Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Status
Not open for further replies.
Tatizo m'metangaza nyie !
Msemaji wa Serikali anapaswa aseme jambo kuhusu hili.

Mbona JK aliumwa ngiri (Waliita tezi dume), akatangaza!

Kama kuna ukweli basi tumuombee.

Tunafahamu kuwa kuna mengi ya haki na yasiyo ya haki aliyoyafanya yaliwaumiza wananchi.Wala tusiombeane mabaya..tuombe yote mawili uzima wa afya na kubadilika kwa kiongozi wetu.

Hakika Mwenyezi ndie mwenyezi kujua
 
Huyu kigogo ni mpumbafuu kumbe et sasa hv huko twitter anacheka cheka tu yaan anajibu ujinga mara et atakufa tu mara recorded anaonyesha alipanga kuzusha uongo kabisa ila ndo mwsho wake huu haaminiki tena

Hahaha Kigogo +Zitto=Zitto Kabwe
 
Mh Zitto umenifikirisha sana, Kuna watu wanaoweza chesa siasa rahisi na za kijinga Kama hizi si wewe, wewe ni mtu unayeheahimiwa na wengi sana na hasa sisi vijana na wapenda siasa.

Mh. Zitto hii no Mara ya pili, Mara ya kwanza ulisema Mh. Rais kutoa mbegu ya korosho tani 25 kwa nchi ya Malawi ni uhujumu uchumi kwakua demand itakua pungua kwakua uzalishaji utaongezeka.

Kwa msomi Kama wewe nilidhani ungeyawaza haya.

1. Kumnunulia mtoto wa jirani daftari za shule na kalamu haimaanishi kwamba itasababisha mwanao akose ajira. Aidha

2. Katika dunia, watu walio kwenye kanda zinazokaribiana hutengeneza mashirikiano, kwakua kidole kimoja hakivunji chawa.

3. Sijawahi sikia popote mtu akafilisika kwa kutoa msaada. Hili limeniogofya sana na kujiuliza namna ambavyo unaamiliana na watu waliokuzunguka.

Mkuu cheza siasa zilizo kwenye levo yako hizi waachie kina Mbowe na Lema nk. Sio wewe Mkuu.
 
VVU a.k.a Vyama Vya Upinzani sasa vimefirisika kabisa.
Hata kiongozi kubwa kabisa wa chama anacheza MDUNDIKO(anaogelea bwawa moja na wazushi mitandaoni)
Kwa hakika sikutarajia kabisa.
Mh. Ziro Zushi Kafiri unatakiwa kuomba radhi bila kukosa.
 
Kwa kifupi, huyu mh. aliyetoa habari za uzushi mitandaoni, mimi nadhani hafai hata kuwa balozi wa nyumba 10. Anaonekana bado ana UTOTO -UTOTO sana.
Maana akiwa balozi, ikatokea siku moja wamepishana kidogo na mwananchi wake, utashangaa kesho asubuhi anagonga ngoma ya kusingizia yule mwananchi wake kafariki, kumbe ni uzushi.
 
Jomba wewe ndio unagundua leo umechelewa...yeye mwenyewe Zitto alishasemaga msimwamini mwanasiasa yoyote wa upinzani..umeshasahau...
Kiukweli mimi baada ya Tundu Lissu mtu mwingine niliyekuwa namuona angalau ana ujasiri wa kuichachafya hii serikali kwa kutujuza mambo ambayo serikali inajitahidi kuyaficha tusiyajue ni Zitto.

Lakini kwa hichi alichokifanya leo, siwezi tena kumuamini wala kumchukulia serious.

Analalamika kwamba Magufuli na serikali yake ameirudisha nchi nyuma kisiasa kwa chuki zake kwa wapinzani, wakati hata yeye ana siasa za chuki tena za kitoto sana.

Nadhani leo ni watu wengi sana tumemshusha vyeo.
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019

Umefuatilia mjadala au ulianzisha? Sio wewe Zitto ulipost picha ya mama Samia akikagua gwaride la heshima ukaweza maneno ya kuonesha anakarabia kukalia kiti cha urais? Inakuwaje Kiongozi mzima wa Chama cha siasa anakujiingiza kwenye cheap politics kiwango hiki?
 
Ndiyo Maana huwa nakwambia kwamba wapinzani Wana Safari ndefu Sana.
Hawana Sera imara, kazi Yao kusubiri matukio ili washabikie,wapinge na kukosoa.
Inasikitisha Sana kuona watu wanashabikia vifo.
Kwa siasa hizi bado sijaona mbadala wa CCM na ndiyo Maana niliamua kutokuwa mfuasi wa chama chochote Maana wapinzani wengi Ni wanafiki tu.
 
Msemaji wa Serikali anapaswa aseme jambo kuhusu hili.

Mbona JK aliumwa ngiri (Waliita tezi dume), akatangaza!

Kama kuna ukweli basi tumuombee.

Tunafahamu kuwa kuna mengi ya haki na yasiyo ya haki aliyoyafanya yaliwaumiza wananchi.Wala tusiombeane mabaya..tuombe yote mawili uzima wa afya na kubadilika kwa kiongozi wetu.

Hakika Mwenyezi ndie mwenyezi kujua
Hivi serekali iwe inajibu kila uvumi wa kinafiki imekua ni taarabu sasa majibu ni hayo amewajibu jpm
 
Nimesikitishwa sanaa sana hiki kitendo kufanywa na mtu kama Zitto.

Hivi mtu ambaye ana huge popularity,kiongozi mkubwa wa chama na ni inspirational kwa wanasiasa wengi wanaochipukia inakuwaje anaonesha chuki za wazi wazi kiasi hiki mpaka kuombeana vifo? Hii picha inaashiria hali ya furaha kwamba.. Halafu eti na yeye ana ndoto siku moja aje awe raisi?

Hakika ningekuwa nna kadi ya hicho chama chake ningeirudisha leo hii hii.
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Ovyoo sana wewe mtu.
 
TL na wengineo walipopatwa madhila wale maccm walioshangilia walipata nini?
Iko aina mbovu na mbaya ya siasa inajengwa katika nchi hii tumeikemea muda mrefu haya ni matokeo ya awali...
Ila kuna watu wanafiki sana na zito ni mmoja wao... hivi JPM akipatwa na mabaya wewe utafaidikaje?
 
Huyo jamaa ana roho mbaya sidhani km ni Mtanzania huyu
Umefuatilia mjadala au ulianzisha? Sio wewe Zitto ulipost picha ya mama Samia akikagua gwaride la heshima ukaweza maneno ya kuonesha anakarabia kukalia kiti cha urais? Inakuwaje Kiongozi mzima wa Chama cha siasa anakujiingiza kwenye cheap politics kiwango hiki?
 
Ndugu zitto unajulikana wewe ndiye kigogo 2014 , nakuhurumia sana future yako na kizazi chako Kwa ulichokifanya toka juzi

Pole sana
Hivi hili mnaliona kubwa sana eeh! Kaeni chini mjiulize tukio hili la uvumi wa kifo na jaribio la kuua pale Dodoma lipi hasa limemchukiza Mungu katika matendo haya ya kibinadamu?
Mkipata jibu basi yote tumwachie Mungu atuazibu kwa kadri ya ukubwa wa makosa yetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom