Ziwa Victoria limewahi kukauka maji yote mara tatu

Mastori Ya Town Ukiwa Umepiga Chibuku Toka Ubungo DSM
 
Sintakaa nisahau enzi hizo. Kulitokea uhaba mkubwa sana wa maji.. Watu wa kona ya Bwiru wanaweza kukumbuka vizuri ziwa lilipokauka. Unaambiwa tulikuwa tunasafiri kwa bodaboda hadi visiwani Ukerewe.
 
Kuna mzee flani nilipiga nae story akaniambia kisiwa cha nyamesiga kule bukoba kilikuwa nchi kavu miaka ya 1957 tu hapa. Na yalikuwa mashamba ya watu. Hata hilo jina nyabesiga nilakihaya na linamaana ya palipobaki. Enye kubaki) na alisema watu wazima walienda misira kwa miguu huku maji yakiwa kifuani tu. Wazee wa ukerewe kabla ya uhuru tu hapa waliweza kuvuka kisorya kwa miguu kabisa.
 
Haya ukerewe na bwilo kisiwani pamejitenga hata miaka 80 haijaisha. Kwa hiki kipindi cha miaka chini ya mia kuna visiwa vingi tu vimemezwa na ziwa na kuna sehemu kubwa ya nchi kavu imemezwa huku sehemu nyingine yenye miinuko ikiachwa kama visiwa. Sasa ukiangalia mabadiliko tu ya ziwa victoria ya miaka ya hii 100 ambayo inasimulika tu hata na wazee basi napata picha kuwa ziwa huenda linakua kila siku. Endapo utafikiria miaka 17000 huko nyuma nakubaliana na wanaosema huenda lilikauka ama lilikuwa dogo sana ukilinganisha na leo. Pia kama utatembelea visiwa vingi ziwa victoria na kuviangalia visiwa vyenye milima yenye miinuko mikibwa kama bumbire huko kagera na ukanda wa fukwe za karwazi kerebe na milima ya baadhi ya mazingira kisiwani ukerewe utagundua misitari kwenye miamba inayoonyesha kama maji yaliwahi kuwa pale. Mimi nahisi hili ziwa lilishawahi kuwa kubwa kuliko lilivyo leo pia lilishawahi kuwa dogo kuliko lilivyo leo
 
Sintakaa nisahau enzi hizo. Kulitokea uhaba mkubwa sana wa maji.. Watu wa kona ya Bwiru wanaweza kukumbuka vizuri ziwa lilipokauka. Unaambiwa tulikuwa tunasafiri kwa bodaboda hadi visiwani Ukerewe.
Maji kupungua kwa ziwa victoria kulitokea mwaka 2006 ule ukame uliathiri ghuba ya speak yote kiasi kwamba boat ama mtumbwi wa kivuvi ulikuwa unakwama kwa zaidi ya 500 mita kutoka ulipokuwa unakwamia 2004. Lakini hali ilianza kuwa sawa kwa mwaka 2008 na kuendelea. Kuna watu walikuwa wanatoka kayenze na igombe kupitia katikati ya ukerewe na kisorya hiyo kuelekea visiwa vya msoma ila hiyo njia ilikufa. Maana vyombo vilikuwa havipiti hapo. Ilibaki kidogo tu mara na ukerewe watu waende kwa migiu
 
Kwahiyo "mkodomi" nyie wana bk ndo wamiliki halali wa ziwa victoria?
 
Hekaya
Hizo ni hekaya za abunuasi!
 
Inawezekana.

Ukiwa pale S/M Mazoezi-Butimba kwenye uwanja wa mpira utaona kabisa mahali maji yalipokuwa yanafika zamani ni tofauti kubwa mno na yalipo sasa.

Hata kisiwani Saanane ile miamba inaonesha mahali maji yamewahi kufika wakati fulani.
 
Sasa babu zako waliishi hapo bukoba miaka 17,300 toka sasa... ? Maana mara ya mwisho kukauka ni miaka 17,300 toka sasa
Anadhani labda limekauka juzi!
Kumbe ni inshu ya maelfu ya miaka imepita.

Mababu zetu hata history ya miaka 800 iliyopita hawana, ije kuwa maelfu ya miaka.
 
Kwahiyo wewe unaona uharibifu wa vyanzo vya maji ndiyo kitu pekee kinapelekea Ziwa au chanzo Cha maji kukauka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…