Uchaguzi 2020 Zitto: Membe hajaacha kufanya kampeni, yuko bize kuandaa Baraza la Mawaziri

Jiwe anaenda kuandika historia ya kuwa Rais wa awamu moja

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Weka hapa link ya hiyo tathmini.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Kura kwa Mh Lissu, achana na Jiwe ambaye kila kitu chake kina utata kuanzia elimu, kabila mpaka manunuzi ya ndege

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
ACT tulifikiri ndio wangeweza kupata wabunge wengi lakini imekuwa kinyume sana kwenye kampeni. Chadema bado itaongoza huku bara, Zitto sijui kafeli wapi!
 
Nadhani Zitto yuko frustrated sana jinsi ambavyo Membe amemwangusha. Maalimu Seif ameanza kampeni baada ya huku bara kuanza na yuko active kuliko Membe.

Pia kwanini Zitto mara zote toka 2015 haoni sababu ya yeye kugombea na kuweka wengine(wasio na ushawishi kumzidi) kigombea inaonyesha chama chake bado focus yake ni ndogo.

Nilitegemea aogombee Urais mwaka huu, kwa nguvu ya ushawishi aliojijenga nao ingekuwa faida sana kwa upinzani. Imagine duo ya Zitto na Lissu jukwaani.
 
Kwa mujibu wa sheria, katika hatua tulipo ya uchaguzi, vyama au wagombea hawaruhusiwi kuungana,na ikiwa watafanya hivyo rungu la NEC na lile la msajili wa vyama vya siasa litawashukia na litawaondoa katika kinyang'anyiro.

Hivyo option iliyopo ni Membe kutokupiga kampeni ili hasije akagawana kura na Mh Lissu. Hongera Membe hivi ni viwango vikubwa vya uzalendo.
 
Zitto amemjibu kuwa baada ya chama chao kuona wanaelekea kushinda wameamua kuweka nguvu nyingi kumsaidia Membe kuandaa baraza lake la mawaziri na hivyo kuwa katika nafasi nzuri kutimiza waliyoahidi siku 100 za kwanza
Dah!
 
kwa hiyo unaamini kabisa membe hatopata kura kutoka kwa wafuasi wa zambarau?
 
Zitto hawezi fanya ujinga wafanyao Chadema saccos. Kuzunguka nchi nzima, huku wakijua kuwa hawawezi shinda.
 
Wa Tanzania tunaonekana wajinga Sana kwakweli, kalamba Ruzuku yote yeye na Zito, then kaamua kukaa kimya na hakuna wa kumuuliza, vya vingi huingia kwenye uchaguzi ili tu kupata Ruzuku, mwingine Chauma yeye kila siku ni hadithi za ubwabwa tu akitumia Kodi zetu na Ruzuku kalamba, ifike mahali hivi vyama vya kipuuzi vifutiliwe mbali, wanachezea jasho letu hawa.
 
[emoji848]kumbe..!!
 
Zitto> wana Kigoma Lissu anawahutubia leo msikilizeni hoja zake ( HAPA PANA AKILI KUBWA INATUMIKA )
 
Mkuu unamaanisha kama Zitto angekuwa mgombea wa ACT na Lissu mgombea wa CHADEMA kwamba upinzani ungepata faida sana?
 
zitto>wana kigoma lissu anawahutubia leo msikilizeni hoja zake ( HAPA PANA AKILI KUBWA INATUMIKA )
Akili ni ipi ndugu, huo ni ujinga wa Hali yajuu Sana na sichelei kusema hata anaesema niakilikubwa naye nimjinga kabisa, akili wakati watu Ruzuku za kampeni zipo mifukoni mwao na kampeni hawafanyi bado unasema akili kubwa, kumbuka hizo Ruzuku ni pesa zangu mimi, wewe na Watanzania wote tuliyeumia kulipa Kodi miaka yote. Leo wanaume wamezifinya mfukoni na kukaa kimya na safari za nje wakijidai wagonjwa, ifike mahali upuuzi huu tunao fanyiwa na wanasiasa ukome jamani, tuwe na uchungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…