Zitto: Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema...

Status
Not open for further replies.
Leta screenshots za yeye kueneza

IMG_0178.JPG
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Kaka ZITTO umefuatilia au Umeshiriki? Moja ya post yako ilikuwa na ujumbe sawa sawa na ule wa KIGOGO. Nilichogundua ulilishwa Tango Pori ukaamini, na gesture yako ulikuwa unafurahia Sana. Ila baada ya kujua ilikuwa tango pori, ukarudi kwa aibu kuandika tofauti kufuta aibu. Ni bora tukafanya siasa lakini tukatanguliza UTU, UNDUGU na Utanzania wetu.
Mwigulu
 
Yalizungumzwa mengi mzee alipopata hiyo dharura. Yalizungumzwa mema na mabaya. Waliozungumza mabaya ni wengi mno na sababu ziko wazi. Katika waliozungumza ametoa kauli ya kuomba radhi na hiyo ndo hekima. Si wote watakaoomba radhi na sababu bado ni zile zile.
ulicho kiposti kile ndo umegundua sasa kuwa umebugi na kujishusha hadhi...kwa kiongozi kama wewe, bora useme wali hack acc yako.
 
Kiukweli mimi baada ya Tundu Lissu mtu mwingine niliyekuwa namuona angalau ana ujasiri wa kuichachafya hii serikali kwa kutujuza mambo ambayo serikali inajitahidi kuyaficha tusiyajue ni Zitto.

Lakini kwa hichi alichokifanya leo, siwezi tena kumuamini wala kumchukulia serious.

Analalamika kwamba Magufuli na serikali yake ameirudisha nchi nyuma kisiasa kwa chuki zake kwa wapinzani, wakati hata yeye ana siasa za chuki tena za kitoto sana.

Nadhani leo ni watu wengi sana tumemshusha vyeo.
jomba na sio wewe tu umemshusha cheo hata watu wa jimboni kwake wanasubiri kumshusha cheo kwenye boksi la kura..hapo mwakani..subiri uone yatakayompata. namsikitikia sana dogo..
 
Km huamini Muulize Mwakyembe aliponea wapi? alikuwa afe! anatoka unga tuuuu! wa kutosha. mimi ni CCM, nitagombea ccm. ila nimekataa kulamba viatu kiunafiki..

lakn naamini kuna kufufuka ccm ukimwamini Yesu, mwambieni huyu rais wenu aje atubu tu. aone km hafuffuki
 
Hakuna mwenye mamlaka juu ya afya na uhai wake. Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayetupa vyote hivyo. Hivyo hatupaswi kujivunia juu ya afya zetu au uhai wetu, wala hatupaswi kufurahia wenzetu afya zao zinapopata matatizo hata kama tutakuwa na tofauti kimitazamo/kifikra!

Nimesikitika kwa baadhi ya watu wanaoshabikia kuhusu tetesi juu ya afya ya rais wetu!
Achilia mbali upendo tunaohubiriwa kwenye dini zetu, kuna ile hali ya ubinadamu ambayo ni natural hiyo nayo wanaikosa?

Wengine wanadhani kupata matatizo ya kiafya ni adhabu kwa sababu wanazozijua wao. Je wewe au kwenye familia yako au ukoo wenu hakuna mwenye tatizo la kiafya? Kama wapo unadhani ni kwa sababu wamefanya machukizo kama unavyofikiria kwa mwenzio kwa hiyo wanaadhibiwa? Kuna wengine kiafya hatuko wazima na wengine tumepoteza wapendwa wetu. Je na sisi tunaadhibiwa au wapendwa wetu waliotutangulia ni kwa sababu walikuwa wakosaji sana?

Nimesikitika sana kwa response ya baadhi yetu baada kuwepo kwa taarifa za uvumi juu ya tetesi za afya ya rais wetu!

Kibusara kabisa hata kama mtu mna tofauti naye kwenye suala kama hili ni vema ukawa kimya kama utashindwa kutoa pole au kufanya dua yako kwa kumoumbea nafuu! Hakuna anayeijua kesho yake hasa kiafya na uzima, Mungu pekee ajua! Wala afya zetu zisitufanye tukajivuna sana dhidi ya wale wanaopitia changamoto za kiafya!

Mungu ni wetu sote! Tuishini kwa upendo na wala ubaya haushindwi kwa ubaya bali kwa wema!

Mungu amtie nguvu rais wetu na ampe wepesi kwa matatizo yanayomkabili juu ya afya yake na uongozi wa nchi yetu!

Mungu ibariki Tanzania
mungu pia amutie nguvu lissu licha kuvuliwa ubunge wake mungu alilinda uhai wake kwa waliokuwa na nia mbaya ama mamlaka za kutoa uhai
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
We jamaa MNAFIKI SANA..
aibu yako mdogo wangu
 
Nikikumbuka jinsi Tundu Lissu;
●Alivyopigwa risasi Bungeni
●Alivyonyimwa matibabu na Govt
●Alivyonyimwa mshahara
●Alivyoporwa ubunge
Kwa kweli sasa nimeamini malipo ya ubaya ni hapa hapa duniani.
Ukimtendea ubaya mwenzio nawe utalipwa kwa ubaya.
Walivyopiga marufuku hata kumuombea!
 
