Sikujuwa kama Jamhuri ilikatia rufaa kesi, ila naomba kujuzwa je washtakiwa walikuwa jela muda wote wakisubiri hii hukumu ya rufaa?
Ushahidi wa kuwatia hatiani umekosekana..!
Inaonekana Li-Zombe lilikuwa likicheza hizi deal kimakini sana.
Kwa mtu yoyote aliyefuatia lile tukio la mauaji atakubaliana na mimi kuwa hapa mahakama imetoa hukumu halali. Huyu jamaa aliyehukumiwa kunyongwa kweli ndie mhusika mkuu kwani marehemu wote walichukuliwa chini ya usimamizi wake na wafikwa na umauti chini ya usimamizi wake. Zombe ni lazima angepona kwa sababu hakuwepo kwenye tukio na hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa alitoa amri wauawe.Kwa kuwa walishinda Mahakama Kuu walikuwa huru na hivyo siyo wafungwa wa kukaa gerezani.
Ila kwenye hii issue ilikuwa tamaa zao tuu, hasa huyo Zombe, na sijui amechomokaje aisee.
Kwa kuwa walishinda Mahakama Kuu walikuwa huru na hivyo siyo wafungwa wa kukaa gerezani.
Wanajamvi
naona hisia zimetawala kiasi kwamba hoja za msingi zinaachwa
1. Kuna Christopher Bageni
2. Abdallah Zombe
Kosa la msingi ni mauaji ambalo mahakama kuu haikuona hatia kwa wahusika
Kesi imefikia tamati mahakama ya rufani, Bageni amepatikana na kosa la kuua na hivyo anyongwe hadi afe.
Mahakama haikuona Zombe kama 'accomplice' kwa namna yoyote
Mwendeaha mashtaka hakuweza ku associate mauaji na Zombe
Kumbuka hapa ni mauaji kwanza, kabla ya habari nyingine
Kilichokatiwa rufaa kwa Zombe ni kuhusu cover up aliyofanya
Kimahakama, mwenye jukumu la kuthibitisha tuhuma ni mshtaki.
''The onus is on the complainant to prove guilty''
Inaonekana wameshindwa kwa hilo, Zombe yupo huru
Hata kama tunajua alifanya hivyo, kama haikuthibitishwa mahakamani, mahakama haiwezi kutoa hukumu hisia.
Kwa mtu yoyote aliyefuatia lile tukio la mauaji atakubaliana na mimi kuwa hapa mahakama imetoa hukumu halali. Huyu jamaa aliyehukumiwa kunyongwa kweli ndie mhusika mkuu kwani marehemu wote walichukuliwa chini ya usimamizi wake na wafikwa na umauti chini ya usimamizi wake. Zombe ni lazima angepona kwa sababu hakuwepo kwenye tukio na hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa alitoa amri wauawe.
Utapigwa kipapai na usipone ooh huyo jamaa hachezewi...kidunia na kipepo we haya weeHata hilo Zombi lilitakiwa likae lupango japo miaka 5
Justice denied.....nimekuelewa Jurist....Justice delayed...
Una criminal behavior kumbe?Dah, Nikimkumbuka Bageni!!!
Hakika jamaa ana damu za watu za kutosha mikononi mwake.
Ilikua ukiingia anga zake anachofanya ni kukuchagulia kosa lokote kama siyo kukupoteza kabisa