ZITTO: Sitopokea posho ya 300,000 kwenye mbunge la Katiba

ZITTO: Sitopokea posho ya 300,000 kwenye mbunge la Katiba

Status
Not open for further replies.
Amwambie na mama yake Shida Salum asipokee tuone UMWAMBA WAKE.
 
muvi zimeanza where is my coke..........!!!!!!!:smile-big::smile-big:
 
Bwana Mzigo mi naimbaaa..
Nitoke vipi eh...
Siku nyingi najiulizaaa
Niwapo mjengoni eeh!..Mpate kunielewa aah!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Teh teh teh bwana mzigo anakazi ameshakufa kisiasa..
 
Watu bana, wasioweza kuyafanya wao wenzao wakifanya wanalalamika. Sasa kisa cha kumkandia huyu kijana kisa amesema hapokei posho ya kukaa ni nini hasa? Nyie kama hamuwezi kuacha si muendelee kupokea kwani nanyi kawazuia?
 
Kati ya wanasiasa wazalendo tanzania ambao bado wapo hai nadhani amebaki zitto pekee wengine wote ni waganga njaa na wapo kimaslahi zaidi. Natamani siku moja huyu mzalendo ashike nchi ili atuongoze kujenga taifa la kizalendo
Kweli mzalendo na majina ya watu walioweka pesa uswiss..
 
Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg



Zitto akilejea barua yake ya 2011 akiwa anaongea na mwandishi wa gazeti la majira amesema hatapokea posho yoyote kwenye hili bunge la katiba. Zitto amesema ametumwa na wanakigoma kuja kuandika katiba wala sio kipokea posho.
Zitto ameongezea kuwa kuwa huu ni wizi kwa wananchi yaani mwalimu analipwa kati ya 200000 mpaka 300000 kwa mwezi wakati wabunge wanapokea kwa siku

usidandanyike, kwani malipo aliyolipwa na CCM ili kusaidia kudhoofisha juhudi za wananchi za kujitoa kwenye makucha ya watawala wasiojali wapiga kura wake zinamtosha hata kama hatarudi bungeni kabisa! ILA KWA GHARAMA ZA MAISHA YA WATANZANIA WALALAHOI !
 
Zitto anaweza kuwa na lengo la kuokoa fedha za umma lakini angeweza kusaidia zaidi kama angewashawishi wajumbe wenzake wa bunge la katiba kupokea angalao nusu ya kiwango hicho cha posho kwani ni kikubwa sana ukilinganisha na maisha yetu ya sasa. Posho hii kubwa inaweza kupelekea kutungwa kwa katiba ya matajiri.hivi mkulima au mfugaji,au mlemavu kwa posho hii wataweza kuwakumbuka waliowaacha maeneo yao kwa kuwatetea ipasavyo kwenye hilo bunge la katiba? Pia napenda kumkumbusha ZITTO asisahau kuhoji kwenye hilo bunge la katiba juu ya kauli ya mkuu wa nchi kuwataka wanachama w chama chake kuwapiga wanachama wa vyama vingine pindi zinapotokea tofauti kati yao.
 
What's 300, 000 wakati una uwezo wa kukodisha shangingi kwa miaka from one of the most expensive lawyers around -Nkono? Siasa inalipa jamani?
 
Binafsi naunga mkono hoja! Mabarabara mengi hayapiti hasa vijijini, lakini watawala wanaponda raha tu!
 
Zamani kidogo wakati JF inaanza kulikua na mijadala mizuri kweli na yenye akili, lakini siku hizi hata punguwani wanachangia humu ndani tena wengine kwa matusi ya nguoni kabisa. Nimeona mjadala kuhusu Zitto Kabwe kukataa posho, lakini kwa upungufu wetu wa hekima na mawazo tunamshambulia na mama yake eti kama vile wote wana akili moja na msimamo sawa juu ya jambo hili. Zitto ni Zitto na Shida Salum ni yeye kama yeye kama ilivyo kwa Ndesambulo na Lucy Owenya, we can not put them in same basket.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom