Zombe aachiwa huru, Mshirika wake ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Zombe aachiwa huru, Mshirika wake ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

TUNATAKA TUONE LIVE WAKINYONGWA ILI WENGINE WAOGOPE KUFANYA HUO UJINGA
 
Sawa kabisa.
Lakini Mkuu ukisikiliza mmoja wa mashahidi wakati kesi ilikuwa Mahakama kuu wakati wakiwa katika eneo la mauaji inaonyesha Bageni alikuwa akiongea kwa simu na Mtu mara kwa mara.

Inawezekana kuwa alikuwa Mkuu wake, bila shaka Zombe. Kama upande wa mashtaka wangedukua mawasiliano ya simu ya Bageni pengine Zombe angekuwa matatani
 
Katika vitu ambavyo sitavisahau ambavyo alifanya jk ni hili la kuunda tume ili kuchunguza hakika alinigusa ktk uvungu wa moyo vinginevyo tungeendelea kuaminishwa na polisikuwa hawa wafanyabiashara walikuwa majambazi, lakini swali la kujiuliza ni watanzania wangapi wamepoteza maisha ktk hali kama hiyo ya kusingiziwa na polisi......?
 
Lakini Mkuu ukisikiliza mmoja wa mashahidi wakati kesi ilikuwa Mahakama kuu wakati wakiwa katika eneo la mauaji inaonyesha Bageni alikuwa akiongea kwa simu na Mtu mara kwa mara.

Inawezekana kuwa alikuwa Mkuu wake, bila shaka Zombe. Kama upande wa mashtaka wangedukua mawasiliano ya simu ya Bageni pengine Zombe angekuwa matatani

Unaweza kuwa unataka Zombe ashtakiwe kwa kosa la kusaidia kuua au kutoa ushauri wa kuficha ushahidi.

Haya yote ni maeneo ambayo majaji wamepitia na wameona hakukuwa na ushahidi wa kutosha.

Hata ikiwa nchi ingine ni yule askari aliefyatua risasi ndiye anafunguliwa kesi na labda iwe ksei ya kumhusu gaidi ndiyo inaweza kuwa haina mjadala sana lakini kwa kesi ya kuua kizembe kama hii huwezi kupona.
 
Hahahahaahah Hukumu hio itatekelezwa lini? Hakuna kitu kilichoniuma kama kile aiseee, ni wangapi wamekufa mikononi mwa hawa jamaa wanaojiita Polisi? Shame on them. Anyongwe hadi kufa tena haraka sana
Hili ni fundisho kwa wale wasio na uwezo wa kuchambua amri wanazopewa na mabwana zao. Huyo aliyetekeleza maagizo ya mkubwa wao anaenda kuwekwa kitanzi wakati aliyemuagiza kutekeleza mauwaji akiachiwa huru. HAHAHAHAHAHA
 
Mkuu, umehitimisha vizuri.

Pia ukisoma hii sehemu ya Bageni kujitetea utaona wapi alipatwa na hatia.

Utetezi wa bageni;

Jaji: Mshitakiwa, hebu kwanza nikuulize, hii ripoti ya daktari hapa mimi bado inanisumbua kidogo, Kwanza umesema ulipokwenda katika ukuta wa Posta ulipopelekwa na James hamkukuta damu

Bageni: Ni kweli

Jaji: Jana yake siku mliyokwenda ama asubuhi yake kulikuwa na mvua?


Bageni: Hapana hapakuwa na mvua.

Jaji:Umesema ukutani uliona matundu sita yalidaiwa kuwa ni ya risasi, lakini hawa marehemu walikuwa ni wanne je hizi risasi sita zilitoka wapi au baada ya kupigwa waliendelea kupanda ukuta?


Bageni:Mtukufu Jaji. mimi sikuwepo lakini mapambano mengine zinaweza kupigwa risasi nyingi zikajeruhi chache tu.

Jaji:Na kwa nini hapakuwa na damu?


Bageni: Mtukufu Jaji,hata mimi sijui kuwa ilikuwaje.

Jaji:Umesema matundu yale jinsi yalivyokuwa ukutani inaonekana yalipigwa kutokea pembeni, je katika hali hiyo inawezekanaje kumpiga mtu kisogoni? Alihoji Jaji na kumuelekeza Bageni aegemee ukuta na kisha kumtaka eleze mtu akipiga risasi kutokea upande wa kushoto kwake ni jinsi gani inaweza kumpata kisogoni.


Bageni: Mtukufu Jaji hapa zitampiga hapa,alisema Bageni akionyesha sehemu za begani.

Jaji:Umesema ulipelekewa maganda ya risasi baada ya siku tatu, nne je uliuliza kuwa maganda hayo waliyapata wapi?

Bageni: Niliuliza wakasema waliyatoa Sinza eneo la tukio.

Jaji:Waliya-collect siku hiyohiyo?


Bageni: Nadhani maana askari akipiga risasi lazima a-collect maganda.

Jaji:Kama pale ukutani kulikuwa na matundu sita na walikuletea maganda tisa je haya matatu uliuliza waliyatoa wapi?


Bageni: Ni kawaida Mtukufu Jaji kuwa unaweza kulenga risasi ikapita juu ya kitu ulichokusudia.

Jaji:Kwa maelezo ya James (mkuu wa upelelezi kituo cha Urafiki) ni askari wangapi waliopiga risasi siku hiyo?

Bageni: Hakunieleza ni wangapi.

Jaji:Balistic (Mtaalamu wa masuala ya silaha na milipuko) alisema ni silaha mbili tu ndizo zilizopia ya Saad na ya mshtakiwa wa 12 ,una ‘comment’ yoyote kwa hilo?


Bageni: Mtukufu Jaji, yeye ndiye mtaalamu.

Jaji:Umeeleza kuwa mshtakiwa wa kwanza alikushauri lini mbadili taarifa ya kwenda kwenye Tume ya Kipenka?


Bageni: Mtukufu Jaji, sikuwa specific katika tarehe ila rekodi isomeke siku ambayo alikuwa ‘summoned’ kwenye tume.

Jaji:Kwa nini alikwambia uandike nyingine wakati ulikwishaandika taarifa ya kwako?


Bageni:Aliniambai ifanyiwe marekebisho kidogo ili mambo yawe sawa.

Jaji:Mshtakiwa wa kwanza alisema hapa kuwa polisi hutii amri halali tu je hiyo ilikuwa ni amri halali?


Bageni:Ni halali sababu yeye ni mkubwa wangu

NB: Kuna sehemu kama hapo penye rangi nyekundu ndio palikuwa panatayarisha kabisa jeneza la Bageni.
Richard I wish ningepata kitu kama hicho toka day 1.
 
ivi nyinyi polisi wanavyo uwawa mbona mnakuwa amchongi San domo lenu ilo dah yaan raia sijui mpew nn majuzi tu mbande askari watano wamekufa but watu wanacomment utumbo dah kwan unazan wao awaumii wanavyo kufa .yaan askari wanakazi kubwa San yaan kuwalinda watu wasio wapenda dah mm nashukuru kwa kuachiwa kiongoz zombe but mungu amtangulie uyo oc cid asant
 
Kujua ukweli, ni kaaz kwelikweli.
mkuu,ni kweli kujua ukweli ni kazi kweli kweli kama kujua signature yako kama sio msukuma..mkuu,litendee haki kabila hilo kwa kuweka mazuri yake..dah,nimesikitika sana mkuu..
 
BINAFSI NASUBIRI KUONA KAMA YULE JAMAA, ATAHIDHINISHA UTEKELEZAJI WA HUKUMU, SI MNASEMA NI MTU WA MAAMUZI MAGUMU, LET'S WAIT N SEE.
 
ivi nyinyi polisi wanavyo uwawa mbona mnakuwa amchongi San domo lenu ilo dah yaan raia sijui mpew nn majuzi tu mbande askari watano wamekufa but watu wanacomment utumbo dah kwan unazan wao awaumii wanavyo kufa .yaan askari wanakazi kubwa San yaan kuwalinda watu wasio wapenda dah mm nashukuru kwa kuachiwa kiongoz zombe but mungu amtangulie uyo oc cid asant
Kwenye matukio kama haya ndio nafasi ya kujua uhusiano kati ya polisi na wananchi usisubiri Twaweza.
 
Back
Top Bottom