Acacia, ni ile ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick katika kumaliza mgogoro wa Makanikia na masuala ya Kodi. Nyaraka hiyo (ambayo Serikali imekuwa ikiificha baada ya Majadiliano yaliyofanywa na Prof. Palamagamba Kabudi) sasa imewekwa wazi kama Kiambatanisho namba 4 cha nyaraka za manunuzi ya Acacia.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Serikali ya Tanzania imeingia makubaliano na Barrick Gold Corporation mnamo tarehe 19 Mei, 2019. Makubaliano hayo ni MABAYA, ya HOVYO, yasiyo ya KIZALENDO na yanayoumiza nchi kuliko makubaliano yaliyokuwepo kwa Mujibu wa sheria ya Madini ya mwaka 2010. Kwa ufupi tu ni kuwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi WAMEUZA nchi kwa vipande vya dhahabu. Nitaeleza kama ifuatavyo.
Kiambatanisho namba 4 kimeweka muhtasari wa kinachoitwa ‘Material Terms’ katika Makubaliano ya awali kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick Gold ambayo yamesainiwa (INITIALED) mwezi Mei mwaka huu. Kimsingi Barrick imelazimishwa na kanuni za masoko ya mitaji kuweka wazi makubaliano hayo. Ni masikitiko makubwa kuwa Serikali yetu haijathubutu hata kuliambia Bunge kuwa kuna makubaliano ya namna hiyo wakati wa Bunge la Bajeti, imesaini kwa siri kama ulivyosainiwa mkataba wa Buzwagi.
Ikumbukwe kuwa makubaliano hayo yamesainiwa wakati Bunge likiwa linaendelea na mkutano wake jijini Dodoma. Sisi kama wawakilishi wa Wananchi imebidi kusubiri masoko ya mitaji ya ‘MABEBERU’ wa London yaweke wazi masuala yanayohusu nchi yetu. Hii ni dharau kubwa ambayo Serikali ya Rais Magufuli imefanya kwa Wananchi na kwa Bunge. Sasa tutazame ni nini Serikali yetu imekubaliana na Barrick Gold katika maeneo matano tu.
1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO
Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.
Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.
2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M
Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.
Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.
3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE
Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.
Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.
Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.
4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote
Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).
Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.
5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria
Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.
Serikali mara zote iliambiwa kuwa mabadiliko ya sheria kuhusu ‘arbitration’ hayakuwa halisi na ni ulaghai. Serikali yenyewe imekuwa ya kwanza kuvunja sheria yake yenyewe kwa kuingia makubaliano na Barrick Gold kuwa Mahakama zetu hazitahusika na kutatua mgogoro wowote kati ya Barrick na Tanzania.
Tanzania Imekosa Shilingi Trilioni 2 kwa Sababu ya Viongozi Kukosa Maarifa
Siku za mwanzo kabisa za mgogoro wa Makanikia nilieleza kuwa Serikali ya Rais Magufuli haina Maarifa ya kuwezesha nchi kupata ushindi katika suala hili, watu wengi walinitukana, lakini leo imedhihirika hivyo.
Wakati ule nilitoa mfano kuwa Acacia ilipotaka kununuliwa na Kampuni nyengine ya Canada kwa thamani ya Dola za Marekani 4.4 Bilioni (wastani wa TZS 10 Trilioni), Tanzania ingefaidika sana kwa kupata Kodi ya Ongezeko la Mtaji ya Dola za Marekani 880 Milioni (wastani wa TZS 2 Trilioni), Serikali haikufanya subira na ikazuia Makanikia na mpango ule wa Acacia kununuliwa ukavubjika.
Leo Serikali yetu imekwenda kuingia MAKUBALIANO YA AIBU kabisa ambayo kiuhalisia tunaishia kufuta kesi za Kodi ya Dola za Marekani 190 Bilioni (wastani wa TZS 400 Trilioni) na tunawalipa Barrick fedha badala ya sisi kupata Fedha. Ni jambo la fedheha mno, wanaojigamba kuwa ni wazalendo leo wametuuza.
Ingekuwa nchi nyengine, Makubaliano haya ya KIMANGUNGO kati ya Serikali ya Rais Magufuli na Kampuni ya Barrick, ingetosha kuiondoa Serikali madarakani. Rais John Magufuli na Waziri Palamagamba Kabudi wameuza nchi yetu kwa kipande cha dhahabu. Wamelihujumu Taifa.
Kabwe Z.Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Vuga, Zanzibar
Julai 20, 2019
natahadharisha tu mkuu isije ikawa tunafanya jinaiNaona umeumia mkuu au vp
Wewe ni nani wa kumwita binadam mwenzako shetani.
Akili zenu nyinyi nyumbu, hovyo sana.
MAKUBALIANO YA SERIKALI NA BARRICK GOLD CHANGA LA MACHO

Hahaa!! Labda kama humfahamu huyo jamaa!! Kimsingi, huyo jamaa kwenye uzi wa Pascal Mayalla alikuwa anawa-challenge watu aina yetu ambao tulikuwa tunasema haya maafikiano ni magumashi tu! Na alikuwa anawakejeli watu kama akina Lissu! Sasa kwenye huu uzi wa Zitto, kasoma mambo ambayo kwa akili ya kawaida mtu huwezi kuamini na ndio maana wenzake walikuwa wanadai source material! Mimi nikaweka baadhi ya vifungu ambavyo Zitto amevielezea; na nilivieka kama ambavyo vilivyaondikwa na source material!Nyie hamjaelewana kdg....nyote mpo upande mmoja na mnaongelea kitu kimoja ila mwenzako alihisi upo tofauti naye.
Na ni kutokana na hilo, ndio maana nikamwekea video ya Kabudi siku za nyuma alivyokuwa anadanganya kupitia ufafanuzi kuhusu 50/50 arrangement, ndo nikahoji ikiwa anataka tusibiri ufafanuzi toka kwa watu aina hiyo!Ziko tuhuma nyingi tulizo wahi kuaminishwa dhidi ya serekali hii ambazo mwisho wa siku zinakuwa hazina mashiko. Hii nayo itapita kama zilivyo pita nyingine. Niwaulize enyi watetezi wa mafisadi/vinana mmesha isikia serikali upande wake kutolea hili suala maelezo kabla ya kuhitimisha haya mnayo ya tuhumu.
Picha inayojengwa na majizi yenye hasira kwa kukatiwa njia zao za wizi ni kwamba iko namna kama wao walivyokuwa wanafanya huko nyuma katika ufisadi wao. Subirini kwani serikali itatolea ufafanuzi maana serikali ya JPM haija wahi/haitowezekana kujificha katika kivuli cha usiri wa mikataba. Huko kipindi cha nyuma kilicho kuwa cha mafisadi/vinana ndio mbinu hii ya wizi kwa usiri wa mikataba ilitumika.
Serikali ya awamu ya 5 imejipambanua kuwa yenyewe inasimamia maslahi ya nchi kwa niaba ya Watanzania walioipa ridhaa kuwa ongoza ikipigania manufaa yao kwa mikataba ya win-win conditions na hata huu mwisho wa siku tutaliona hili tutakaposikia maelezo ya serikali.
Hii ni hoja dhaifu kutaka watu wanaoji elewa kama wa hapa Jf wafikirie timu ya majaliano haikujua kwamba makubaliano waliyo ya fikia na kusaini yangeliwekwa wazi katika asoko ya hisa.
Leo mji wa Pemba kule Mozambique umechangamka sana kutokana na uwekezaji wa dola bilioni 20 kwenye LNG project. Mji wa Tete Mozambique umenawiri na ukifika tu unaona uwepo wa ukuaji wa uchumi kutokana na uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe. Leo watanzania wamejaa mji wa Pemba Mozambique kwa sababu kuna fursa. Na Mozambique kwa kurahisisha, wameufanya uwanja wa ndege wa Pemba kuwa international airport ili kokote utakako unamalizia mambo yote Pemba, huna haja ya kwenda Maputo.Sehria alizoleta zimeua sekta ya nishati na madini. Unaleta sheria inayoweka VAT kwenye madini. Ni ujinga. Unaleta sheria inayotaka mahakama za nje zisitumike kusuluhisha migogoro. Mpaka leo LNG Project ya $20bn haina uwelekeo wa kupatikana.
Mpaka Rais Magufuli ikabidi akutane na wafanyabiashara wa madini wamueleze.
Kwa huu mgogoro na Acacia, wameshusha investors confidence kwa kiwango kikubwa na tumeonekana ni wendawazimu tunaoweza kulala na kuamka na kodi ya mabilioni tukiimba nyimbo tunaibiwa.
Maprofessa wa jalalani na kujikomba kumfurahisha Rais hawana msaada kwa Taifa.
Hayo makubaliano yako initialed,by both parties means ni legal bindingSalary slip wewe ni member mkongwe humu mh zito anajua kwanini ipo hivyo. angetueleza na upande Wa pill kwanini ipo hivyo iwe balanced. Inaingia kweli akilini rais aliyekataa kusaini mradi Mkubwa wa bagamoyo leo hii uamini kama rais kasaini mkataba wa kimangungo, kama ni hivyo watanzania kuna kazi kubwa ya kusugua brain zetu, ambazo kwa brashi ya kawaida haitoshi labda brashi waya ndiyo inaweza kufaa
Tafadhali usinikumbushe hili jambo, I wanted to make this Sunday, a beautiful sunday! Yaani ile USD 30 Billion Gas Processing Project pale Lindi ndo basi tena 😳😳!!Leo mji wa Pemba kule Mozambique umechangamka sana kutokana na uwekezaji wa dola bilioni 20 kwenye LNG project. Mji wa Tete Mozambique umenawiri na ukifika tu unaona uwepo wa ukuaji wa uchumi kutokana na uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe. Leo watanzania wamejaa mji wa Pemba Mozambique kwa sababu kuna fursa. Na Mozambique kwa kurahisisha, wameufanya uwanja wa ndege wa Pemba kuwa international airport ili kokote utakako unamalizia mambo yote Pemba, huna haja ya kwenda Maputo.
Hahaha mta mtoa roho Pascal Mayalla mwenzenu alidhani kamaliza, kumbe bado.
Sasa nimegundua tayari....Hahaa!! Labda kama humfahamu huyo jamaa!! Kimsingi, huyo jamaa kwenye uzi wa Pascal Mayalla alikuwa anawa-challenge watu aina yetu ambao tulikuwa tunasema haya maafikiano ni magumashi tu! Na alikuwa anawakejeli watu kama akina Lissu! Sasa kwenye huu uzi wa Zitto, kasoma mambo ambayo kwa akili ya kawaida mtu huwezi kuamini na ndio maana wenzake walikuwa wanadai source material! Mimi nikaweka baadhi ya vifungu ambavyo Zitto amevielezea; na nilivieka kama ambavyo vilivyaondikwa na source material!
Sasa hapo ndugu yetu Harambeeta amejikuta hana pa kupenya, kwa sababu source material tumeweka! Sasa kwavile hana pa kupenya, ndo maana mara kwa mara anasisitiza ufafanuzi kutoka serikalini huku akimaanisha "there must be some explanation" ambayo kimsingi anajaribu kujipa matumaini kwamba, Zitto ameshindwa kuvielewa hivyo vifungu, na serikali ndo watatuelewesha!
Nisikuchoshe, ukitaka kumfahamu Harambeeta japo kwa uchache kuhusiana na huu mjadala, msome hapa:-
Na ni kutokana na hilo, ndio maana nikamwekea video ya Kabudi siku za nyuma alivyokuwa anadanganya kupitia ufafanuzi kuhusu 50/50 arrangement, ndo nikahoji ikiwa anataka tusibiri ufafanuzi toka kwa watu aina hiyo!
Tangu nimwekee hiyo video, sijamuona tena!!
Na kwa faida ya wale ambao hawakupata bahati ya kumsikia Kabudi akidanganya live, Profesa huyu hapa:-
Hahaha Pascal anachombeza tu, hana maslahi yoyote lakini, soma vizuri nyuzi zake utamuelewa.Haaahaaa eti watamtoa roho Paschal, ukiona Paskali alivyovyalia njuga hili jambo utadhani kama nchi tumepiga bao, kumbe tumeingizwa chaka.
