Wanajamvi
naona hisia zimetawala kiasi kwamba hoja za msingi zinaachwa
1. Kuna Christopher Bageni
2. Abdallah Zombe
Kosa la msingi ni mauaji ambalo mahakama kuu haikuona hatia kwa wahusika
Kesi imefikia tamati mahakama ya rufani, Bageni amepatikana na kosa la kuua na hivyo anyongwe hadi afe.
Mahakama haikuona Zombe kama 'accomplice' kwa namna yoyote
Mwendeaha mashtaka hakuweza ku associate mauaji na Zombe
Kumbuka hapa ni mauaji kwanza, kabla ya habari nyingine
Kilichokatiwa rufaa kwa Zombe ni kuhusu cover up aliyofanya
Kimahakama, mwenye jukumu la kuthibitisha tuhuma ni mshtaki.
''The onus is on the complainant to prove guilty''
Inaonekana wameshindwa kwa hilo, Zombe yupo huru
Hata kama tunajua alifanya hivyo, kama haikuthibitishwa mahakamani, mahakama haiwezi kutoa hukumu hisia.