Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Zitto: Ushauri wangu kuhusu Mlipuko wa Korona

Nililiwaza hili, wakina Zero IQ na biashara ya kuchakata viazi kuwa chips itabidi waende likizo bila malipo kwa siku 14.
 
Ndio fikra za viongozi wetu wanadhani kila mtu analipwa tarakimu za mishahara yao na wakishaangalia international news yanayotokea huko wanadhani na sisi yanatuhusu.

Ata ikitokea panic buy Tanzania aiwezi dumu wiki moja watanzania walio wengi hiyo hela ya kufanya monthly stocking tu shida, ya miezi miwili ndio waitoe wapi; wakati vibarua wanaishi from hand to mouth.

Get back to the real world changamoto itabaki kwenye sabuni za kuoshea mikono na sanitizers.
 
tilburg1,
Ndio maana ndugu yangu nina sema vitu vingine ni unsustainable kama kuna kuangalia old age people ambao ni vulnerable kwa huu ugonjwa, kuna nurses , kuna ulinzi na usalama etc, hata sisi huku bongo kuna vitu hatuwezi kuhimili labda iwe kwa nguvu za asili au matokeo ya hatua za wenzetu kama ndege kutokuja
 
Serikali ina akiba ya chakula cha siku 3???

This is absurd!😱nchi hii tajiri...utajiri gani kama hatuna hifadhi ya kutosha ya chakula kwa wiki 1??..

Everyday is Saturday.....................😎
 
Ungesema wafanyakazi wa utalii wapewe likizo ya kulipwa hata nusu mshahara ungeeleweka, Serikali iwafidie kwani ndio ilileta corona
Trump ametangaza dola 1000 kila familia Marekani leo na zile zenye watu wengi wataongezewa dola 500.
Hao ndio wanajua thamani ya mwananchi.

inaonekana wewe hata hujui umuhimu wako wala majukumu yako katika nchi yako.
Pathetic
 
Kiuchumi, sekta nyingi sana zitaathirika, na ajira nyingi zitaatirika. Tukianzia sekta ya usafirishaji, migahawa, michezo n.k Hivyo kama ni suala la kungiza fungu la fedha kwenye uchumi ili kulinda ajira, itabidi liangaliwe kwa upana zaidi.
 
Zitto,
Ukisoma kisha elimu ikawa haikusaidii kufikiri bado tunakuona hujasoma,ukisoma ukatawaliwa na hisia zaidi ya reality bado tunakuona hujasoma.

Zitto umebagaiza maswala ya kiuchumi,hivi kwa mawazo yako ni kweli wakulima wanaathirika katika magonjwa kama haya?..Kuna mkusanyiko gani shamabani ?...Lengo lako ni kutengeneza taharuki ili watu wasifanye kazi na iwepo njaa ili watanzania wafe.Watanzania wakifa wewe ndio furaha yako na ndio malipo yako kutoka kwa mabeberu yanaongezeka.

Suala la wafanyabiashara kufidiwa unatengeneza sympathy kutoka kwa wafanya biashara ili uonekane unawajali,huku ukijua wazi kwenye biashara kuna risk na mfanyabiashara anatakiwa ajiandae na risk kwenye biashara yake.

Serikali makini haiwezi kufidia wafanya biashara
Mengine uliyoandika ulikuwa chooni kwa hiyo siyajibu
 
jd41,
Hii ni pumba,biashara yeyote ina risk na ni lazima utenge fungu kwa ajili ya kupambana na risk.Wafanyakazi walitakiwa wafanye savings,unakula bata unategemea serikali ikagawe pesa kwa natajiri wawekezaji...Mnatumwa nyie na Zitto
 
Zitto, Kwahiyo badala ya kuhudumia wananchi unataka wahudumiwe watalii? Mipaka ikifungwa kutakuwa na watalii kutoka wapi?

Stimulus package itasaidia nini kwa secta ya utalii inayokufa?

Emphasis should be on deseas control by testing, treatment and prevention of wide infection.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto,
corana/covid-19, isifanye kama vile ninavyo ona, sijui tumejipanga kiasi gani katika suala la vifaa tiba. najua hapa kuna viongozi watachukulia hili jambo kisiasa zaidi, hatuoni juhudi zozote za kuelimisha wananchi hata kwa kutumia magari yenye vipaza sauti,

kama wanavyo kumbushiaga kulipa kodi, hakuna nguvu yoyote inayo tumika katika kujadili namna ya kukabiliana na corona na side effect zake kiuchumi, na endapo corona itaambukiza zaidi ya robo ya watanzania, nini kifanyike, hakuna, wanaongelea vitu vyepesi vyepesi tu, lakini gonjwa lipo serious na wakikaa vibaya, litapiga hadi wao wenyewe.
 
Bambushka,
Usipokuwa makini wanasiasa watakupanikisha.
Hakuna nchi yoyote duniani yenye akiba ya chakula kwa kila mwananchi kwa hata wiki moja. Akiba ya chakula huwa ni kwa ajili ya majanga tu na huwa wana hesabu zao wamefanya kulingana na matukio ya nyumba na nchi ambazo zimewahi pata majanga.

Hivyo kuambiwa kwamba chakula hakitoshi kwa siku tatu kwa kila mwanachi ni kweli lakini siyo lengo mahala popote kuweka chakula cha kila mwanachi.

Hili la kusema kwamba tupeleke bungeni lina ukakasi ukiliangalia kwa jicho la tatu. Katika watu ambao hawamuhurumii mwanachi kwa njia yoyote ile huwa ni hili kundi.

Fikiria Bajeti ya bunge kukaa siku tatu na kujadili korona, maana hawa watu hawatakaa bure hata kama taifa linaangamia.

Kada ya afya wana vyama vyao na hawa ndo wanafaa kujadili hili kwa kuwa watakuja na uamuzi wa kitaalamu kuliko kuanzia bungeni.
 
Back
Top Bottom