Zitto: Makubaliano ya Serikali na Barrick Gold changa la macho

Hakufunga goli lolote lile....ni muda tu ungetuambia ukweli.
 
Wamefanya siri wapi? Sheria yenyewe inakataa usiri how possible upande mmoja wafanye siri wakati ni makubalano ya pande mbili. Mbona mnachanganyikiwa mapema hivi zikiwa ni mvua tu za rasharasha bado masika yenyewe kuwanyea kisawasawa.

Kwa hiyo kuna uwezekano kuwa serikali itatuonyesha mkataba wenye vipengere tofauti na vile vilivyopo kwenye huo uliotolewa na Barrick? Hapa ni sawa na kuamini kuwa unasubiri taarifa kutoka timu zote mbili ili ujue matokeo ya mechi yalikuwaje.
Ccm mna mambo haki ya nani!🤣🤣🤣🤣
 
Duh! Hatari sana
 
Wewe ni nani wa kumwita binadam mwenzako shetani.
Akili zenu nyinyi nyumbu, hovyo sana.

Mimi ni mimi!

I can call anybody anything!

Be a hero jump over the ocean kama ume-mind!

Bure sana!

Awamu hii ya majinga jinga,maarifaless!

Your stupidity so sophisticated!
 


Duh!! Nimesoma Tangazo la Barrick, hususani Kielelezo Na. 4, sehemu A (kifungu cha 10 hadi 16), B (kifungu 1 hadi 3), C (kifungu 1 hadi 8), D na F. Maeneo hayo yote ni misumari ya moto!

Anyways, hicho kielelezo 4 wahusika wamesema sio final agreement, huenda kunaweza kuwa na makubaliano mengine yenye afya zaidi kwetu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Nyie hamjaelewana kdg....nyote mpo upande mmoja na mnaongelea kitu kimoja ila mwenzako alihisi upo tofauti naye.
Hahaa!! Labda kama humfahamu huyo jamaa!! Kimsingi, huyo jamaa kwenye uzi wa Pascal Mayalla alikuwa anawa-challenge watu aina yetu ambao tulikuwa tunasema haya maafikiano ni magumashi tu! Na alikuwa anawakejeli watu kama akina Lissu! Sasa kwenye huu uzi wa Zitto, kasoma mambo ambayo kwa akili ya kawaida mtu huwezi kuamini na ndio maana wenzake walikuwa wanadai source material! Mimi nikaweka baadhi ya vifungu ambavyo Zitto amevielezea; na nilivieka kama ambavyo vilivyaondikwa na source material!

Sasa hapo ndugu yetu Harambeeta amejikuta hana pa kupenya, kwa sababu source material tumeweka! Sasa kwavile hana pa kupenya, ndo maana mara kwa mara anasisitiza ufafanuzi kutoka serikalini huku akimaanisha "there must be some explanation" ambayo kimsingi anajaribu kujipa matumaini kwamba, Zitto ameshindwa kuvielewa hivyo vifungu, na serikali ndo watatuelewesha!

Nisikuchoshe, ukitaka kumfahamu Harambeeta japo kwa uchache kuhusiana na huu mjadala, msome hapa:-
Na ni kutokana na hilo, ndio maana nikamwekea video ya Kabudi siku za nyuma alivyokuwa anadanganya kupitia ufafanuzi kuhusu 50/50 arrangement, ndo nikahoji ikiwa anataka tusibiri ufafanuzi toka kwa watu aina hiyo!

Tangu nimwekee hiyo video, sijamuona tena!!

Na kwa faida ya wale ambao hawakupata bahati ya kumsikia Kabudi akidanganya live, Profesa huyu hapa:-

 
Leo mji wa Pemba kule Mozambique umechangamka sana kutokana na uwekezaji wa dola bilioni 20 kwenye LNG project. Mji wa Tete Mozambique umenawiri na ukifika tu unaona uwepo wa ukuaji wa uchumi kutokana na uchimbaji mkubwa wa makaa ya mawe. Leo watanzania wamejaa mji wa Pemba Mozambique kwa sababu kuna fursa. Na Mozambique kwa kurahisisha, wameufanya uwanja wa ndege wa Pemba kuwa international airport ili kokote utakako unamalizia mambo yote Pemba, huna haja ya kwenda Maputo.

Wakati tafiti za gas na madini Tanzania zimesimama, Mozambique makampuni uameweza kugundua gas nyingi kuliko iliyogundulika Tanzania.

Tunahangaika kuwabembeleza warudi lakini wanasema hata wakiamua kurudi, uwekezaji katika LNG hautaanza ndani ya miaka 5 kuanzia sasa.

Tulijifanya vichaa lakini wenye akili wanatudhihirishia kuwa kichaa hawezi kumshinda mwenye akili. Hakuna tulicho nacho ambacho kisipopatikana Tanzania, Dunia itasimama. Sasa nchi imesimama au kurudi nyuma wakati Dunia inaendelea kusonga mbele.

Watanzania msife na tai shingoni, tazameni fursa kwa mataifa jirani. Nchi kama Burundi, Rwanda, Zambia na Mozambique wana sera nzuri sana za uwekezaji na ufanyaji biashara kuliko kwetu. Kwa wenye uwezo nendeni Ghana, huko naweza kusema ni the best. Ghana inaongozwa na wanaoujua uchumi hasa, ndiyo maana kuna wakati uchumi wao ulifikia ukuaji wa 17%.
 
Hayo makubaliano yako initialed,by both parties means ni legal binding
 
pascal mayalla nilitegemea ungekuwa wa kwanza kuchangia uzi huu lakini sikuoni, i asked you why unatetea uongo na kwa maslahi ya nani kila kukicha kutuletea porojo za makinikia ukashindwa kunijibu.
 
Tafadhali usinikumbushe hili jambo, I wanted to make this Sunday, a beautiful sunday! Yaani ile USD 30 Billion Gas Processing Project pale Lindi ndo basi tena 😳😳!!
 
Kwenye ansadi za wananchi kumbukumbu hii itatunzwa ila kwa ansadi za serikali kitu kama hiki ni uchonganishi wa serikali dhidi ya wananchi.

But, Nasema but kila zama na wakati wake wa kula, huko nyuma kipindi cha Mkapa, Mwinyi, JK kila mtu alitengeneza njia yake ya kukusanya gharani
(private menu) hii ndiyo tunaipigia kelele utadhani ni mpya.

Tusiandike sana maana nafsi zinaumia tu, hata twiga kupanda ndege, machimbo ya chuchuma, dowans, nk..
 
Sasa nimegundua tayari....
 
Haaahaaa eti watamtoa roho Paschal, ukiona Paskali alivyovyalia njuga hili jambo utadhani kama nchi tumepiga bao, kumbe tumeingizwa chaka.
Hahaha Pascal anachombeza tu, hana maslahi yoyote lakini, soma vizuri nyuzi zake utamuelewa.
 
Asante sana. Great presentation and interpretation.
 

Watu wanaongea mambo mazito ya msingi ww unakuja na propaganda mfu. Tusubiri kutoka upande wa serikali wakati tunajua fika serikali inapika data na kuongopea umma kuhusu ukweli? Kila siku Paskali yuko na post za hilo suala la Barrick na Acacia, lakini taarifa nyingi hapati kutoka serikalini bali kwenye hizo kampuni. Tena taarifa anazoziona huko nje ni zile zilizifichwa na serikali yetu hapa nyumbani.

Serikali kusema inajipambanua kupigania maslahi ya umma ni kwa mdomo, je uwezo wa kupambania hayo inao? Unajinasibu kupambania maslahi ya umma kisha unaficha taarifa za hicho unachokipambania, mpaka watu wakaonee taarifa kwa huyo unayeingia naye mkataba!? Ww kaendae tu vikundi vya ukatili kwenye uchaguzi ili kuilinda ccm, mada hii acha wajadili wenye akili.
 
haya tuambie wewe sasa mzungu
Zitto ametafsiri alichokisoma kwa namna livyoona yeye japo sivyo ilivyo katika uhalisia wake. Msioelewa Kiingereza na/au misamiati/lugha ya uwekezaji katika tasnia ya uziduaji mtachotwa sana na hekaya hizi za akina Zitto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…