Asante sana. Great presentation and interpretation.Kama mnadhani Zitto anadanganya, moja ya vipengele alivyoelezea hapo juu document inasema:-
Maelezo hayo yapo kwenye kipengele cha Dispute Resolution! Mnaona hapo ni namna gani endapo itatokea kushindwa ku-solve any dispute, basi issue itapelekwa mbele in accordance to UNCITRAL Conciliation Rules, na sisi, of course, citizens of arguing parties hawatakuwepo kwenye team!
Sasa kama tunatarajia huko mbele watu wata-resolve issues kwa kuzitangatia maslahi yetu basi tuna safari ndefu!
Kuhusu 16% ya shares zetu kuwa Class B Shares, makubaliano yanasema:-Haki za Class A and Class B Shareholders zimeelezewa kwenye Shareholders Agreement, lakini Zitto aliposema kwamba hizo shares zetu huwezi kuziweka hata kuwa dhamana ni kutokana na kipengele kinachosema:- Suala la kwamba lile sharti la Tanzania kumiliki 30% akina Kabudi na Magu wameliuza kwa Wazungu, makubaliano yanasema:- Kwahiyo hiyo 16% itaendelea kubaki hivyo hivyo! Vipi kuhusu suala la kusafirisha madini nje? Makubaliano haya hapa:-Kumbe wanayo unfettered rights ya kusafisrisha madini na makinikia nje ya nchi hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kufanya refining and smelting ndani ya nchi!
Kama ndivyo, kwanini basi tusiwalazimishe hawa Barrick wajenge mtambo wa kuchenjua makinikia hapa hapa Bongo ili wasiendelee kutupiga changa kwa kusafirisha makinikia nje ya nchi?! Makubaliano yanatoa jibu kwa hilo swali, kwamba:-
Aidha hapa tukumbuke kwamba, JPM alinukuliwa akiongea na Maswahiba zake, including Steven Makigo kwa kusema kwamba, uchenjuaji wa makinikia sio kazi kivile; it's a matter of building a furnace na kuongeza boiling point of so and so, kitu na box! Sasa nadhani ni wakati wa JPM kuitumia kemia yake kuongeza hiyo B.P ya Copper Concentrates ili iyeyuka mapema ili tubaki na dhahabu yetu!
Yaani hapa mtu akihoji PhD ya Mkulu, ndo basi tena yanakukuta ya Ben!!!!!!
Ziko tuhuma nyingi tulizo wahi kuaminishwa dhidi ya serekali hii ambazo mwisho wa siku zinakuwa hazina mashiko. Hii nayo itapita kama zilivyo pita nyingine. Niwaulize enyi watetezi wa mafisadi/vinana mmesha isikia serikali upande wake kutolea hili suala maelezo kabla ya kuhitimisha haya mnayo ya tuhumu.
Picha inayojengwa na majizi yenye hasira kwa kukatiwa njia zao za wizi ni kwamba iko namna kama wao walivyokuwa wanafanya huko nyuma katika ufisadi wao. Subirini kwani serikali itatolea ufafanuzi maana serikali ya JPM haija wahi/haitowezekana kujificha katika kivuli cha usiri wa mikataba. Huko kipindi cha nyuma kilicho kuwa cha mafisadi/vinana ndio mbinu hii ya wizi kwa usiri wa mikataba ilitumika.
Serikali ya awamu ya 5 imejipambanua kuwa yenyewe inasimamia maslahi ya nchi kwa niaba ya Watanzania walioipa ridhaa kuwa ongoza ikipigania manufaa yao kwa mikataba ya win-win conditions na hata huu mwisho wa siku tutaliona hili tutakaposikia maelezo ya serikali.
Hii ni hoja dhaifu kutaka watu wanaoji elewa kama wa hapa Jf wafikirie timu ya majaliano haikujua kwamba makubaliano waliyo ya fikia na kusaini yangeliwekwa wazi katika asoko ya hisa.
Zitto ametafsiri alichokisoma kwa namna livyoona yeye japo sivyo ilivyo katika uhalisia wake. Msioelewa Kiingereza na/au misamiati/lugha ya uwekezaji katika tasnia ya uziduaji mtachotwa sana na hekaya hizi za akina Zitto.