Kaka ZITTO umefuatilia au Umeshiriki? Moja ya post yako ilikuwa na ujumbe sawa sawa na ule wa KIGOGO. Nilichogundua ulilishwa Tango Pori ukaamini, na gesture yako ulikuwa unafurahia Sana. Ila baada ya kujua ilikuwa tango pori, ukarudi kwa aibu kuandika tofauti kufuta aibu. Ni bora tukafanya siasa lakini tukatanguliza UTU, UNDUGU na Utanzania wetu.
Mwigulu
Mkuu heshma mbele!

Ulipokuwa waziri wa mambo ya ndani, ubinadamu wako ulionekana Ben Saanane alipotekwa? Tena ukizingatia ulisema kuwa ni rafiki yako?

Hivi shambulizi kwa Tundu Lissu haukuwa waziri wa mambo ya ndani?

Ulifanya mambo gani ili kuonyesha kwamba hukufurahia? Mbona wanachama wa ccm na wapenzi wa serikali walishangilia hadi nikajiuliza kuhusu hilo la utu. Tuacheni unafiki wabongo.
 
Nimefuatilia uvumi na mjadala mtandaoni kuhusu afya ya Mheshimiwa Rais wetu. Nina matatu ya kusema:

Mosi: Afya ya Rais wa nchi ni maslahi ya taifa na inapaswa kutofanyiwa soga. Afya ya Rais inahusika na maslahi ya nchi yetu ndani na nje. Tusiuendee uvumi huu kwa papara. Tuwe watulivu, tuipe nafasi Serikali na mamlaka zake zitupatie taarifa kamili na kwa wakati unaofaa.

Inawezekana kuwa katika hali hii ya sintofahamu baadhi yetu tumefanya mambo yanayotafsirika kuombea mabaya kutokea. Binafsi naomba radhi kwa tafsiri hizo hata kama haikuwa nia wala madhumuni.

Pili: Tuendeleze tunu yetu ya utu, umoja na mshikamano ambazo tumeachiwa na Mwalimu Nyerere ambaye tumetoka kuadhimisha miaka 20 ya kifo chake wiki iliyopita. Tusiruhusu chuki kuteka mijadala yetu. Chuki haiwezi kuwa jawabu la chuki. Utu ndio jawabu sahihi la chuki.

Tatu: Ni busara kwa Serikali kuwaondoa hofu wananchi juu ya uvumi huu maana kutofanya hivyo kunazua taharuki inayoweza kuepukika. Ikiwa kweli Rais wetu amepata dharura ya kiafya kama uvumi unavyosema basi haitakuwa mara ya kwanza kwa hilo kutokea nchini.

Watanzania ni waelewa na wenye mapenzi na wenye utu. Tumeona walivyowaombea marais wao Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walipopata matatizo ya kiafya wakiwa madarakani. Naamini wataungana na kusimama pamoja kama taifa kumuombea Rais wetu na nchi yetu.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa ACT Wazalendo
Kibingo, Mamlaka ya Mji Mdogo Mwandiga, Kigoma
20/10/2019
Zitto umeshindwa sana, aibu yako
 
Nikikumbuka jinsi Tundu Lissu;
●Alivyopigwa risasi Bungeni
●Alivyonyimwa matibabu na Govt
●Alivyonyimwa mshahara
●Alivyoporwa ubunge
Kwa kweli sasa nimeamini malipo ya ubaya ni hapa hapa duniani.
Ukimtendea ubaya mwenzio nawe utalipwa kwa ubaya.
Hakika na kweli, wote waliodhulika kwa maagizo yake nao ni binadamu
 
Kaka ZITTO umefuatilia au Umeshiriki? Moja ya post yako ilikuwa na ujumbe sawa sawa na ule wa KIGOGO. Nilichogundua ulilishwa Tango Pori ukaamini, na gesture yako ulikuwa unafurahia Sana. Ila baada ya kujua ilikuwa tango pori, ukarudi kwa aibu kuandika tofauti kufuta aibu. Ni bora tukafanya siasa lakini tukatanguliza UTU, UNDUGU na Utanzania wetu.
Mwigulu
Anasikitisha sana huyu mwanasiasa mwezio, sasa sijui hapa mnawafundisha nini wanainchi kama sio kufuata kile mnachokifanya nyie.

Saint anne
 
Wanatufundisha tuendelee kuchagua CCM milele Maana wao Ni wa hovyo kuliko hata hao CCM.
Pia wanatuonyesha walivyo na uchu na madaraka ,kwa vyovyote vile watakuwa wakuchumia matumbo tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom