Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Hahaha mwenzenu anatafuta sifa za kuwa rais bora Afrika na Dunia, anapata shida kwanini hasifiwi hivyo anatafuta cha kumtoa, tatizo watanzania siku hizi mnajua hamtoi sifa hovyo hovyo anateseka sana.
Zitto umetoa analysis nzuri. Mimi nimekuelewa. Sidhani wakazi was Lumumba watakuelewa. Watakachoweza kusema ni kuwa unatumika na mabeberu.
 
Naona spinning imeshafanyika tayari juu ya hili kwa kumtoa kafara Mgosi January..

Wale wote wenye nguvu ukiwemo ZZK msikubali kutoka kwenye reli kwenye hili suala la ACACIA.. Hapa linatafutwa kuzikwa kwa kuspin mambo lakini hili ni suala nyeti na very serious na lenye implication kubwa kwa Taifa...
 
North Mara
hapa mgodi kinu kimefungwa
sababu ni
1. Mazingira
kuna bwawa la maji machafu (TSF)
2. Mgogoro wa Barrick na Acacia
Ila pia General Manager
alikimbia more than two months amekatalia South Africa

Kuna mjaruo mmoja ndiye ana-Act
sasa na hizi taarifa za Zito
Duh hapa njia panda!

coz hapa North Mara Nyamongo
ndiyo tunashuhudia huu mziki

Dhahabu hakuna kutoka zaidi ya Wiki sasa!

kwamba huu wote ni mkwara?
Kiini macho?
maigizo?
Mmh nadhani hadi Jumatatu ndiyo itaeleweka rasmi!

wacha tusubirie
Serikali inaweza nayo kuja na hoja

askari ndiyo wanalinda huku
Wanajeshi pia wapo huku

Acacia wenyewe hawaamini huu mziki hapa wamekimbia tangu Asubuhi

Yaani maswali ni mengi kuliko majibu sasa
But
Offices zao ziwe Mwanza na Dsm
Alikimbia au alisafiri? Lini Nyamongo iliacha kulindwa na FFU? North Mara inamilikiwa na Barric au Acacia?
Mikataba mibovu + matokeo mabovu = maamuzi mabovu
Chini ya CCM tutegemee kina chifu Mangungo wengi...
Maendeleo hayana vyama...
 
Goli aliyefunga Pascal Mayalla limerudishwa dk ya 87, naona upande wa pili wanapata Penalt ! kila mtu anaomba kipa wetu aucheze huo mpira usijae nyavuni wakati huo huo mchezaji wetu tegemezi nae anagaagaa kwa maumivu makali huenda akatolewa nafasi yake kuchukuliwa na mwingine!!
Hapa siyo kwamba Barrick wamerudisha goli bali wamerudisha na kupata magoli mengine mawili.

Niliwahi kusema, Barrick haijawahi kushindwa kulinda maslahi yake mahali popote Duniani na miaka yote. That is what it means to be SMART. Siyo kelele za akina Kabudi. People are silent, they act silently but smartly and perfectly. Siyo hawa wa kwetu ambao kila siku ni kelele kwenye TV.

Smart people spend much of their time thinking but foolish people much of their time they spend talking.
 
Kulinda aibu yao ndio wametuingiza chaka zaidi,kama yalioandikwa hapa yana ukweli hata kwa 25% tu basi tumeumia viaya mno!!!!
Nilikuwa najiuliza,kwanini hawa barrick wanapigana sana vita na Acasia juu ya hisa za Acasia,kumbe washaona chaka la kutupiga hela!!!!
Nchi imelaaniwa hii!
Mzungu uwaga si mpumbavu!ukiona amekubali kuingia kwenye deal na wewe ujue kuna sehemu lazima akupige!Barick alikuwa anapambana na mwenzake abaki yeye atupige
 
Inasikitisha,cha msingi yawekwe hadharani hayo makubaliano tujiridhishe!Ila sidhani Zitto kaandika hili bila kuwa na taarifa za uhakika!
Nilikuwa nashangaa kwanini Barrick walikuwa wamekomaa kumuondoa Acadia njiani,kumbe wameona ndio mwanya wa kutuliza!!!?Daaah,tumepigwa kisawa sawa,hii yote mtu mmoja apate sifa kuwa amefanikiwa kuwaondoa Acasia waliokuwa wanamkwamisha,karuka mkojo kakanyaga mavi,shame!
Paschal mayalla atawaambia nini watu😂😂
 
Tatizo Lugha iliyotumika hawakuwa wanaielewa
 
Natamani habari hii ingetokea kwenye magazeti ya Musiba labda tungejua kama ana nia thabiti ya kuijenga hii nchi.
Binafsi, naona kale ka msemo ka Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu kanafaa kabisa kuelezea kwa nini haya yote hutokea. Na kangetungiwa mdahalo mzito "Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu. Discuss. Labda ingesaidia viongozi wetu kujitathimini wanakwama wapi.
Kwa mfano, kiongozi anapoendekeza ubabe na kejeli kwa wale wanaopingana na. Mawazo yake kwa kivuli cha uzalendo. Huo ndio uwendawazimu wenyewe.
 
Tafuta ile clip inayoitwa fake ya mazunguzo part 3. Yuko fake mmoja chambo wa familia aliahidiwa tunu kutokana na pendekezo la mama mtu. Kwa kawaida wa africa tuko na extended family ndio nikauliza jina atapewa nani?
Hahah

Ngoja nisikilize tena nitakuja tena mkuu
 
Natafuta comment ya mtu mwenye kupinga kwa hoja nipate mizani humu na sio mwenye kutukana ngoja niendelee kutafuta wanalumumba mnatuangusha wananchi au ndo wanasubiri wakina msukuma na polepole waje kwanza ndo waelewe zitto kasema nn nao wajibu nn chemshe vichwa jmn msisubiri data kwa polepole
 
Mpinzani wa kupinga. Yeye (Zito) awamu ya nne ndiye alikuwa mstari wa mbele kusema kuwa kinana ni mwizi mkuu wa rasilimali za taifa. Kuwa ni jangiri maarufu wa meno ya tembo. Ajabu hivi sasa yeye ndiye mtetezi mkubwa wa Kinana. Hivi huyu binadamu ni binadamu wa aina gani?

Mkuu kumbe ujumbe huu wote wa zitto hapa ni wa kumtetea kinana au kuna uzi mwingine mkuu nielimishe unanichanganya samahani lkn nataka kujua tu nitoe ujinga usiniache na upumbavu
 
Zitto ameshirikiana na mabeberu kuweka classified infoz hadgarani,anatumika na mabeberu wasioitakia mema nchi hii!!!!
Haiwezekani atoe siri za nchi,makubaliano yalikuwa ya siri!

Natamani dunia ipasuke niingie,nchi hii imelaaniwa!

Mkuu ebu soma vizur comment yako na uzi wa zitto alafu tafuta msaada pembeni yako uone nani mwenye matatizo na kulaaniwa nchi haina laana bana ila baadhi ya watu wake tena wale walio mstari wa mbele
 
Nyie kaeni mkidhania ikifika 2020 mtawashawishi wapiga kura wa kule kijijini kwetu kwa kutumia hoja ya kisomi. Shauri lako.

Kweli mambo ya mahaba niue, kwahiyo unachojivunia ni kwakuwa hao wanakijiji hawaelewi hoja za kisomo!? Kama hao wanakijiji wanaelewa hoja zisizo za kisomi ni kipi kinafanya vyombo vya dola vitumike kulazimisha ushindi, badala ya hizo hoja zisizo za kisomi zinazoeleweka kujibeba? Ni kipi kinachangia wapinzani wasiongee na wananchi kama hawaelewi hoja za kisomi? Bado unaamini ile propaganda mfu kwamba kura ziko vijijini, kama ni hivyo, huu ukatili wa wazi kwenye box la kura huku mjini ni wa nini, wakati kura ziko huko vijijini? Ni hivi, mzee umeishiwa kwa ajili ya kuendekeza siasa za kipuuzi kwa upofu wa ukanda.
 
Mm nilishakuelewa na ndiyo maana mapambio yako yote huwa unampigia jiwe tu na siyo wateule wake. Hapa naona kabisaa kuna kitu umekiona,na kwamba bado akili yako ipo upinzani lkn hoja km hizi hazina ile nguvu ya ushawishi kwa wapiga kura km kule kwetu maririta. Nafikiri unamuunga mkono jiwe kwa sababu anajua kuwapanga wapiga kura wetu.

Inaweza kufika mwezi wa 5 jiwe akampiga chini palamagamba kwa mbwembwe zote kutokana na hili la Barrick..na kura zote akazibeba. Ila tuacheni utani jamani,jiwe ni kiboko aisee!

Jamaa ni mpiga porojo sijawahi kuona hii nchi. Kipindi kile amepewa wizara ya uvuvi,samaki ,Dagaa mpaka mayai ya vyura alikuwa anajua idadi yake!

Wakati ule alikuwa anawadanganya watu kirahisi maana hakuwa na madaraka ya kutoa maamuzi ya mwisho. Aliposhika madaraka ndio muamuzi wa mwisho, maamuzi yake yanatumia nguvu kubwa ili yakubalike, hapo ndio watu wamegundua kwamba ni bingwa wa kupika data ili kuhadaa umma.
 
Yaani nahitaji kujua walau kidogo tu ukweli wa uchambuzi huu wa ZZK, nimeshtuka, moyo umeniuma sana..! 😳 Kama ni kweli Kabudi ndio ana kiwango kidogo hivi na kulifanyia Taifa letu hivi kweli? Kweli? 😪 Bado siamini kwa sasa, nikijua ZZK ni mpinzani na hawezi support serikali ya JPM, hilo tu ndio linanipa moyo kwa sasa nisiamini.

Mzee mwanakijiji anasema nyie watu wa vijijini hamuelewi hoja za kisomo, bali yale mnayolishwa na jiwe na genge lake ili mtoe kura. Ili roho isikuume, ww baki na ujinga wako subiri upewe data za kupikwa na serikali. Hapo roho haitakaa ikuume.
 
North Mara
hapa mgodi kinu kimefungwa
sababu ni
1. Mazingira
kuna bwawa la maji machafu (TSF)
2. Mgogoro wa Barrick na Acacia
Ila pia General Manager
alikimbia more than two months amekatalia South Africa

Kuna mjaruo mmoja ndiye ana-Act
sasa na hizi taarifa za Zito
Duh hapa njia panda!

coz hapa North Mara Nyamongo
ndiyo tunashuhudia huu mziki

Dhahabu hakuna kutoka zaidi ya Wiki sasa!

kwamba huu wote ni mkwara?
Kiini macho?
maigizo?
Mmh nadhani hadi Jumatatu ndiyo itaeleweka rasmi!

wacha tusubirie
Serikali inaweza nayo kuja na hoja

askari ndiyo wanalinda huku
Wanajeshi pia wapo huku

Acacia wenyewe hawaamini huu mziki hapa wamekimbia tangu Asubuhi

Yaani maswali ni mengi kuliko majibu sasa
But
Offices zao ziwe Mwanza na Dsm

Mbona mimi sio mzito, lakini hapa nimetoka bila kitu.
Unamaanisha uwepo wa TSF umesababisha Mill kuzimwa? Inamaana miaka yote hapakua na TSF.
Nini kimesababisha dhahabu kukosekana kwa zaidi ya wiki? Maana kama ni kuongozwa na GM mbongo akina Rweyemamu walishaongoza miaka ile na migodi ilikua inatema
 
Mkuu njoo na hoja ya kumjibu kutokana na mada yake hapo juu ueleze jibu ya kila point yake hapo na ufafanuzi na faida tutakayo ipata kuendelea kumpa majibu kama haya ulio yaleta ni kuendelea kumpa kichwa ndugu huyu tusikwame kiasi hiki kwa kuja na vioja mimi ni mwana CCM ila ningefurahi kwa mwana chama mwenzangu mwenye uelewa na hivi vitu waje kumjibu vizuri kupangua hoja moja mpaka nyingine ili kumfedhehesha huyu kiumbe mnafiki zitto

Tuwe wakweli, maendeleo hayana chama/vyama
 
Back
Top Bottom